TAARIFA KWA UMMA: MAALIM SEIF HAJAMBO VIZURI
Katibu Mkuu wa chama cha CUF, Maalim Seif Shariff Hamad.
7 Machi 2010
Hali ya afya ya Maalim Seif yaendelea vizuri
Chama Cha Wananchi CUF kinawajulisha wanachama na wapenzi wa CUF na Watanzania wote kwa ujumla kwamba Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, amelazwa katika hospitali ya Hindu Mandal, mjini Dar es Salaam ambako anapatiwa matibabu kufuatia kusumbuliwa na bronchitis ambayo ilisababisha kupanda kwa blood pressure.
Hali hiyo ilimtokea ghafla juzi Ijumaa, tarehe 5 Machi, hapo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere wakati akiwa katika hatua za mwisho za kuondoka kuelekea Muscat, Oman kwa ziara ya binafsi.
Ingawa alikuwa akisumbuliwa na bronchitis kwa siku kadhaa, alikuwa akiendelea vyema na shughuli zake hadi alipokutwa na tatizo hilo wakati akiwa Uwanja wa Ndege.
Kwa kuwa Maalim Seif ni kiongozi wa kitaifa ambaye anaheshimiwa na Watanzania walio wengi tumeona kuna haja ya kutoa taarifa hii ili Watanzania wajue. Tunawahakikishia wana-CUF na Watanzania wote kwamba hali yake ya kiafya inaendelea vizuri na daktari wake ameridhika kwamba ataweza kuendelea na shughuli zake za kawaida katika siku chache zijazo.
Haki Sawa kwa Wote
Imetolewa na:
Salim Bimani,
Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma, CUF
Simu: +255 777 414 112
letest toka Hindu Mandal: Maalim Seif, ameruhusiwa kutoka hospitali, ila ameshauriwa kuendelea kupumzika hospital leo atatoka rasmi kesho.
.....Tunashukuru kwa taarifa ingawa kitaalam Brochitis haisababishwi na high blood pressure.
Bronchitis ni "inflammation of the airway" na husababishwa na virusi, bakteria, kemikali, vumbi au uvutaji wa sigara.
Ushauri: Ni vyema wasemaji wa CUF wakawaachia wataalam wa tiba kutoa maelezo ya kitaalam kuhusu afya ya kiongozi wao.
Kwa waelewa Bronchitis na BP ni vitu viwili tofauti na havina mahusiano ya karibu.
Chama Cha Wananchi – CUF kinawajulisha wanachama na wapenzi wa CUF na Watanzania wote kwa ujumla kwamba Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, amelazwa katika hospitali ya Hindu Mandal, mjini Dar es Salaam ambako anapatiwa matibabu kufuatia kusumbuliwa na ‘bronchitis' ambayo ilisababisha kupanda kwa ‘blood pressure'.
Swelling in the ankles and legs, and sometimes swelling in the abdomen, may occur in advanced chronic bronchitis. This happens because blood vessels narrow (constrict) to try and divert blood to less damaged areas of the lungs where more oxygen is available. This constriction can lead to high blood pressure in the lungs (pulmonary hypertension). Pulmonary hypertension causes the right side of the heart to work harder than it should. Eventually, that side of the heart may not be able to keep up with the workload. This is called right heart failure, or cor pulmonale. Right heart failure may cause blood to back up in the liver, intestines, and legs. This may cause swelling in the ankles, legs, and abdomen. High blood pressure and chest pain may also occur.
Kabla ya kukimbilia utaalamu mwingi ni vizuri ukajifunza kusoma.
Rejea taarifa
Kuna tofauti kati ya ulichosema wamesema na walichosema, elewa tofauti ya "ilisababisha" na "ilisababishwa"
You got it backwards, hawakusema kwamba blood pressure imesababisha bronchitis.Hawakusema bronchitis haisababishwi na bcteria.Wamesema Hamad ana bronchitis ambayo ilimsababishia blood pressure kupanda.
Mimi si mtaalamu, lakini hata mtu asiye mtaalamu mwenye general interest anajua kwamba moyo ni pampu na pressure ya damu ina uhusiano na mfumo wa kupumua. Si kweli kwamba bronchitis na high blood pressure havina uhusiano wa karibu.
Ona wataalam wanavyosema hapa
http://www.tappmedical.com/bronchitis.htm
Hatukatai mtu kutaka kuwa critic, that is the salt of JF. Lakini kabla ya kushutumu watu fanya homework yako kwanza.
Kwa sababu kazi ya kuwa critic ni sacred, na kama huifanyi vizuri tupo hapa ma "critic's critic" .
Kiranga ni noma!!!!!!