Selelii awazima Lowassa na Rostam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Selelii awazima Lowassa na Rostam

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 15, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,449
  Likes Received: 81,506
  Trophy Points: 280
  • Adai Kikwete alikabidhiwa mapema ripoti ya Richmond
  • Asema kama kumuokoa ni yeye aliyepaswa kufanya hivyo

  Na Saed Kubenea
  MwanaHALISI


  JUHUDI za mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na mwenzake wa Igunga, Rostam Aziz kutaka kujivua na gome la Richmond zimezimwa, MwanaHALISI limeelezwa.

  Taarifa kutoka ndani ya kikao cha kamati ya wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika Dodoma wiki iliyopita, zinamtaja mbunge wa Nzega Lucas Selelii kuwa ndiye aliyezima ndoto za Lowassa na Rostam kujisafisha.

  Inaelezwa kwamba Selii alizima ndoto za Rostam na Lowassa baada ya kuanika ushiriki mzima wa wanasiasa hao wawili katika mkataba huo. Mkutano kati ya kamati ya wazee na wabunge ulifanyika siku tatu mfululizo katika ukumbi wa zamani wa Bunge mjini Dodoma.

  Akiongea kwa kujiamini na kuchambua hoja moja baada ya nyingine, Selelii alisema Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wa Richmond ambapo yeye alikuwa mmoja wa wajumbe wake inaoushahidi kwamba Richmond ni mali ya Rostam.

  Kwa upande wa Lowassa, Selelii alisema alibeba kampuni hiyo kwa maslahi ya binafsi ya rafiki yake huyo.

  Akiongea baada ya Rostam kukana kumiliki kampuni hiyo na kutaka kuundwa kwa Tume huru kuchunguza mkataba huo, Selelii alisema “Rostam amewadanganya kwa kusema hahusiki na Richmond.”

  “Huyu Rostam ndiye aliyetafuta nyumba kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya Richmond. Ni yeye aliyelipia pango la nyumba hiyo,” alisema Selelii huku akitolea macho Rostam. Alisema, “Kamati yetu ilihakikishiwa na mtoto wa Mucadam (Hussen Mucadam) ambaye ndiye mwenye nyumba kwamba nyumba iliyotumiwa na Richmond ilipangwa na Rostam.”

  Huku wabunge na wajumbe wa kamati ya wazee wakiwa wamepigwa na butwaa, Selelii alisema “hata jopo la waadishi wa habari lililofanya kazi ya kusafisha Richmond lilitafutwa na Rostam.”

  Alisema Rostam alifikia hatua ya kutumia waandishi hao wa habari mara baada ya vyombo vya habari kuanza kueleza utata wa mkataba. “Ni huyu Rostam aliyekodisha jopo la waandishi wa habari watatu mashuhuri nchini kwa ajili ya kupoza makali. Tumezungumza na waandishi wa habari hawa mmoja baada mwingine na wote wametuthibitishia hili,” alisema Selelii.

  Alitaja hata majina ya waandishi hao kuwa ni Gideon Shoo, Jimmy Mdoe na Salva Rweyemamu ambaye sasa ni mkurugenzi wa mawasiliano ya rais. Tarehe 29 Juni 2006, serikali kupitia Shirika la Umeme la Taifa (Tanesco) ilisaini mkataba wa kufua umeme wa megawati 100 na kampuni ya Richmond Development Company (LLC) bila kwanza kuhakiki uhalali wa kampuni hiyo.

  “Kama hahusiki kwa nini aliwatafuta hawa waandishi wa habari? Kwa nini aliwapa kazi,” alihoji Selelii.

  Alisema mbali na waandishi wa habari na utafutaji wa nyumba, Kamati Teule iliweza kuthibitisha kwamba baada ya Richmond kuhuisha mkataba wake kwa Dowans, wafanyakazi watatu wa Caspian walionekana katika Dowans.

  “Kwa maana nyingine, Dowans, Richmond na Caspian ni baba mmoja mama mmoja.”

  Alisema Kamati Teule imepata ushahidi kwamba “fedha za Dowans zilihamishiwa katika akaunti ya Caspian; Rostam alikuwa akifuatilia mwenyewe fedha hizo hazina,” alisisitiza Selelii.

  Mbunge mmoja wa Bunge la Muungano aliliambia MwanaHALISI kwamba wakati Selelii akieleza wajumbe taarifa hiyo, ukumbi mzima ulikuwa kimya.

  “Hata sindano kama ingeanguka, ingeweza kusikika. Nakuambia yule jamaa jinsi alivyokuwa akiongea kwa upole na taratibu, kila mtu alikuwa na shauku ya kumsikiliza,” alisema.

  Anasema, “Rostam alikuwa amekaa kimya. Alikuwa kama vile amelowa mvua.”Baada ya kueleza ushiriki wa Rostam Selelii aliyeongea kwa kupanga hoja zake alirukia Makongoro Mahanga, mbunge wa Ukonga, ambaye awali alidai kuwa “ripoti ya Bunge ilikuwa feki.”

  Makongoro amesema “ripoti yetu ni feki; Kamati Teule haikumshirikisha Rais Jakaya Kikwete. Haikumueleza; kama angeelezwa angemuokoa Lowassa,” alisema Selelii kwa taratibu. Alisema madai hayo ya Mahanga hayana ukweli, na kwamba yamelenga kuhamishia tatizo kwa wengine. Alihoji: Kama ripoti ilikuwa feki inawezekanaje rais aliyepewa taarifa hiyo kabla ya kuwasilishwa bungeni akaiamini?

  Kuhusu Kamati Teule kutomshirikisha rais Kikwete, Selelii alisema kabla ya kamati kuwasilisha ripoti yake bungeni ilikabidhi ripoti kwa rais. Selelii alikuwa akijibu hoja ya Andrew Chenge na Mahanga waliotumia muda mrefu kueleza kikao juu ya kutoshirikishwa rais Kikwete.

  Alisema, “Rais alikuwapo hapa Dodoma wakati mjadala wa Richmond unafukuta. Tayari alikuwa na ripoti yetu. Sasa kwa nini yeye hakumpa waziri mkuu wake,” alihoji Selelii na kuongeza, “haikuwa kazi ya kamati kumpa ripoti Lowassa.” Alisema, Rais ana vyombo vya ulinzi na usalama. Je, kama yeye mwenye vyombo hivi hakuona kasoro, nani mwingine mwenye mamlaka ya kudai kuwa ripoti yetu ilikuwa feki,” alihoji.

  Akiongea huku akionekana mwenye hasira, lakini kwa taratibu mno, Selelii alisema, “mnaleta umbeya hapa eti rais hakujua haya. Rais tulimpa ripoti hii kabla ya kuwasilisha bungeni.” Taarifa zinasema Selelii alikiambia kikao hicho kwamba Kamati Teule imefanya kazi yake kwa kufuata misingi ya sheria. “Duniani kote mtuhumiwa hawezi kupewa taarifa ya kilichomo katika ushahidi hadi pale suala hilo linapoingia mahakamani. Katika hili Lowassa hana wa kumlaumu,” Selelii alisisitiza.

  Baada ya kumaliza kuumbua Mahanga, Selelii aligeukia Sophia Simba ambaye alituhumu Kamati Teule kuwa imemuonea Lowassa na kumvua nguo mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela na mumewe Joh Malecela. Katika hilo, Selelii alisema, “Sophia Simba huyu ni mwenyekiti Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). Pia ni waziri anayesimamia utawara bora,” chanzo cha habari ndani ya kamati kinanukuu Selelii. Anasema, “aliyoyasema hapa hayakustahili kutolewa katika kikao hiki. Haya ni maneno yanayopaswa kutolewa kwenye kitchen party. Nimemsikiliza kwa makini, mheshimiwa Simba amezungumza mambo binafsi yanayohusu mtu binafsi,” alisema.

  Mbili, Selii alisema, “Sophia Simba amesema hapa kuwa Lowassa ni mwanamme namba moja. Ni mwanamme wa shoka. Akimaanisha kwamba wanaume wote akiwamo rais, waziri mkuu, wabunge na madiwani siyo kitu. Mimi sikubaliani naye. Labda kama mwanamme wa shoka katika masuala mengine,” alisema kwa kujiamini.

  MwanaHALISI limefahamishwa kuwa mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Dk. Harrison Mwakyembe alikabidhi ripoti ya kamati yake kwa Spika wa Bunge, Samwel Sitta 31 Desemba 2007.

  Mara baada ya Sitta kupokea ripoti ya Mwakyembe aliondoka nchini kwenda Uingereza kuhudhuria mkutano wa Bunge la Jumuiya ya Madola.

  Taarifa zinasema mara baada ya Sitta kurejea nchini alikabidhi ripoti hiyo kwa rais Kikwete. Hiyo ilikuwa 29 Januari 2008; kabla ya Kikwete kuelekea Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria mkutano wa viongozi wakuu wa Afrika (AU).

  Rais Kikwete alisafiri kuelekea Ethiopia 29 Januari 2007. Alirejea nchini 5 Februari 2008. Lowassa alikabidhiwa ripoti na Sitta 6 Februari 2009.
  “Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, iwapo nitakupa ripoti hii, sharti nifanye hivyo pia kwa kiongozi wa upinzani,” Sitta alinukuliwa akimueleza Lowassa.

  Baada ya Sitta kumkabidhi Lowassa ripoti hiyo, alimkabidhi ripoti hiyo “Kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed,” taarifa zinaeleza.

  Kwa upande wake, Sitta amekana kuwa Rostam aliwahi kuwasuluhisha yeye na Lowassa. “Ni uwongo mtupu. Mimi sijawahi kusuluhishwa na Lowassa. Kwanza, hatukuwa na ugomvi, sasa kwa nini tusulihishwe,” alihoji Sitta. Alisema madai ya Rostam kwamba Sitta alitaka nyumba yenye hadhi Dar es Salaam na Urambo hayana msingi, kwa kuwa suala la makazi ya spika hupangwa na katibu mkuu kiongozi.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  as usual we are tired of this ngonjera because to me now i see this kama mipasho..if all these facts are there why not taking actions? upuuzi mtupu
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,449
  Likes Received: 81,506
  Trophy Points: 280
  Yeah! You are tired because you don't care of what is happening to our beloved country. For those of us who care we want to know the WHOLE TRUTH and NOTHING BUT THE TRUTH. And who do you expect to take action against those culprits? Kikwete!? Huh! :confused:
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  iam suprised to you whon you care about this country for months and years you have been complaining nothing is happening.to me complaining without taking action like you people is as good as wasting my time.i better use that time to go and drink TUSKER rather than kuongelea mambo ya RICHMOND...maana hata yesu arudi hakuna atakalokuta limefanyika
   
 5. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ngonjera, Mipasho, Woga

  Kama hawawezi kumchukulia hatua wamwache sio tu kulalama maana sasa umekuwa Kama Wimbo wa Taifa
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  you are absolute right mkuu.maana toka tuanze kusikia mambo ya RA ,Lowassa ni mwaka unakatika sasa na hakuna la maana..
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ndio hapo napochoka na Wadanganyika.. yaani mnapewa ukweli na Mpiganaji badala yake mnamtazama yeye kumwondoa uhalali wa maelezo yake. atakwenda vipi mbele ya sheria ikiwa wananchi wenyewe hamridhiki na ushahidi huu..
  Jamani someni maandishi kwanza kisha jukumu la kumhukumu Rostam mnalo nyie wananchi na sii Seleli. Maadam kisha wakilisha kazi yake ni jukumu lenu kuipokea na kuifanyia kazi, leo mnataka tena yeye ndiye akafungue mashtaka! mfanyiwe kila kitu....
  Ama kwelim maneno ya MkamaP naanza kuyaamini kwamba ni kazi kubwa sana kuongoza Umma wa Kitanzania.
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kama JK mwenyewe anawaogopa sisi tutafanya nini ni kupotezeana muda tu
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wabunge wanawa confuse tu wananchi, Wabunge hawaeleweki, Kama wao wabunge wameshika Mpini na wanashindwa kuvuta unataka wananchi wafanye nini sasa

  Ngoma ikivuma sana mwishowe ni kupasuka
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hao wabunge wenyewe waoga..wanatapatapa tu.hayo mambo ya RA kupanga nyumba ya ofisi ya Richmond mbona hayamo kwenye ripoti yao..ni upumbavu mtupu
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,449
  Likes Received: 81,506
  Trophy Points: 280
  So according to you mtetezi wa mafisadi if nothing is happening then we should all forget about mafisadi who're plundering the wealth of our beloved country while millions of our fellow Tanzanians are living in very poor conditions.

  Kanywe Tusker wewe fisadi ambaye unataka RICHMOND ipotee katika mijadala ya Watanzania ili muendelee kuchota mabilioni. Watu wengine kwa kujikweza bwana! Duh! Who do you think you are!? Wabunge ambao ni wawakilishi wa Watanzania katika majimbo mbali mbali walikaa kumsikiliza Selelii bila kuchoka lakini wewe fisadi umeshachoka na sijui kauli yako hapa inamuwakilisha nani!? na huu mjadala wa RICHMOND unakukera sana unataka uachwe ili watu wakanywe Tusker! :confused: Kweli ukistaajabu ya Mussa...... Na wewe utajidai una mapenzi ya kweli na nchi yako wakati hutaki ufisadi uliokithiri ndani ya Tanzania ujadiliwe! Kanywe Tusker zako na tuache sisi tunaotaka kujadili hali ya nchi yetu tufanye hivyo.
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hakuna kitu hapo, wangekuwa na Ushahidi wasingesalimu amri
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,449
  Likes Received: 81,506
  Trophy Points: 280
  Naam kwako wewe ni upumbavu mtupu lakini kwa Watanzania tulio wengi hatuoni huu kama ni upumbavu mtupu. Kweli Mifisadi ndivyo ilivyo!!
   
 14. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #14
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Huku si Kupambana na Ufisadi bali ni Kusengenya Mafisadi
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tatizo la Wabunge wetu hawajui nguvu walizonazo, wanafikiri kwamba wao ni waajiriwa wa Serikali, kwamba wao wanawajibika kwa Serikali. Wengi waliingia bungeni wakiwa bado hawajui hata kama Kuna mihimili mitatu ya dola inayojitegemea!
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Nov 15, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kigogo na ndege ya uchumi, je hapa mnabeza BAK, Selelii au upuuzi wetu?? Maana binafsi nadhani katika magazeti mengi hili halikuandikwa which is bad because ni vizuri watanzania wangeyasikia pia haya

  Binafsi hata maka ni ngonjera, wacha iwe hivyo kwani hata ule mwimbo wa samaki (ambao ni matusi, umepigwa mpaka ukazoeleka) na sasa umekubalika

  Kwahiyo tusichoke kusikia hizi ngonjera kwani ipo siku tutafika nchi ya ahdi... Kumbukeni tunasali kila siku (dini zote) sala hizohizo na hatujaacha kumuomba na kushukuru mungu

  Wacheni hizi ngonjera ziendelee, hata jua linakucha na kuchwa kila siku na hatujalichoka

  Tanzania bila ufisadi ni ndoto inayoweza kuwa kweli
   
 17. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #17
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nadhani itafikia wakati inabidi tuchague watu wa kuwajibu au kuwaelimisha.

  Bob, angalia wewe na Bubu ataka kusema msije mkawa mnapoteza muda wenu bure. Angalia unajadiliana na nani.
   
 18. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #18
  Nov 15, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mkandara,

  Ni kweli wananchi tunataka ukweli; tunataka ukweli wote na wala sio nusu nusu.

  Hayo ndio mambo ambayo walitakiwa kuyaweka kwenye report ya Richmond lakini hawakufanya hivyo, why?

  Kwenye uchunguzi wowote, watu wanasema follow the money? Sasa kama walijua hata fedha zilikuwa zinatumwaje na nani alikuwa anafuatilia, mbona hiyo ndio ingelikuwa taarifa muhimu zaidi?

  Kama wanachoandika sasa ni sahihi, ilikuwa muhimu mno kumhoji Rostam maana mahojiano chini ya kiapo cha bunge yangelikuwa na maana zaidi, huko ndiko kungelikuwa ni kumfunga paka kengere. Nashangaa pamoja na info wanazotoa sasa, walishindwa kutumia nguvu ya bunge kuwahoji hawa wahusika. Hata kama Rostam asingeenda kuhojiwa kwa mapenzi yake, kuna njia zingine ambazo zingemlazimisha yeye kuhojiwa.

  Hii kamati ilikuwa na nafasi ya kuisafisha serikali kwa kutoa ukweli wote lakini bahati mbaya wakaamua kulindana. Sasa wameanza kugombana ndio wanajifanya eti wanataka kutoa ukweli wote, huo ni usanii tu wa kisiasa wa kutaka kutudanganya wananchi.

  Miaka mitatu tunapiga mduara kwenye jambo moja huku hali ya umeme inazidi kuwa duni na kuathiri uzalishaji na huduma zingine. Ifike mahali tulimalize hili suala na kuhangaika na mambo mengine kwa faida ya wananchi wote.

  Hii kamati ya Richmond wasalimishe documents zote walizo nazo kwa spika na polisi, ili vyombo vya umma vizipitie na kuchukua hatua pale inapobidi. Kutoa habari nusu nusu kwa faida zao kisiasa ni abuse of power. Walipewa hiyo kazi kwa niaba ya bunge na wananchi. Wanatakiwa kutuambia wananchi ukweli wote na hawana haki ya kuficha baadhi ya documents.


   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Nov 15, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  True FP... that is a fair play and positive indeed!!
   
 20. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #20
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  mkuu kumbuka ripoti ya Mwakyembe ilionyesha kuwa Rostam alikataa kutokea na alipuuza 'samansi'. Bila shaka Rostam alisha jiapiza kutohojiwa na Kamati ya Mwakyembe.
   
Loading...