Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Misingi ya kuishi Pamoja!
.
1. Ukifika Sehemu... Salimia
2. Ukiondoka Sehemu..... Aga
3. Ukisaidiwa....... Shukuru
4. Ukiahidi...... Tekeleza
5. Ukikosea.... Omba Msamaha
6. Kama Hujaelewa..... Uliza
7. Unacho... Gawa Kwa Wengine
8. Huna.... Usione Donge
9. Ukivunja.... Lipa
10. Kama Hupendi...... Heshimu
11. Ukipendwa... Onesha Upendo
12. Huwezi Kusaidia... Usisumbue
13. Ukiharibu... Rekebisha
14. Ukikopa.... Lipa
15. Wakikuuliza .... Jibu
16. Ukiwasha....... Zima
17. Ukifungua...... Funga
18. Ukinunua.... Lipa
19. Ukichafua.. Safisha
20. Ukipungiwa..... Punga
21. Ukipewa.... Shukuru
22. Ukiazima... Rudisha

''Ukizifuata kanuni Hizi, Utaona Jinsi Utakavyoishi Na Watu Vizuri Hata Kama Huna Hela, Hii Ni kwa Binadamu Wote Hata Kama Ni Kiongozi'''

Sent from my LM-V500N using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom