Selfika na JF: Snap it. Show it

Kuna mtu aliuliza ulipofika Dar kwa mara ya kwanza ulishangaa kitu gani? Jamaa mmoja akajibu kuwa alishangaa daladala imeandikwa Gerezani na watu wanagombania kuipanda ndiyo kama wewe sasa!
 
Bado yeye ni Mungu



Baba Mtumishi unakesha kazini??
Akhsante kwa selfie
, nimefurahi kuuona mkono wa baba mtumishi..bado sasa kumuona baba mtumishi mwenyewe
.. nataka nimuone jamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu aliuliza ulipofika Dar kwa mara ya kwanza ulishangaa kitu gani? Jamaa mmoja akajibu kuwa alishangaa daladala imeandikwa Gerezani na watu wanagombania kuipanda ndiyo kama wewe sasa!
Tangu nimefika Dar hii ni mara yangu ya pili kupanda daladala.

Hakiyanani nimeteseka Leo,yaani Korogwe hadi Kimara mwisho kwa mwendokasi huwa natumia dakika 2 hadi tatu.
Leo nusu saa nzima


Nimeshangaa utaratibu wa kudandia gari kabla haijasimama,na abiria waliofika hawajashuka Bado
.

Nilishangaa pia daladala za Dar hazina maandishi nyuma Na mbele kama Mbeya.

Yote tisa, kumi Zile ngazi za lift zinazotembea,pale City Mall aisee zilinitoa jasho Mno.


Huyo wa daladala ya gerezani


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee pole
Bila kugombania gari haufiki ...
 
Watoto mboga 100 nyie
 

Karibu daslam. Kuna mengi ya kushuhudia ambayo ni ya kushangaza na kuchekesha zaidi ya hayo cha msingi usisepe mapema tu.
 
Ujumbe umfikie pia NDINDA na mtaalam wa kutoa maua and 100 others 😁😁😁😁View attachment 1975050
Mkinipa ulinzi mkali natupa maua yote!!!πŸ™‚πŸ˜πŸ˜‰
Asante sana, kwa sababu umezungumzia ulinzi mkali itakuwa kama ifuatavyo...

1-Nyumba yako tutaizungushia sensors zenye uwezo wa kugundua hata kipepeo akiwa half mile away, sensors zitakuwa na uwezo wa ku detect moshi just in case intruders wataamua kutumia njia hio kupuliza moshi au spray zenye madhara

2-tutaweka sensors na mifumo ya biometric recognition, akija mgeni software zitamgundua hata kwa kutembea tu ukiachilia mbali fingerprint na iris scanner..

3-mafuta, vipodozi, vyakula, malazi, maji, vinywaji itabidi kuchunguzwa na mtaalamu/mkemia kabla hujavitumia.., hata maji ya kuoga...

4-Tutafunga wireless detectors(wireless intrusion detection system), kuanzia simu unayotumia, computer na kila kitu, lazima taarifa zipite kwenye device maalumu ambayo ita decrypt taarifa zote kabla hazijaingia wala kutoka, kwa hio vyote unavyo chat lazima tujue unachat na nani na una browse nini..hio ni kuzuia udukuzi..

5-tutaweka fire proof, tutaweka pia smart home security systems kuhakikisha kila kitu una ki control kwa kutumia simu ya mkononi tu, kuanzia kufunga milango, madirisha, geti, kuwasha taa na kila kitu hata tv..

Kutakuwa na walinzi tofauti tofauti wenye kazi tofauti, achana na wale wenye silaha na miili mikubwa..

wapo njiani wanakuja..
NB gharama zote juu yangu..πŸ™‚, toa ua sasa
 

Karibu daslam. Kuna mengi ya kushuhudia ambayo ni ya kushangaza na kuchekesha zaidi ya hayo cha msingi usisepe mapema tu.
Na hili fukuto la joto kwenye daladala,utadhani tukewekwa kwenye mfuko.
Nashangaa tu miguu inaniwasha kwenye daladala,kumbe ni mbu wananing'ata!


Pameshanichosha.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…