Mimi ratiba ikiwa ngumu napotea gym hata mienzi mitatu ila kila siku asubuhi napiga push 400+ (40 Γ 10),huwa napungua ila frame ya body inabaki na power ya mikono inakuwepo.
Ila nikirudi gym(2hrs) huwa nakamia sana kwa mwenzi napumzka siku tano tu, mwili unauma siku nne tano za mwanzo misuli ikiachia hakuna maumivu tena ni kufumuka tu.
Nikipumzika sisikiagi maumivu napunguaga kimtindo push up ndio huwa zinanilinda.