Samahani sn..nilisoma vibaya
Kuhusu inshu ya kuondoa mafuta yasiyohitajika mwilini( cholesterol au lehemu Kwa Kiswahili) hapo inabidi u-sacrifice vitu vingi sn
mahondaw
1.punguza Kula vyakula vyenye sukari nyingi,vinaongeza unene
2.kufunga(fasting) ni Bora zaidi ktk kupunguza mafuta na unene kuliko mambo ya kujinyima Kula wenyewe mnaita diet
3.km ni mlaji wa chipsi mara Kwa mara achana nazo
4.pendelea Kula vyakula visivyo na mafuta mengi..mbogamboga na matunda ni Bora zaidi ktk Kila mlo
5.kama usiku ulikuwa unakula kisha unaenda kulala badili hii ratiba,Kula mapema zaidi kisha ukae Masaa mawili au matatu then lala.Punguza Kula vyakula vya wanga usiku(wali ugali chipsi na hata bia) vinaongeza unene na kitambi
6.MAZOEZI;hapa ndy penye mtihani

..nikuambie Tu ukweli,hapa ndy penye tiba kamili ya kuondoa mafuta,manyama uzembe yanayoshuka kwenye tumboni na kitambi Kwa mtu mwenye nacho..hayo mambo yote huko juu unaweza kuwa umefanya lkn matokeo yasiwe mazuri,lkn Kwa kufanya mazoezi kila siku angalau nusu saa Asubuhi na jioni Una uhakika wa kupunguza walau kilo moja kila siku.nunua zile kamba za kuruka wanauza machinga barabarani.
Mara nyingi naona unalalamika kuhusu kitambi,nikuambie Tu ukweli,hakuna kitu kigumu kukiondoa Kama kitambi.Mafuta ya kwenye kitambi yanaisha taratibu sn na ndy sehemu ya mwisho kupata matokeo.Hata ufanye mazoezi Masaa 24,sehemu ya mwisho kuisha mafuta ni tumboni
Ndy maana wengi wanaofanya mazoezi Kwa lengo la kuondoa kitambi wanakata tamaa mapema,wanaishia Kusema kitambi changu hakitoishi hata nifanye mazoezi,kumbe asichojua ni kwamba tumboni ni sehemu ngumu kuisha mafuta,inahitajika juhudi na moyo ili kupata matokeo..Kazi kwako mrembo,jitahidi utafanikiwa