Selfika na JF: Snap it. Show it

kabisa mkuu wangu, sahii nataka kutega vilipuzi kwenye FX nyingine kwenye miti ya dawa hii consistency yake sio kama FX kunisomesha vitabu kama natafuta PHD no, 3 months tu namtafuta broker anipe changu..
FX ukiweza kuwa mzuri kwenye RM, na ukawa mwenye subira ya kuingia sokoni.. huitaji Phd.. hata 😀😀😀.. kila mtu anajua TA na hata FA.. pamoja na SA.. ila tuna fail kwenye RM kwasababu ya tamaaa
 
FX ukiweza kuwa mzuri kwenye RM, na ukawa mwenye subira ya kuingia sokoni.. huitaji Phd.. hata 😀😀😀.. kila mtu anajua TA na hata FA.. pamoja na SA.. ila tuna fail kwenye RM kwasababu ya tamaaa
mkuu sio tamaa ni njaa, yaani naona $100 inaelea elea kwenye profit na chart haichelewi kuretrace mimi ni nani nisifunge order!?..
 
Kitambi kisikuharibie pozi; hakiwashi wala hakiumi. Yeah mpasuo umekaa penyewe. Mpo vizuri na fundi wako mama. Kongole sana
 
Ulifanya la maana kamanda. Hawa viumbe wengi wao wana vurugu na ni waonevu sana ukiwa mnyonge utaonewa sana.

Kuna scenario moja ilitokea maeneo fulani. Kuna traffic polisi wale wanawaitaga tigo sijui voda fasta wale ambao wakikuambia usimamishe gari ukakimbia wanakufukuzia na vile vipikipiki vyao hadi wakukamate.

Basi bhana kuna siku wakamsimamsha jamaa mmoja jamaa akaona pale aliposimamishwa hakuna sehemu nzuri ya kupaki hivyo akasogea mbele kidogo ili apaki. Wale jamaa wakajua labda sijui anakimbia wakaanza kumfukuzia alipofika akapaki ile anashuka tu wakaanza kumshambulia oo we kwanini tunakuambia usimame unakimbia.

Jamaa hata hajapata nafasi ya kujielezea wakaanza kumtia mateke mara mitama jamaa akawa tu mpole wala hakutaka kusema yeye ni nani. Tena alikuwa amevalia koti jeupe la kidaktari wakamvua wakalitupa chini wakaendelea kumpiga.

Pembeni kulikuwa na kituo cha bodaboda. Wale bodaboda wengi wao walikuwa wanamjua jamaa aliyepigwa ni nani. Basi kwa pembeni wakaanza kuambizana kuwa hivi hawa polisi wanajua wanayempiga ni nani hawajui kama ni boss huyo.

Wale polisi wakasikia yale maneno ya bodaboda wakawa kama wamepunguza kumpiga wakabaki wanajiuliza huyu atakuwa nani mbona hawa bodaboda wanasema hivyo. Wakati wale mapolisi wanaendelea kushangaa yule jamaa akapata nafasi akapiga simu Lugalo kumbe jamaa ni daktari pale Lugalo.

Ndani ya dakika chache tu ilitoka defender Lugalo imejaa ma MP. Wale matraffic wakawa bado wamezubaa tu hawajui kinachoendelea pale pale wakapakizwa kwenye defender wakapelekwa Lugalo.

Sasa wakati wanapakizwa wale bodaboda wakawa wanashangilia wanasema ndiyo wakamateni hao wamempiga boss wetu ona wamemtupia hadi koti lake wamemchafulia. Inaonesha wale bodaboda nao walikuwa hawawapendi wale matraffic na walishawachoka na tabia zao za uonevu.

Polisi wetu (wengi wao) inabidi wajitafakari sana asee hawajiulizi kwanini kila kukicha wanalalamikiwa wao tu yaani hiyo tabia yao ya uonevu wananchi wengi wameshaichoka. Huwa najisemea tu sasa huyo kwa vile alikuwa ni mwanajeshi ndiyo maana wale mapolisi ilikula kwao.

Jiulize ni raia wangapi wanaonewa na kuteswa kama hivyo huko mitaani kwa sababu tu hawana mamlaka yoyote. Ni wengi sana sema tu ni vile hawana cha kujitetea wala pa kusemea.

Watu wanaleta uonevu hadi kwa watu wasiowajua halafu yakiwakuta ya kuwakuta wanaanza kusema wanajeshi wakorofi na wana roho mbaya. Wacha waendelee kujichanganya na kuingia kwenye anga za watu wasiowajua.
 
FX ukiweza kuwa mzuri kwenye RM, na ukawa mwenye subira ya kuingia sokoni.. huitaji Phd.. hata
.. kila mtu anajua TA na hata FA.. pamoja na SA.. ila tuna fail kwenye RM kwasababu ya tamaaa
Tamaa mbaya, nadhani ni kwa sababu ya mitaji mbuzi mategemeo tembo. Tunataka $20 ilipe Kodi, inilishe hotel, inunue tv, ijenge nyumbani, inunue premio nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…