Luka 12:16-21
Neno: Bibilia Takatifu
16 Kisha akawaambia mfano, βShamba la tajiri mmoja lilizaa sana.
17 Akawaza moyoni mwake, βNifanye nini? Maana sina mahali pa kuweka mavuno yangu.β
18 Kisha akasema, βNitafanya hivi: nitabomoa maghala yangu na kujenga maghala makubwa zaidi na huko nitaweka mavuno yangu yote na vitu vyangu.
19 Na nitasema moyoni, βHakika nina bahati! Ninayo mali ya kunitosha kwa miaka mingi. Sasa nitapumzika: nile, ninywe na kustarehe.β
20 Lakini Mungu akamwambia, βMjinga wewe! Usiku huu huu utakufa! Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea vitakuwa vya nani?β
21 Hivi ndivyo itakavyokuwa kwa mtu yeyote anayehangaika kujikusanyia utajiri duniani lakini si tajiri mbinguni kwa Mungu.β