Ndiyo maana nchi yangu haiendelei. Kama mtoa maada utakuja kuwa kiongozi wa hii nchi, basi tutegemee madudu hayahaya mnayo yalalamikia kwa CCM. Hakuna budget inayopangwa bila kujua catchment population ya eneo husika. Mpango mkakati wa kudhibiti aina fulani ya ugonjwa lazima uzingatie takwimu ya ugonjwa huo ndani ya jamii husika (Disease Prevalence). Uagizwaji wa madawa katika hospitali lazima useme kwa mwaka umehudumia wagonjwa wangapi, na ni ugonjwa gani umewaathiri watu ewngi(hapa takwimu inatakiwa siyo blah blah). Bila sensa(takwimu halisi), tutakuwa tuna panga budget ambayo siyo halisi(realistic), mwisho wake lawama kwa serikali. Kama leo tusipopata idadi ya watu iliyo halisi hauoni hata hao CDM mtawapa wakati mgumu kama watachukuwa nchi 2015? Watapanga nini wakati watu hamtaki kutoa taarifa sahihi zinazosaidia katika maendeleo.?
Tuache ujinga. Kama tatizo ni serikali iliopo, basi tugomee kila huduma inayo tolewa na serikali: Mfano Tugome kwenda kutibiwa hospitali za serikali, Tugome kuweka fedha kwenye taasisi zote za fedha za serikali, Wafanyakazi wagome kufanya kazi na kugoma kupokea mishahara ya serikali dhalimu, Tugome Kupanda vibuko vya serikali (mfano Kigamboni), Tugome kwenda kupeleka mashitaka mahakamani au Polisi, Tugome, Kwawale wanao tumia umeme wa Tanesco nao wote wanyofoe meter zao au service line ili wasitumie umeme wa shirika la serikali,Watoto wetu au wadogo zetu wanopewa mkopo na serikali nao wagome kupokea mikopo hiyo.Tukifanya hivyo serikali hii ndani ya siku 3 itaondoka madarakani maana nguvu ya umma ya kususia huduma zote za serikali itakuwa imefanya kazi. LAKINI kama huduma hizo bado tutaendelea kuzifuata kutoka serikali hii, basi UNAFIKI TUACHE sensa ikifika tujitokeze kuhesabiwa kwa faida ya serikali tunayoitaka kuanzia 2015.