Selfika na JF: Snap it. Show it

PENZI KITOVU CHA UZEMBE

KISA CHA NGONSWE NA MAZOEA KWENYE SENSA

MITOMINGI: nadhani sasa mgeni amekwisha kumaliza kula hebu nenda kaondoe vyombo.

MAMA MAZOEA: Basi fanya haraka (Mazoea anatoka, anaenda kwa Ngoswe alipo).

MAZOEA: Hodi! Hodi!

NGOSWE: Karibu.

MAZOEA: (Akiingia). Ahsante. Nimekuja kuchukua vyombo.

NGOSWE: Vyombo! Kaa basi mbona unasimama kama vile hakuna viti.

MAZOEA: Nimeambiwa nifanye haraka.

NGOSWE: Mmm! Haya ngoja ninawe basi (Ngoswe ananawa kwa taratibu jicho likiwa usoni mwa Mazoea ambaye anatazama kando). Hivo mzima wee?

MAZOEA: Bee!?

NGOSWE: Salama?

MAZOEA: Salama tu.

NGOSWE: Sasa ndio umekataa kukaa?

MAZOEA: (Ajidai hakusikia) Si umekwisha maliza?

NGOSWE: Bado kidogo.

MAZOEA: Basi nitakuja chukua baadaye. (Ataka kutoka)

NGOSWE: Basi nenda navyo. (Mazoea anarudi kuinama kuvichukua. Ngoswe kwa sauti ndogo). Hivyo waitwa nani?

MAZOEA: Mie?

NGOSWE: Ndio wewe hapo kisura.

MAZOEA: (anatabasamu huku akiondoka). Mazoea!

Story ni tamu ila tulishaambiwa ya Ngoswe tumuachie Ngoswe!

JIANDAE KUHESABIWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…