Selfika na JF: Snap it. Show it

Wanaume wanaopigwa na wake zao wana mkutano kesho kule Kigamboni. Muende huko nao mkawape maneno ya kutia moyo
Binafsi ndoa au mahusiano ya minyukano ya makonde ikiwa kwa Me au Ke.. Hayana maisha marefu na huwa ni kutaabika sana kwa ambae anajipa moyo wa mabadiriko katika upande mmoja. Mwanamke ikifikia hatua ananyoosha hata kofi kwa mwenza wake, basi hayo mapenzi na yafe
 
Kuna msichana mmoja alinipiga ngumi, sijui ni ngumi ile sijui ni kitu gani, alinipiga usoni miwani ikavunjika, daaahhh, aisee nilikunja ngumi kwanza iliyoshiba, nikaivuta nyuma huku nimemshika nguo kifuani, yaani nilivuta ile ngumi iliishia hewani anaiangalia sikumpiga, huku nikiwa na hasira sana, niliondoka machozi yakinilenga kwa ile hasira.

Kuna wanawake huwa wanajaribu kukufanya uwapige au uwatukane muanze kutukanana na hii inasababishwa na baadhi yao wanatokea kwenye mahusiano ya namna hii, unakuta watu waliokuwa nae au familia anayotokea kuna mambo hayo.

niliondoka hatukuonana kwa siku kama 4, hakuwahi kunitukana wala kujaribu kunipiga, nilimfundisha mapenzi sio ngumi wala kutukanana..

Mkuu we acha tu mahusiano yapo very complicated usizungumzie upande mmoja tu.
 
Duh! Mahusiano ni kama chemical equation, mkikosa balance kinachotokea mashudu.. Ukifanya uchunguzi wa ndoa na mahusiano kwa miaka hii ya karibuni rudi nyuma kwa 10 10 utapata pucha kamili

Ebu vuta picha ungempiga ngumi alafu akaanguka akafa ingekuwaje πŸ˜…πŸ˜…
 
Na kipimo kimojawapo cha uanaume ni kuwa na kifua na kuzuia hasira. Mimi mwanamke akiniudhi sawa sawa natoka nje kupunga upepo na kama tuko nje basi naondoka kidogo. Wala sisemi wala kufanya cho chote. Halafu tutaongeleshana vizuri baadaye mambo yakiwa yamepoa.

Sema sasa kuna wanawake wakorofi aisee. Akianza kuongea hanyamazi hata ufanyeje. Hata ukijifanya kuondoka ukirudi unakuta moto uko pale pale. Hawa ndo inabidi uwe mwangalifu sana kwa sababu unaweza kuishia kuua bila kukusudia na njia bora ni kupiga chini tu kimoja liwalo na liwe. Mi mwanamke anipe tu amani basi. Yaani nitoke kazini na kichupa changu cha mvinyo na kizawadi chake tukae zuliani jioni tunywe kwa raha zetu basi. Kama kuna ishu tunaziongea kwa amani na heshima zinaisha, tunasameheana na kusonga mbele. Lakini makelele kila siku aisee hapana. Hata kama ni mzuri kumzidi Boss Lady napiga chini tena bila kuangalia nyuma kamwe!
 
haimaanishi hamuwezi tofautiana .. kupo ila kuna ile hadi unashindwa tofautisha mwanaume yupi na mwanamke yupi ndio nayo maanisha .. kwenye kupiga siungi mkono .. Na kandoa kachanga tu mwana wa Mungu
Mungu Akasimamie kandoa kako Baba Mchungaji. Naamini ulichagua vyema na kwa subira sana na Mungu Akakupa hitaji la moyo wako. Mbarikiwe
 
Hapo ni murder case.
Sema huyo mtoto hatonisahau, ni manzi alikuwa na career yake nzuri tu, mahusiano yalikufa tokana na umbali, maisha mzee daahh..

Ni muda mrefu sasa ummepita lakini nilikutana nae mwaka jana, alinishukuru sana kwa jinsi nilivyokuwa nampa care, i wish ningefanya zaidi lakini ndio hivyo, ilikuwa nje ya uwezo wetu.

Naamini ana furaha huko aliko.
 
βœοΈπŸ“ŒπŸ“Œ

Harakati zinawapoteza, kutaka 50/50 kuna waangamiza. Umemaliza kila kitu
 
Pole ulikuwa unampenda eeh
 
Ni kweli mkuu.
 
Pole ulikuwa unampenda eeh
Yeah! Inaonekana bado ana maumivu. Nadhani karibu sote tuna mtu wa aina hiyo. Mtu ambaye japo mambo hayakwenda kama yalivyotakiwa kwa sababu mbalimbali zikiwemo utoto na kutoyajua maisha sawasawa lakini bado tunaamini kuwa pengine wao ndiyo walikuwa watu sahihi kwetu. Ila ndo hivyo tena hakuna la kufanya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…