Serikali isijibebeshe mzigo mzito zoezi la sensa

G-Mdadisi

Senior Member
Feb 15, 2018
157
99
Anaandika Gaspary Charles.

Ukifuatilia kwa jicho la ndani namna mwenendo wa uhamasishaji jamii zoezi la Sensa ya watu na makaazi linavyoendelea kuchukuliwa nchini utagundua kuna jambo haliendi sawasawa eidha kwa makusudi au bahati mbaya na linahitaji kurekebiswa mapema kabla ya siku yenyewe ili kufanya zoezi hili kufanikiwa kwa kiwango kikubwa na watanzania wote wanahesabiwa.

Mpaka sasa ukidadisi vizuri utabaini kwamba zoezi limebebwa zaidi kwa mtazamo wa kiserikali kutokana na kundi lililo msitari wa mbele zaidi kwenye uhamasishaji na utoaji elimu zaidi ni viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya mtaa na hata serikali kuu, wakiongozwa na kamisaa wa Sensa kitaifa, Anna Makinda kwa Bara, na Balozi Moh'd Haji Hamza kwa Zanzibar, maDC, DED, RC nk. na kwa mbali kabisa Chama cha Mapinduzi CCM.

Ni wazi ushiriki wa Asasi za kiraia katika uhamasishaji wa watu bado ni mdogo na pengine hii inatokana na namna ambavyo mamlaka zimeratibu zoezi hili imepelekea asasi kujiona mchango wake ni mdogo katika zoezi hili, na hivyo kushindwa kujitokeza mbele kusaidia ufikishaji wa elimu moja kwa moja.

Ukifungua TV, ukasikiliza radio na kusoma magazeti na mitamdao ya kijamii, habari kuu ya Sensa ni kuhusu kamisaa wa Sensa kitaifa Mhe. Makinda au Balozi Hamza wa Zanzibar ambao wamefunga kambi na kutembea nchi nzima mkoa kwa mkoa kuhakikisha jamii inafahamu umuhimu wa kuhesabiwa, jambo ambalo linatafakarisha na kutia mashaka juu ya uwezekano wa watanzania wote kufikiwa na elimu hii.

Ikiwa ni karibu siku 40, takriban mwezi mmoja tu umebaki kufika August 23, Vyama vya siasa hasa upinzani vipo kimya kuhusu zoezi hili, Asasi za Kiraia zipo kimya. Hii si sawa hata kidogo, hili ni zoezi ambalo linahitaji ushiriki wa kila mmoja kwa nafasi yake.

Licha ya juhudi na kazi kubwa inayofanywa na viongozi wandamizi wa serikali, zoezi hili linahitaji ushiriki wa makundi yote katika ufikishaji wa elimu ili lifanikiwe kwa ukamilifu na sio serikali kujibebesha mzigo ambao sekta binafsi kupitia asasi za kiraia kama wadau wa maendeleo wangeweza kusaidia kwa kiwango kikubwa.

Hili ni zoezi la kitaifa, sio la serikali, chama wala kundi fulani.

JIANDAE KUHESABIWA.
 
Shida iko wapi? Au unatamani kulamba asali mkuu? Kwa dunia ya Leo vyombo vya habari na mitandao ya kijamii inatosha Sana kuwa nyenzo ya kufikisha habari Kwa jamii,tena Kwa haraka na Kwa gharama nafuu.

Endelea kufanya shughuli zako mkuu.
 
Shida iko wapi? Au unatamani kulamba asali mkuu? Kwa dunia ya Leo vyombo vya habari na mitandao ya kijamii inatosha Sana kuwa nyenzo ya kufikisha habari Kwa jamii,tena Kwa haraka na Kwa gharama nafuu.
Endelea kufanya shughuli zako mkuu.
Januari Makamba aione hii, amesema anaanza ziara ya siku 21 kutembelea mikoa 14 ili kujua kero za wananchi kuhusu wizara yake.

Kwenye mitandao ya kijamii kuna kero za kutosha kuhusu TANESCO na upandaji wa bei ya gesi na mafuta, haihitaji kufanya ziara juu ya hilo. Labda ishu ni kuhalalisha per diem tu
 
Njaa mbaya! Zoezi la Sensa ni la kiserikali asikuambie mtu. Hapo unataka nawe ulambe Asali tu
 
Shida iko wapi? Au unatamani kulamba asali mkuu? Kwa dunia ya Leo vyombo vya habari na mitandao ya kijamii inatosha Sana kuwa nyenzo ya kufikisha habari Kwa jamii,tena Kwa haraka na Kwa gharama nafuu.
Endelea kufanya shughuli zako mkuu.
Huyu anatafuta hela tu. Wapi na wapi NGO au Vyama vikashiriki kuhamashisha Sensa. Hajui kuna sheria ya Sensa ambapo usipotoa taarifa acha kukataa kuhesabiwa unafungwa? Sensa ni zoezi la kutafuta takwimu kwa ajili ya kupanga maendeleo ya nchi. Si la hiari
 
Vyama vya upinzani haviruhusiwi kufanya mikutano, nchi hii haiwahusu vinginevyo watakamatwa kwa kosa la kuwatangazia wananchi wakati wao si serikali.
 
Back
Top Bottom