Selfika na JF: Snap it. Show it

E Mungu nisaidieee

Nikumbushe wema wako nisije laumu
Nikumbushe ukuu wako wakati wa magumu
Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu
Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozi.


Ni rahisi kinywa kujawa na lawama tele
pale mambo yanapoonekana hayaendi
Ni ajabu sana kama moyo unahangaika
Kutafuta majibu
Ajabu sana moyo unapoonyesha mashaka
......
..
.

Nakumbuka wana wa Israel katika bahari ya Sham
Japo walikatiza katikati ya bahari kwa ushindi
Kwa nyimbo nyingi waliimba na kumsifu Bwana
Lakini baada ya kuvuka na kuliona jangwa yalibadilika mambo
Manung'uniko yalisimama
Na kusahau muujiza alotenda Bwana mwanzo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…