Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

FB_IMG_1637755740783.jpg
 
FAHAMU KISA CHA DISMASI NA UKOMBOZI WAKE.

• Dismasi ni nani?

Dismasi ni mmoja kati ya wahalifu wawili waliosulubiwa Msalabani pamoja na Kristo.

Huyu ndiye yule aliyemkanya mwenzake na kuomba msamaha akiwa Msalabani, na kisha Yesu akamuahidia Mbingu. (Luka 23:42-43).

Inasadikika kuwa Dismasi na Yesu Kristo walizaliwa mwaka mmoja, hivyo wote wakiwa na umri sawa.

Pia hata kukutana kwao pale Msalabani haikuwa ndiyo mara yao ya kwanza, bali Wanateolojia wanatuambia walishawahi kukutana tangu utotoni.

Maana baada ya tangazo lililotolewa na Mfalme Herode, juu ya kuuawa kwa watoto wote wa kiume kule Bethlehemu na viunga vyake. (Mathayo 2:16).

Kwa maelekezo ya Malaika, Yosefu na Mkewe Mariamu walianza safari ya kukimbilia Misri. (Mathayo 2:13).

Hivyo katika safari ndefu na ngumu yenye milima, jangwa na mabonde, Maria na Yosefu walichoka mno kwa safari, na hata Mtoto Yesu pia aliweza kuchemka sana kwa sababu ya kupigwa na jua kali mwilini.

Lakini kwa bahati nzuri, Wazazi hawa wawili walibahatika kuona nyumba na kuomba hifadhi walau wajipumzishe kidogo, kabla ya kuendelea na safari yao.

Hivyo kutokana na hali ya Mtoto Yesu kuchemka sana, waliomba maji wapate kumuogesha ili wampunguzie joto alilokuwa analihisi mwilini. Wakapewa maji lakini maji hayo yalikuwa ni madogo mno kwa sababu ya hali ya jangwa iliyokuwepo pale.

Kadhalika katika nyumba hiyo pia, kulikuwa na mtoto mchanga ambaye ndiye Dismasi, mtoto huyu alizaliwa akiwa na ugonjwa wa ukoma.

Baada ya Yesu kuogeshwa, maji yale yale yalitumika pia kumuogeshea mtoto Dismasi kutokana na shida ya maji iliyokuwepo.

Basi mtoto Dismasi baada ya kuogeshwa maji yale, ukoma wake ulimuacha, Dismasi akapona yaani alitakasikika kabisa.

Lakini kwa bahati mbaya katika makuzi yake, Dismasi akakua huku akiwa na tabia ya unyang'anyi, lakini licha ya uovu wake, Dismasii bado alimtambua Yesu kama ndiye mtu aliyeweza kumponya ukoma utotoni.

Kwahiyo hata walipokutana pale Msalabani, alimjua Yesu kama ndiye Kristo ajaye ulimwenguni, na ndio maana alipopata nafasi aliomba msamaha, na ile neema aliyoipata tangu utoto wake iliweza kumkomboa na kumfanya Yesu amuahidie Mbingu.

Basi nihitimishe kwa kusema kwamba, najua wengi wataniuliza hii hadithi nimeitoa wapi, mbona haiko ndani ya Biblia?

Lakini ninachotaka kueleza ni kuwa, Kanisa Katoliki linajua Biblia vizuri sana na muktadha wake. Na ndio maana tunajua undani wa mambo na visa vingi vya Biblia visivyoandikwa.

...TUMSIFU YESU KRISTO...
Milele amina

Sent from my CPH2059 using JamiiForums mobile app
 
MISS FAITH ODUNSI CROWNED "MATHEMATICS QUEEN" OF NIGERIA AND BEST IN THE WORLD.

The national mathematics centre of Nigeria (NMC) has crowned Miss Faith Odunsi of Ambassador College, Otta in Ogun State Nigeria as "MATHEMATICS QUEEN" for her outstanding performance in the National Olympiads Competition.

Miss Faith Odunsi solved 19 mathematics questions in 60 seconds, and became the best girl in mathematics competition.
26 students of both senior and junior secondary Schools across the country were also given awards in different categories in mathematics science.

Miss Faith Odunsi, 15 years old represented Nigeria at the Global Mathematics Competition, beats China, United States of America, United Kingdom and others and became the world best mathematics student .

Congratulations Miss Faith Odunsi.

Copied from: Aare Adekunle Ayo Bolarinwa.View attachment 2020983
 
Kwanini tuki' concentrate mawinguni tunaona imagine flani ?
Unaona kile ambacho ubongo wako umezoea kukiona. Na kwa binadamu image ya kwanza inayomjia akilini akitazama ombweni ni uso wa binadamu. Kila anakotazama anategemea kuona sura ya binadamu...ndiyo maana hata akimulika makamera yake huko kwenye sayari na ma-galaxy mengine huko kitu cha kwanza anachokiona ni sura ya binadamu. Binadamu anafikiri hata Mungu mwenyewe ana sura ya binadamu!
 
Unaona kile ambacho ubongo wako umezoea kukiona. Na kwa binadamu image ya kwanza inayomjia akilini akitazama ombweni ni uso wa binadamu. Kila anakotazama anategemea kuona sura ya binadamu...ndiyo maana hata akimulika makamera yake huko kwenye sayari zingine na ma-galaxy mengine huko kitu cha kwanza anachokiona ni sura ya binadamu. Binadamu anafikiri hata Mungu mwenyewe ana sura ya binadamu!
kumbe MUNGU ana Sura ya nini km siyo binadamu?

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom