Selfika na JF: Snap it. Show it

 

Samahani kama nimekosea kumuweka huyo jamaa hapa. Najua ni msanii na ana dimpozi...na anajivunia kweli kweli... mengine aisee siyajui...

Pointi yangu ilikuwa ni kwamba mara nyingi tunachodhani kuwa ni udhaifu tunaweza kukibadilisha na kuwa jambo jema tu. Na mifano ipo mingi...



Mike Strahan (pichani), kwa mfano ana mwanya. Na mwanya kwa Wamarekani ni sawa na kilema na wengi huishia kuiziba. Yeye walipomwambia kuwa kama anataka kuwa mtangazaji wa TV itabidi kwanza auzibe huo mwanya wake alikataa. Leo hii mwanya ndiyo umegeuka kuwa kitambulisho chake na ana shoo karibu tatu zinazofanya vizuri.

Sasa kama wewe hapo. Mungu ndo kakupa hizo dimpozi. Una nini kingine cha kufanya mbali na kujikubali na kuzifanya ziwe sehemu yako? Hospitali nzima unajulika kama Dr. mwenye dimpozi tayari si ujiko huo? Jibidishe sasa uwe daktari bora kabisa kabisa. Hizo dimpozi zitageuka na kuwa ishara ya weledi katika kazi yako. Gifted hands (with dimples!)....
 
Noted mkuu..Ila umening'ang'ania sn ktk hili😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…