It's never too late. Jitahidi sana;sio tu kuwa present, bali uwe available to your kids. Na uzuri watoto ni very understanding; ongea nao waambie kwa nini unakuwa mbali nao, watakuelewa tu. Na mawasiliano yamerahisishwa sana siku hizi, wapigie simu, do video calls n.k. Unawauliza habari zao na siku zao zimeendaje, wasaidie homeworks, unawauliza wanahitaji nini; na unamwambia kabisa nimetumia mama hela akununulie kitu fulani; wajue kuwa baba yupo, anatujali na kutuhudumia.
Siku ukipata nafasi ya kuwa nao; make sure mnakuwa na wakati mzuri ambao unaweka alama kwenye maisha yao. Toka nao, shiriki kwenye hobby zao, wapeleke shopping, wasaidie kuchagua vitu wanavyovipenda, omba nao, shiriki kwenye vikazi vyao vya nyumbani n.k. Yaani siku ukiwepo, ionekane kweli baba yupo, jitahidi kufidia ule muda ambao hukuwepo