Sensa: Hotuba ya Rais Kikwete, yatokanayo

Sensa: Hotuba ya Rais Kikwete, yatokanayo

i wish angetoa takwimu za kweli tusikie,otherwise RC,TBC,wikipedia ni wakweli.
 
JK asianzishe moto wa hivo, utamshinda!
Asitafute kumridhisha Ponda na regime yao wanayoota kuipandikiza nchini!
Nchi imemshinda sasa anataka kuiingiza nchi kunako machafuko ili apate namna ya kujitetea!
 
Du, Inaonekana mmekasirika sana JK kushindwa kuwapa sapoti kwenye kukataa kuhesabiwa
 
amewakemea kwa kutoa takwimu za uongo, je wamefanya haya kwa faida ya nani? kama ni kuhesabu hesabu waumini wako ni lini wakatolini wakawahesabu waislam?.

Mkigoma. Haya tutangaze kuanzia leo 26.08.2012 Waislamu ni 70% ya Watanzania wote. SO WHAT???
 
Kikwete Hajui pa kushika.
Sina uhakika kama ana asylum baada ya kuondoka madarakani?
 
Gari bovu hata upake rangi kwa china bado litaendelea kuwa bovu tu, dawa yake ni 2015 kuwamwaga ili mkajipange upya
It was worthy listening President JK Delivering one of his greatest speechs."I listened to what I exactly wanted to listen".
The President was very sensitive on the issue, very explainative,the speech was very balanced,never threw blame to either sides.The body languange was absolutely perfect.The timing was right.
Cant wait to be counted!!!

Thank you.
 
Jamani ! Kwa hiyo kama muda na maandalizi yangeruhusu kipengele cha dini kingeingizwa katika suala la sensa.

Naweza kuipata hotuba yote ya Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa kuhusiana na jambo hili?
 
Mimi nadhani ingefungiwa TBC kwa kutoa takwimu za uongo na kuzua mtafaruku wa kipengele cha dini
 
Udhaifu wa Jakaya umejidhihirisha zaidi leo wakati anahutubia taifa juu ya sensa, alijichanganya aliposema kuwa serikali ilishafanya maandalizi ya sensa kwa kipindi kirefu hivyo kwa muda huu si rahisi kuingiza kipengele cha dini, wakati awali alishasema kuwa serikali haipangi maendeleo kwa kufuata dini wala kabila za watu na kwamba wakoloni ndio walikuwa wanahesabu watu kwa makabila yao na dini zao. Wanajamii JK anaamanisha nini juu ya hili suala mbona anazidi kudhihirisha udhaifu wake?

Hiyo mipango ya muda mrefu hawakujua kua jambo hili na ni muhimu, lina wagusa wapagania uhuru wa nchi hii ambao, walimvisha Nyerere kofia na akafunga ili apate Uraisi. Yeye mwenyewe si alikiri, au hamkumsikia. ALIPOPATA URAISI AKURUDI KANISANI. Kama walikosea kwanini wasirekebishe. KUCHINJA PUNDA MILIA NA KUENGEZA ATTACHMENT TU YA SWALI MOJA, NI IPI DINI YAKO, LIPI RAHISI.? SASA HUYU MHESHIMIWA HANA LOLOTE ANAJIKOMBA TU ILI ASTAAFU BILA KULAUMIWA AENDELEE KULA KUKU. KWA TAARIFA YAKE, TUZO YU MORE IBRAHIMU KESHA IKOSA. ILE TUZO IS BASED ON PERFORMANCE.

 
Kiongozi wa kwanza duniani kushindwa kusimamia zoezi la kuhesabu watu wake...
Huyu jamaa ni janga la kidunia, huu udhaifu wa JK unatokana na mfumo kristo kutawala nchi yetu.

Hapana jamani, hizi sio kauli za watu wastaarabu.
 
ndio madhara ya kutumikia mfumo kristo, ni lazima mwisho ukose hoja, Tuna HOJA NA SABABU ZA MSINGI, HATUHESABIWI

Mfumo Kristu, Mfumo Kristu, kila siku yaleyale!
Alikaa Mwinyi miaka 10, mbona hakuuvunja?
Mbayuwayu ana miaka 7, why asiukomeshe?
Waislam wamekuwa makamu wa Rais, toka Karume mkubwa hadi leo Dr Bilali,
mbona hawaukomesh?
Kawawa amekuwa Waziri mkuu miaka mingi, why hakuukomesha?
Tena kina Mwinyi na Mbayuwayu ndo wameuimarisha, tazama Mwinyi, alikuwa na ma PM watatu, wote Wakristu!
JK anao wawili hd sasa, wote Wakristu.
Someni enyi watu, acheni kulalamika.
 
kila mtu anamadhaifu yake huku duniani ama we huna?
ni kweli ila tatizo udhaifu wake unaangamiza taifa. Anataka kutwambia kama muda ungetosha sasa kipengele cha dini kingeingiza. Tatizo la jk waislam anawaogopa sana hawambii ukweli.
 
Ni rahisi sana kumpuuza Kikwete kwa kila anachosema au kufanya, lakini ninaweza kukuhakikishia sio mjinga hivyo kama wengi wetu tunavyodhania, na kama kweli ameongea hivyo usidhani ni mjinga, Kikwete ni mwanasiasa na anajua anachokifanya na mwisho wa siku utaona nani ni dhaifu yeye au sisi tunaopinga sensa kwa maana mwishowe wote tutahesabiwa na kubaki kuapia tu kwamba Sensa ijayo haki hapa patachimbika hatahesabiwa mtu,kama vile tunavyosema we ngoja 2015 ndio watatujua, ikifika 2015 oktoba tutaandamana kidogo tutasahau tutamkubali raisi mpya wa CCM na kuanza tena we ngoja 2020 ni kiama cha CCM hawatoki tumeshachoka! Lakini mwisho wa siku Kikwete gets what he wants, sasa sijui dhaifu ni nani?


hapo umenena mkuu sio kwamba KIKWETE ni MJINGA ila huwa anajitoa ufahamu(uelewa) kwa muda fulan TU
 
Kama mmemsikiliza vzr na bado mnagoma nyie si watanzania na ima nyie ni mahafidhun fin kulyati
 
Wangeingiza cha Dini tu,nami na wanangu tungegoma mpaka waingize kipengele cha MAJI na UMEME vinakatika mara ngapi!.
 
Udhaifu wa Jakaya umejidhihirisha zaidi leo wakati anahutubia taifa juu ya sensa, alijichanganya aliposema kuwa serikali ilishafanya maandalizi ya sensa kwa kipindi kirefu hivyo kwa muda huu si rahisi kuingiza kipengele cha dini, wakati awali alishasema kuwa serikali haipangi maendeleo kwa kufuata dini wala kabila za watu na kwamba wakoloni ndio walikuwa wanahesabu watu kwa makabila yao na dini zao. Wanajamii JK anaamanisha nini juu ya hili suala mbona anazidi kudhihirisha udhaifu wake?

dah!! kwa kweli kuna watu wana bahati hapa duniani, huyu jamaa ana bahati sana ya kuwa rais, kwa sababu nionavyo mimi, hata ukurugenzi wa halimashauri hakustahili. sana sana alifaa kuwa mwenyekiti wa serakali ya mtaa. NASEMA HIVI SIO KWA SABABU NAMCHUKIA, NDIO UWEZO WAKE KIUNGOZI NA KIUTENDAJI, uwezo wa huyu mshikaji ni wa chini sana. ndo maana siku hizi nashindwa kujua uwezo wa NEC ya ccm kwa ujumla wake, inakuwaje mna-mpa madaraka makubwa kama haya mtu mwenye uwezo mdogo kama huyu??? ni bora Magufuli sio huyu jamaa. ingawa ccm ni janga la kitaifa.
 
Mfumo Kristu, Mfumo Kristu, kila siku yaleyale!
Alikaa Mwinyi miaka 10, mbona hakuuvunja?
Mbayuwayu ana miaka 7, why asiukomeshe?
Waislam wamekuwa makamu wa Rais, toka Karume mkubwa hadi leo Dr Bilali,
mbona hawaukomesh?
Kawawa amekuwa Waziri mkuu miaka mingi, why hakuukomesha?
Tena kina Mwinyi na Mbayuwayu ndo wameuimarisha, tazama Mwinyi, alikuwa na ma PM watatu, wote Wakristu!
JK anao wawili hd sasa, wote Wakristu.
Someni enyi watu, acheni kulalamika.


Mkuu

Jamii forum tunalumbana na watanzania wa aina mbalimbali na ufahamu wa aina zote (lowest - highest)

Miaka ya Mzee Mwinyi ukijumlisha na ya Kikwete inakalibia 20. Kagame kaibadilisha Rwanda kwa muda mfupi sana chini ya miaka kumi.

Lakini hapa kwetu kwa sababu za wachangiaji wengi wanachangia kishabiki nivigumu kuuona ukweli, zinabaki lawama za wasionauelewa. Na huu udhaifu wa kuwa na makundi ya kupingana kwa ushabiki tukiacha ukweli kando unatupeleka kubaya, tukijifanya hatuna akili nk tutabaki kusema siku zote
- Mfumo kristu, mou, necta, tugawane nafasi sawa za kazi, watu wasile hadharan mwezi mtukufu, hatuhesabiwi sensa, na bado katiba italeta balaa si mchezo.


Ukitazama kwa undani zaidi lawama hizi kwa kiasi flani utaona wachangiaji wakichangia kwa jazba, ushabiki na bila hoja za msingi. Lakini ndio tanzania yetu na tunaojadiliana ni sisi wenyewe kama watanzania kwa ujumla wetu.


Tuvumiliane, tuelimishane na tujadiliane kwa upendo la msingi tu ni levels and capacities of understanding are in an indefinably range, hence patience and tolerance are highly recommended
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom