Sekeseke la Misafara ya Viongozi ni kero ya kudumu. Hongera Dkt. Mpango kwa kulitambua

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Habari

Siku moja nilikuwa namgonjwa natokea Kahama, Ikabidi tuondoke mapema ili kuwahi dar es salaam mhimbili!

Tulipofika maeneo misigiri singida tukawekwa kando kupisha msafara. Tumekaa nusu saa kimya hakuna kiongozi aliyepita! Nikaona bora nisogee kidogokidogo kupitia rafu road (njia ya ng'ombe) polisi wakanifuata kwa gari lao kuniamuru nisimame. Nikasimama wakaja kuniparamia kutaka kuchukua ufunguo. Nikacheki pembeni nikaona mgonjwa yuko hoi taabani anapumua kwa shida! Nikawasihi polisi wakawa wakali aisee kusema ukweli nikaona kama vipi mbwai na iwe mbwai

Nikawaambia funguo siwapi, fanyeni lolote. Nikaseti mashine yangu nikatulia kwenye gari akili wakati huo ishageuka mbogo nikasema polisi atakayevunja kitasa au kioo na mmwanga ubongo palepale. Wakaizingira gari na mitutu nikawaambia mkitaka lipueni hata na Bomu mkitaka! Lakini funguo hapa haitoki.

Wakampigia RTO singida! Kwamba mimi nimkaindi. Bahati nzuri yule RTO alikuwa ana hekima kubwa sana! Umri wake ni mdogo lakini alikuwa na hekima kubwa sana, nahisi kalelewa vizuri na wazazi wake! Popote aliko Mungu amlinde.

Alipokuja akasema mbona mtu mwenyewe yuko rafu road huko jaman wala hajakaidi chochote. Akanipa pole sana kutokana na mvurugano huo. Tulisimamishwa karibu saa tatu kuanzia saa mbili asubuhi. Wakati huo gari lote wamelizingira na mitutu yao. Nikasema Tanzania kuna uonevu wa kijinga sana basi tu. Misafara inaharibu ratiba za watu vibaya sana hasa barabara kuu za mikoa!

Laiti viongozi wangejua tunaosafiri kutoka mikoa ya mbali huwa tunapangilia masaa! Wangepiga marufuku kufunga njia barabara kuu! Ni ubinafsi ulipitiliza wa kufunga njia kuu. Kwa kauli ya makamu wa raisi hakika nimewasaheme kwa niaba mzee huyu amejua maumivu ya misafara. Wakuu wa vikosi badilisheni namna ya kufunga njia, Leo mko madarakani kuna siku mtatoka!

Ubabe barabarani haufai zingatieni sheria na utu! Mfano jana jumatano! Huko dar es salaam Africana kulikuwa na send off ukumbi wa JC HALL, Saa 6 usiku baada ya sherehe, Sijui ni kiongozi gani alikuwa na ule msafara na king'ora wametoka pale na msafara na kuforce kuingia roads pale kona ya kibona.

Kulikuwa na lori la mchanga likiwa kwenye spidi kutokea mteremko wa mbuyuni! Wakalichomekea likawavaa landcruser ya msafara moja imepasuka vibaya pale jana usiku wa kuamkia Leo. Wale maaskari walimkamata kondakta wamempiga vibaya kwa uzembe wao! Sijui kama yuko hoi hadi tunavyoongea leo.

Fuatilieni lakini kusema ukweli misafara na uendeshaji wa magari ya misafara haujali watumiaji wengine wa barabara.

Ni moja ya mambo ya kudhihirisha upumbavu wa watu wa taifa hili.
Ule hua ni ushenzi na ukatili mkubwa kwa watu na uchumi. Sisi bado sana kuwa civilised.
 
Yeye kaongea kamaliza tatizo utekelezaji.polisi badilikeni hata ninyi mnandugu zenu wanaotumia barabara.yaani usimame barabarani masaa manne huku unamgonjwa kisa tu kiongozi?

Mtu anatoka mwanza kufika dar es salaam saa tano au saa sita harafu unasimamishwa barabarani masaa manne? Kwanza hizi barabara kuu hakuna haja ya kusimamisha watu.
 
Yeye kaongea kamaliza tatizo utekelezaji.polisi badilikeni hata ninyi mnandugu zenu wanaotumia barabara.yaani usimame barabarani masaa manne huku unamgonjwa kisa tu kiongozi?
Mtu anatoka mwanza kufika dar es salaam saa tano au saa sita harafu unasimamishwa barabarani masaa manne?kwanza hizi barabara kuu hakuna haja ya kusimamisha watu.
Inauma sana umeseti masaa yako then unavurugwa
 
Habari

Siku moja nilikuwa namgonjwa natokea Kahama, Ikabidi tuondoke mapema ili kuwahi dar es salaam mhimbili!

Tulipofika maeneo misigiri singida tukawekwa kando kupisha msafara. Tumekaa nusu saa kimya hakuna kiongozi aliyepita! Nikaona bora nisogee kidogokidogo kupitia rafu road (njia ya ng'ombe) polisi wakanifuata kwa gari lao kuniamuru nisimame. Nikasimama wakaja kuniparamia kutaka kuchukua ufunguo. Nikacheki pembeni nikaona mgonjwa yuko hoi taabani anapumua kwa shida! Nikawasihi polisi wakawa wakali aisee kusema ukweli nikaona kama vipi mbwai na iwe mbwai

Nikawaambia funguo siwapi, fanyeni lolote. Nikaseti mashine yangu nikatulia kwenye gari akili wakati huo ishageuka mbogo nikasema polisi atakayevunja kitasa au kioo na mmwanga ubongo palepale. Wakaizingira gari na mitutu nikawaambia mkitaka lipueni hata na Bomu mkitaka! Lakini funguo hapa haitoki.

Wakampigia RTO singida! Kwamba mimi nimkaindi. Bahati nzuri yule RTO alikuwa ana hekima kubwa sana! Umri wake ni mdogo lakini alikuwa na hekima kubwa sana, nahisi kalelewa vizuri na wazazi wake! Popote aliko Mungu amlinde.

Alipokuja akasema mbona mtu mwenyewe yuko rafu road huko jaman wala hajakaidi chochote. Akanipa pole sana kutokana na mvurugano huo. Tulisimamishwa karibu saa tatu kuanzia saa mbili asubuhi. Wakati huo gari lote wamelizingira na mitutu yao. Nikasema Tanzania kuna uonevu wa kijinga sana basi tu. Misafara inaharibu ratiba za watu vibaya sana hasa barabara kuu za mikoa!

Laiti viongozi wangejua tunaosafiri kutoka mikoa ya mbali huwa tunapangilia masaa! Wangepiga marufuku kufunga njia barabara kuu! Ni ubinafsi ulipitiliza wa kufunga njia kuu. Kwa kauli ya makamu wa raisi hakika nimewasaheme kwa niaba mzee huyu amejua maumivu ya misafara. Wakuu wa vikosi badilisheni namna ya kufunga njia, Leo mko madarakani kuna siku mtatoka!

Ubabe barabarani haufai zingatieni sheria na utu! Mfano jana jumatano! Huko dar es salaam Africana kulikuwa na send off ukumbi wa JC HALL, Saa 6 usiku baada ya sherehe, Sijui ni kiongozi gani alikuwa na ule msafara na king'ora wametoka pale na msafara na kuforce kuingia roads pale kona ya kibona.

Kulikuwa na lori la mchanga likiwa kwenye spidi kutokea mteremko wa mbuyuni! Wakalichomekea likawavaa landcruser ya msafara moja imepasuka vibaya pale jana usiku wa kuamkia Leo. Wale maaskari walimkamata kondakta wamempiga vibaya kwa uzembe wao! Sijui kama yuko hoi hadi tunavyoongea leo.

Fuatilieni lakini kusema ukweli misafara na uendeshaji wa magari ya misafara haujali watumiaji wengine wa barabara.

View attachment 2586462
Hii ni stori yako au ni kuhusu Mpango?
 
Mimi nadhani Mkuu amechelewa sana maana wapo watu wamepata matatizo kupitia kufungiwa bara bara wakisubiri Waheshikiwa wapite..

Mimi nilikua na jamaa zetu tunasafirisha mgonjwa alitufia mikononi kisa misafara yao isiyo na kichwa wala miguu, afadhali watumie ndege basi
 
Back
Top Bottom