Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

MAOMBI YA KUSIMAMIA YA MUDA WA USIKU( KABLA YA KULALA)

1.Baba,nafunika nafsi yangu,Roho yangu,mwili wangu ,nyumba yangu, wanafamilia wangu na Marafiki zangu kwa Damu ya Yesu.Naweka ukuta wa Moto kando yetu na ninatangaza kuwa nyumba zetu na mali zetu hazitafikiwa na falme za giza,kwa Jina la Yesu.

2.Baba,nakuomba unifumbulie mafumbo yangu katika ndoto zangu,kwa Jina la Yesu.

3.Ee Mungu,Kila Nguvu inayotaka kunihangaisha Kupitia ndoto zangu,naipiga Upofu ,kwa Jina la Yesu.

4.Malaika wa Vita wa Mungu,pindueni kila anaye nishambulia katika ndoto zangu ,mfanye ale nyama yake mwenyewe na kunywa Damu yake mwenyewe kwa Jina la Yesu.

5.Kila tambara,Kila blanketi,kila Gamba la rohoni linalofunika macho yangu ya kiroho ,chomeka Sasa ,kuwa majivu kwa jina la Yesu.

6.Wachawi wanaowinda Maisha Yangu usiku,napangua silaha zenu zote ,nazimaliza Nguvu Sasa kwa jina la Yesu.

7.Malaika wa Vita wa Mungu aliye hai,piganeni na malaika wote wa giza waliotumwa kupigana na Maisha Yangu kwenye ndoto,kwa jina la Yesu.


8.Ee Mungu,Inuka na unipiganie katika ndoto zangu,kwa jina la Yesu.

9.Nguvu ya kuwa na ndoto za kimungu na kuzikumbuka ndoto hizo,shuka kwangu Sasa,kwa jina la Yesu.

10.Nguvu za giza zinazotaja jina langu mida ya usiku,pokea kofi ya Malaika ,achia kwa jina la Yesu.

11.Naamuru kila Mshale wa adui uliolengwa kwenye ndoto zangu upinduke kwa moto kwa jina la Yesu.

12.Nguvu za giza zinazopanda ubaya katika Maisha yangu wakati wa usiku, chomekeni na muachie kwa jina la Yesu.

13.Baba,naomba unipe maono yaliyo sahihi na masikio yatakayosikia kweli yako usiku huu ,Wacha nione na kusikia kinachoendelea katika ulimwengu wa Roho kwa jina la Yesu
Amen.
 
IMG_20210128_162952_5.jpg
 
Back
Top Bottom