Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,254
Mkandara,
Unaweza kuwa sahihi kwamba RA hata angepelekewa polisi bado angekataa kuhojiwa lakini pia huwezi kujua ukweli bila kujaribu.
Kwa mhusika mkuu kama inavyoonyesha sasa kwenye baadhi ya taarifa, mimi naamini ingekuwa busara kuomba amri ya bunge kumhoji RA baada ya kukataa kuitikia ombi la kwanza.
Sio kwasababu akina RA hawafuati sheria basi na sisi tunaojifanya ni waumini sheria tuamue kupambana nao kwa kukiuka sheria hizo hizo.
Ushahidi wa kiapo wa RA ungelikuwa muhimu mno.
Lakini kikubwa zaidi ifike mahali tuachane na mambo ya Richmond na kusonga mbele. Kama tumeshindwa kuwafunga wahalifu ni bora tukakubali ukweli huo. Lakini kama kuna njia zingine za kuwawajibisha basi zifanyike haraka. Tumepoteza muda mrefu mno kujadili jambo moja huku wananchi wanaendelea kuteseka kwa matatizo mbalimbali. Maamuzi ya wanasiasa wanawajibika wakati wa kura. Kama JK ameshindwa kumshughulikia RA basi kilichobaki ni kumshitaki kwa wapiga kura mwaka 2010. Huu mduara imefika mahali imekuwa sanaa, inafurahisha macho na masikio yetu lakini haumwongezei tija Mtanzania wa kawaida.
Mtanzania, yote hayo nakubaliana nawe. Hata hivyo kuna jambo moja ambalo naona umeliruka... nalo ni nia ya hawa wahujumu uchumi. Lengo lao kubwa hivi sasa ni kujisafisha kwa hayo maovu kwa uwezo na mbinu zozote wanazoweza. Na kibaya zaidi ni nia yao ya kujisafisha kwa lengo la kuwaharibia wote waliowafichua na kuwaanika hadharani. Maelezo ya Mh. Selleli yanaonesha nia yao hii. Tumeshindwa kuwafikisha lupango, sawa, lakini kamwe tusiwaruhusu waonekane ni kondoo weupe machoni pa jamii.