SENSA: Nini faida yake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SENSA: Nini faida yake?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Vijisenti, Aug 23, 2012.

 1. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Sensa ni zoezi ambalo halina faida kabisa kwa watanzania hususani sensa
  hii itakayofanyika. Serikali isiyowajali wanchi wake itafanya nini baada ya
  kuwahesabu zaidi ya kuwa ni zoezi au njia ya kutengeneza nafasi ya kufisadi
  pesa zetu?

  Nitakapokujibu sina kazi utaniajiri?
  Nitakapokujibu sina mke utaniozesha?
  Nikisema kuna mlemavu utanisaidia?
  Watoto utawalea....................?

  Ajabu! kwa serikali hii hii ambayo memba wengi tumekuwa
  tukiilalamikia leo tunaiunga mkono katika zoezi la sensa kwa
  faida ya nani?

  Tuache unafiki hata kama tunawachukia waislamu ukweli unabaki
  pale pale kuwa sensa haina faida kabisa kabisa kwa Watanzania.
  Hakuna huduma yoyote itakayoboreshwa na serikali ya CCM eti kwa
  sababu ya kuhesabiwa. Wangekuwa wameanza hapo kabla
  tungeamini kuwa ni kweli wana nia nzuri.................

  Labda hawa wanaounga mkono kuna manufaa wanayapata.

  Serikali ya msumbiji inatoa huduma kwa wazee na kusaidia
  mambo mbalimbali ya kijamii. Sensa yake inazingatia kuboresha
  huduma hizo.

  SENSA YETU IMELENGA KUSAIDIA JAMBO GANI?
   
 2. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  i see........
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Duh!!
  Aseeee!!!

  Sasa unataka upewe shule au?
   
 4. Mcharuko

  Mcharuko JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Duh hii nchi unaweza kupasuka kichwa, natamani kuhama!
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Waathiika wa HIV wanapata dawa bure za kuongeza maisha
  shule za kata ni bure hakuna ada....
  elimu chuo kikuu wanafunzi wanakopeshwa

  na mengineeyo meengi ambayo Sensa itasaidia sana
   
 6. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Hakuna faida ya sensa kwa watawaliwa labda
  watawala!
   
 7. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu uko sahihi, Ingawa sensa huanzia ngazi ya kaya. Mkuu wa kaya (awe baba au mama) lazima aelewe ana watoto wangapi, hata kama hana uwezo au anao. Kila mpango huenda na takwimu. sasa kama huoni faida za sensa, yawezekana hata huoni faida za kujua idadi ya watu katika kaya yako. (BE POSITIVE)
   
 8. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,577
  Likes Received: 1,084
  Trophy Points: 280
  Huwa sizipendi sana hoja za vijisenti kwa kuwa zimejaa udini
  lakini kwa leo na kwa muda wacha nimuunge mkono. Sioni kama
  hii serikali ina nia ya dhati, pesa zetu za korosho tumenyanyasika
  sanaaaaaaana, maduka yetu yamechomwa moto na polisi wakati tunadai
  haki zetu, malipo ya awamu ya tatu wanataka watulipe tsh 16 kwa kilo
  Kuondoka kwa CCM ni muhimu kuliko sensa, Hakuna siku shetani anamkuwa
  mwema abadani.
   
 9. S

  Sukula JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 1,214
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  aisee! sasa mtoa mada sijui unashaurije,tukatae kuhesabiwa au unalenga kuhamasisha nini hasa.
   
 10. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wajumbe wengi wa JF ni wakufuata upepo unapovumia hawatumii akili zao kufikiri wao wako kule wanakopelekwa ndiko huenda poleni sana leo munamsapoti kisha akija mtu na mada kama hiyo ya kusapoti sensa nae munamkubalia eee hii kali wapi misimamo yenu wakubwaa
   
 11. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Ni we mwenyewe ndo utaamua kwani kuhesabiwa hakuna faida
  hasara yake ni kupotezeana muda kama kuna shuguli zitasimama
  kwa sababu ya zoezi la sensa. Kama muda upo na hakuna usumbufu
  kwako unaweza kuhesabiwa lakini moyoni lichukulie zoezi hilo kama
  mchezo wa BAO ambao mtu anakula nyjmba wakati katika hali halisi
  hawezi kumeza hata kitasa.
   
 12. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #12
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  dah! kama kuna kaukweli kanakouma vileeeee
   
 13. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Kuna faida gani ya kujua idadi ya watu kwenye nyumba yake
  baba ambaye muda wote yu ashinda kilabuni huku kila kitu ndani ya
  nyumba kikitokana na Juhudi binafsi za mama.

  Hoja hapa si umaskini wa serikali, hoja ni nia ya dhati ya serikali
  ya kuhakikisha kile kidogo kilichopo kinafika katika mikono ya
  wananchi.
   
 14. W

  Wimana JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Vijisenti, ajabu wewe unaendekeza unafiki!
  Unaposema sensa haina faida, ulitegemea sensa ndio ikupe mke? Ulitegemea sensa ndio ikupe ajira?
  Weka unafiki kando, sensa ina faida; kwetu wananchi, vyama vya siasa na watawala.
  Takwimu zitakazopatikana zitawasaidia hata wananchi kuzitafsiri na hata kufanya maamuzi kuhusu hali za maisha yao. Mfano, ukijua mkoa fulani una watu wachache zaidi kwa km, ukitaka kulima patafaa.
   
 15. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Ndio maana wanahimiza watu wakapime kwa hiyari ili wawe
  na takwimu sahihi ya watu kama hao. Sensa haiulizi kama mtu
  ameathirika au hajaathirika.
   
 16. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Halafu ukilima unapewa masharti ya jinsi ya kuuza mazao
  yako..... Unadhulumiwa wakati hujasaidiwa pembejeo n.k
  Waulize wakulima wakorosho..... huko watu wa sensa wakienda
  huwa wanazomewa ktika baadhi ya maeneo.
  SENSA NI MUHIMU LAKINI SI KWA SERIKALI YA CCM.
   
 17. Mcharuko

  Mcharuko JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mtoa mada umenifanya nitafakari upya, Serikali hii inashindwa
  kuboresha hata hospitali zetu, hili halihitaji sensa, Duuh. Madaktari
  wanalalamika Hospitali hazina vifaa, Sidhani kama barabara mbovu
  nazo zinahitaji Sensa duh ipo kazi.
   
 18. W

  Wimana JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Sasa hapo kwenye kudhulumiwa sensa inahusika vipi? Huoni kuwa itakuwa imekusaidi kufanya maamuzi sahihi? Kukataa kuhesebiwa hasara yake inakurudia wewe mwenyewe.
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye blue,,,umesoma bure kwenye hizo shule au umehadithiwa,,,,,,,???????kama hujui kaa kimya,,,,,KARUME K£ng€ wewe usidanganye hapa
   
 20. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kama waislamu wangekuja na hoja hizo nne kama zako, hata mie ningevaa kibandiko na makubazi kwenda kuwasikiliza. Lakini wao hoja yao ya msingi ni "sisi wengi" na "wao ni wachache"

  Sasa kama wao ni wengi wanatakia nini kipengele cha dini?
  1. Ili tuwaajiri.......?
  2. Tuwatafutie wake.......?
  3. Tuwasaidie waislamu tu walio walemavu........?
  4. Tulee watoto wa waislamu tu.......?

  Hatuwachukii waislamu isipokuwa tunasema sensa ya waislamu ifanyike misikitini wanakoswali.

  KWELI SENSA HAINA MAANA VIJISENTI!!!!!!!!!!!!
   
Loading...