Mimi ninaona unawaonea hao wapiganaji bure, hali ya kisiasa cha nchi zetu hizi changa ni ngumu kwa mtu yoyote yule kwenda full throttle, kwa sababu ya usiri wa uendeshaji wa Serikali zetu na nyenzo nyingi za habari na ulinzi na usalama kuwa mikononi mwa mafisadi, na pili uelewa mdogo wa wananchi.Bubu Ataka Kusema,Mkandara,FMES,
..I believe we will not get to the bottom of this scandal bcuz Mwakyembe & Co, do not have the full support of the President.
..sasa pamoja na ukweli huo, I dont see "wapiganaji" wakija na plan B.
..vilevile zile kauli za "WAPIGANAJI" kwamba JK ndiyo amiri jeshi wa vita za ufisadi, naamini ni USANII tu. ingekuwa ni hivyo Rostam asingekuwa na jeuri ya kujihusisha na Dowans waziwazi kiasi kile.
..binafsi niko frustrated na serikali, Bunge, pamoja na "wapiganaji."
Sasa ndio watu pamoja na wabunge wanaanza kuelewa umuhimu wa wao kutumia nguvu au uwezo walio nao katika kulipigania taifa.
mfano angalia sasa hivi tu "hao wapiganaji" wanavyo jaribu kuchafuliwa ili kupunguza makali ya hiyo report, sasa isingekuwa sasa hivi na haya mambo ya wavuti, na blog tungekuwa wapi au wangekuwa wapi hao wapiganaji?
kuhusu Bunge pia lazima uelewe kuna wengine wamekwenda kule hata hawajui wamekwenda kufanya nini? wapo wapo ndio matokeo yake unasikia kauli kama za kina Serukamba, Makongoro, etc na kuna wengine labda hawa zungumzi lakini ukifika wakati wa kupiga kura waaangalia nani aliwapa billioni 2 za kuzima richmond, au kuangalia Kaka yupo upande gani.
Ukiwa frustrated na serikali hapo ni sawa maana tuliwategemea wafanye mambo kwa kufuata ukweli na uwazi lakini sivyo, wametumia heshima tuliowapa na imani yetu kwao kutufisadi.
Sawa na wewe leo Mtoto wako aendewe kinyume na kiongozi wa Dini yako, au unapokuta mtaalamu awe Prof na usomi wake lakini badala ya kuchagua wataalamu kumsaidia anachagua watu au mtu kufuatana na ukabila au faida zake za kikazi.
Halafu kauli ya nani atakuwa mteuliwa CCM , bado ni mapema mno kusema fulani atapita au la mengine ni poroja za kisiasa