Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

20211124_105422.jpg
20211124_105506.jpg
 
FAHAMU KISA CHA DISMASI NA UKOMBOZI WAKE.

• Dismasi ni nani?

Dismasi ni mmoja kati ya wahalifu wawili waliosulubiwa Msalabani pamoja na Kristo.

Huyu ndiye yule aliyemkanya mwenzake na kuomba msamaha akiwa Msalabani, na kisha Yesu akamuahidia Mbingu. (Luka 23:42-43).

Inasadikika kuwa Dismasi na Yesu Kristo walizaliwa mwaka mmoja, hivyo wote wakiwa na umri sawa.

Pia hata kukutana kwao pale Msalabani haikuwa ndiyo mara yao ya kwanza, bali Wanateolojia wanatuambia walishawahi kukutana tangu utotoni.

Maana baada ya tangazo lililotolewa na Mfalme Herode, juu ya kuuawa kwa watoto wote wa kiume kule Bethlehemu na viunga vyake. (Mathayo 2:16).

Kwa maelekezo ya Malaika, Yosefu na Mkewe Mariamu walianza safari ya kukimbilia Misri. (Mathayo 2:13).

Hivyo katika safari ndefu na ngumu yenye milima, jangwa na mabonde, Maria na Yosefu walichoka mno kwa safari, na hata Mtoto Yesu pia aliweza kuchemka sana kwa sababu ya kupigwa na jua kali mwilini.

Lakini kwa bahati nzuri, Wazazi hawa wawili walibahatika kuona nyumba na kuomba hifadhi walau wajipumzishe kidogo, kabla ya kuendelea na safari yao.

Hivyo kutokana na hali ya Mtoto Yesu kuchemka sana, waliomba maji wapate kumuogesha ili wampunguzie joto alilokuwa analihisi mwilini. Wakapewa maji lakini maji hayo yalikuwa ni madogo mno kwa sababu ya hali ya jangwa iliyokuwepo pale.

Kadhalika katika nyumba hiyo pia, kulikuwa na mtoto mchanga ambaye ndiye Dismasi, mtoto huyu alizaliwa akiwa na ugonjwa wa ukoma.

Baada ya Yesu kuogeshwa, maji yale yale yalitumika pia kumuogeshea mtoto Dismasi kutokana na shida ya maji iliyokuwepo.

Basi mtoto Dismasi baada ya kuogeshwa maji yale, ukoma wake ulimuacha, Dismasi akapona yaani alitakasikika kabisa.

Lakini kwa bahati mbaya katika makuzi yake, Dismasi akakua huku akiwa na tabia ya unyang'anyi, lakini licha ya uovu wake, Dismasii bado alimtambua Yesu kama ndiye mtu aliyeweza kumponya ukoma utotoni.

Kwahiyo hata walipokutana pale Msalabani, alimjua Yesu kama ndiye Kristo ajaye ulimwenguni, na ndio maana alipopata nafasi aliomba msamaha, na ile neema aliyoipata tangu utoto wake iliweza kumkomboa na kumfanya Yesu amuahidie Mbingu.

Basi nihitimishe kwa kusema kwamba, najua wengi wataniuliza hii hadithi nimeitoa wapi, mbona haiko ndani ya Biblia?

Lakini ninachotaka kueleza ni kuwa, Kanisa Katoliki linajua Biblia vizuri sana na muktadha wake. Na ndio maana tunajua undani wa mambo na visa vingi vya Biblia visivyoandikwa.

...TUMSIFU YESU KRISTO...
 
Back
Top Bottom