Hayo "manguruwepori" hayo yalishamaliza kazi yaliyotumwa kuifanya - kukuandaa na kukuweka tayari. Usingekuwa hivyo ulivyo leo bila ya hayo manguruwe pori. Ungewezaje kuujua upendo wa kweli bila kupitia kwa hayo manguruwe pori? Almasi yawezaje kuwa yenye thamani, imara na yenye kung'ara sana bila kupita katika moto mkali na mgandamizo wa kutisha?