Hakuwa na jinsi kwani hoja za Waislamu si nyyepesi kama wengi wanavyodhani.Nimemsikiliza na nimemwelewa vizuri,yaani JK hana msimamo kabisa, anajikanyaga kwenye mambo ya msingi kama haya, mara ilikuwa wakati wa ukoloni wanahesbu raia kwa dini na makabila yao mara serikali imejipanga kwa muda mrefu na sasa ndugu tafsiri yake ni nini kama si kwamba kwa sasa haiwezekani suala hilo kuingizwa kutokana na muda? hana msimamo huyu DHAIFU, kamsikilize tena tbccm lazima watarudia hotuba yake, nahisi wataifanyia editing kwai yale madudu siyo kabisa!
Serikali ilifanya makosa makubwa kukubali na kuachia taasisi zake kama idara ya utalii kuweka katika website yao asilimia ya watanzania kwa misingi ya dini,na hapa ndipo ambapo Waislamu wamemshika pabaya.
JK si dhaifu kama tunavyowaza ila anajua kwenda na wakati.Kumbuka alipo diffuse tension ya Zanzibar wkt isivyotarajiwa akamteua Ghrib Bilal kuwa mgombea mwenza.
Angalia alivyokubali kuandaa katiba wakati haikuwa katika ilani yake.
Angalia alivyowapeleka kina Mramba mahakamani hata kama watatoka yeye keshanawa mikono.