Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia BWANA.
Wakamwambia Musa, Je! Kwa sababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mbona umetutendea haya, kututoa katika nchi ya Misri?
Neno hili silo tulilokuambia huko Misri, tukisema, Tuache tuwatumikie Wamisri? Maana ni afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani.
Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.
BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
KUTOKA 14:10-14
Bwana atawapigania nanyi mtanyamaza kimya[emoji120].
Kama vile alivyonena na Musa,akaawambie wana wa Israeli warudi na kupiga kambi mbele ya pirahtholi,Kati ya Migdoli na bahari.
- ---------------------------------------------------------
Mkuu umenikumbusha mbali,enzi za shule ya J2 tulikuwa na mikutano ya mitaa.
Nilibahatika kuzunguka mikutano kadhaa..nilikuwa sijawahi kosa kwenda.
Hii chapter hasa hiyo verse ya 14 Ndiyo ilibeba kichwa Cha mtaa.
Mashairi,ngonjera,nyimbo na maswali yalitoka hii sura.
Kuna verse pia "Simameni jipangeni mkauone wokovu wa Bwana"imejirudia pia kwenye mambo ya nyakati,2Nyak20:17
Hapa zile nyimbo nakumbuka hadi leo.
Walitujengea mazingira ya kukariri Neno maana tunaimba Neno [emoji3590]
Nakumbuka namna nilivyokuwa nafurahia.
It's more than 15 yrs[emoji3590][emoji120][emoji120][emoji120]
Wazazi msiache kuwapeleka watoto shule ya jumapili.