Nani kasema?? Mie mwenyewe wale wale tu ndiyo maana nasema wazuri "walikuwa wanahesabika" lakini uzuri unatofautiana kati ya mtu na mtu maana mimi binafsi hadi mwanamke mwenzangu nimuone kama ni mzuri basi nimempitisha kwenye chujio hasa
Yaani sifa nilizoziweka za mimi kusema kwamba huyu mwanamke kweli ni mzuri hata mimi sina hizo sifa ndiyo maana hata mimi sijihesabii kama ni mzuri na wala hata siku moja hauwezi nikuta najisifia kuwa eti mimi ni mzuri yaani sijawahi kujikubali!!