Siyo kwa zile nywele za kukaa masaa yote zinasukwa tu.
Halafu mimi nina phobia na kubadilisha mitindo.
Kipindi nasoma chuo nilikuwa nasuka nywele za aina moja tu!
Sasa kuna watu wakawa wanauliza mbona nywele zako hazifumuki na hazichakai miaka yote,,kumbe mwenzao zikichoka naenda tena kusuka kama zile zile na fundi yule yule.
Kipindi nimeenda graduu yule fundi aliniwahi akasema leo hanisuki nywele ninazosukaga
Alikataa kata kata ,akasema yupo tayari hata kuninunulia weave jingine bure.