Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Mwaka 2010, mama yangu mkubwa aliugua sana, alikuwa anaumwa ugonjwa wa ini tokana na kuwa alcoholic, kabla hajafariki aliugua coma, na hali haikuwa vizuri hata kidogo.
Huyo mama yangu amenisomesha, amenipa mwanga wa mambo mengi sana, maisha yake ya usichana ameishi ughaibuni, nikiwa mshamba kabisa nakwenda kumuona, nashangaa kila kitu, yeye alinipenda sana, na mie nilimpenda sana.

Nimekutana na marafiki wengi kwa sababu yake, na mambo mengine yote ni sababu yake.

Baada ya kuugua sana, watu walikata tamaa akiwemo baba yangu mkubwa ambae ni mmewe, kwa kweli nilimuomba sana Mungu ampe nafuu japo nipate kumuaga mama yangu kipenzi, hata nimwambie tu ahsante mama, anione mwanae anitambue roho yangu ifurahi.

Siku mbili baadae napata taarifa mama amepata nafuu yaani ametoka kwenye coma lakini ana wiki mbili ama mwezi kabla ini lake halija shutdown kabisa.

Namshukuru mungu nilimuona kwa mara ya mwisho , nilimshukuru kwa mema aliyonitendea, nilitoka hapo nalia, sikuamini kama kweli nimemuona akaniona mama yangu kipenzi, nilikua nae karibu sana kabla hajaanza ku hit bottles hard,namshukuru mungu alinipa wasaa kumuona mama yangu mara ya mwisho na kumwambia kwa heri.

Hakika mkuu naweza sema Mungu alisikia maombi yangu

Mungu hajibu kwa kile unachotaka bali unachohitaji.

1 Petro 3:12 NEN​

Kwa maana macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza maombi yao. Bali uso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu.

_King
Pole kapteni.

Muenzi mama kwa yale mema yake aliyoyafanya wakati wa uhai wake.
 
Luka 15 7, 10

7 Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.

10 Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.

#AbbaFather 😍😍
 
Amen mtumishi🙏😊
 
This is very deep Captain.

Mama aendelee kupumzika salama huko aliko. Na anaendelea kuishi kupitia kwako. Na wewe pass it forward...ili chain ya wema wake na legacy yake aliyoianzisha kwako iendelee. Maisha
God is watching over her now.
Mkuu maisha yatakua si mazuri kwa wakati fulani, lakini yatapita, ugumu utarudi utapita tena, utarudi utapita tena, ni kwenda na kurudi over and over again, maisha hayatokaa sehemu moja tu ya furaha au sehemu moja ya kuumiza tu, nililia sana toka alipokuwa anaumwa mpaka mauti yanamfika, maneno yake bado naishi nayo mpaka leo, japo si kila mmoja ataona yana umuhimu lakini kwa mtu ambaye nilimpenda yana umuhimu, nitaendelea kupasisha mema aliyonambia kwa wengine.

Thanks a lot Shimba Ya Buyenze

🙏 🙏
 
🙏🙏🙏🙏 nimefurahi sana hili neno
 
,
20220525_182539.jpg
 
Back
Top Bottom