Seif Maalim - CUF kaanguka jana Dar Airport

Mgombezi

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
610
178
Kuna tetesi kwamba Seif Maalim - CUF kaanguka jana Dar airport na sasa watu hapa kisiwani Zanzibar wamekuwa wakipashana habari kwa simu kwamba hali yake ni mbaya sana.

Tunaomba mweye taarifa sahihi atuletee hapa.

T
 
Kuna tetesi mbaya pia iliingia ikidai yu kwenye hali tete, ndipo kuna mtu amezungumza na Hamad Rashid Mohamed, amethibisha kuwa Maalim Seif ni Mzima bheri wa Afya na anaendelea vizuri, yuko hospitalini kwa mapumziko tuu na uangalizi wa karibu.

Ila amepewa mapumziko ya siku 14.
 
Haya mambo mengine bana! Atakuwa amechoka kama kikwete manake naye siku hizi anakula shavu la safari sana
 
TAARIFA KWA UMMA: "MAALIM SEIF HAJAMBO VIZURI"

Katibu Mkuu wa chama cha CUF, Maalim Seif Shariff Hamad.

7 Machi 2010
Hali ya afya ya Maalim Seif yaendelea vizuri
Chama Cha Wananchi – CUF kinawajulisha wanachama na wapenzi wa CUF na Watanzania wote kwa ujumla kwamba Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, amelazwa katika hospitali ya Hindu Mandal, mjini Dar es Salaam ambako anapatiwa matibabu kufuatia kusumbuliwa na ‘bronchitis' ambayo ilisababisha kupanda kwa ‘blood pressure'.
Hali hiyo ilimtokea ghafla juzi Ijumaa, tarehe 5 Machi, hapo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere wakati akiwa katika hatua za mwisho za kuondoka kuelekea Muscat, Oman kwa ziara ya binafsi.
Ingawa alikuwa akisumbuliwa na ‘bronchitis' kwa siku kadhaa, alikuwa akiendelea vyema na shughuli zake hadi alipokutwa na tatizo hilo wakati akiwa Uwanja wa Ndege.
Kwa kuwa Maalim Seif ni kiongozi wa kitaifa ambaye anaheshimiwa na Watanzania walio wengi tumeona kuna haja ya kutoa taarifa hii ili Watanzania wajue. Tunawahakikishia wana-CUF na Watanzania wote kwamba hali yake ya kiafya inaendelea vizuri na daktari wake ameridhika kwamba ataweza kuendelea na shughuli zake za kawaida katika siku chache zijazo.
Haki Sawa kwa Wote
Imetolewa na:
Salim Bimani,
Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma, CUF
Simu: +255 777 414 112
 
TAARIFA KWA UMMA: “MAALIM SEIF HAJAMBO VIZURI”

Katibu Mkuu wa chama cha CUF, Maalim Seif Shariff Hamad.

7 Machi 2010
Hali ya afya ya Maalim Seif yaendelea vizuri
Chama Cha Wananchi – CUF kinawajulisha wanachama na wapenzi wa CUF na Watanzania wote kwa ujumla kwamba Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, amelazwa katika hospitali ya Hindu Mandal, mjini Dar es Salaam ambako anapatiwa matibabu kufuatia kusumbuliwa na ‘bronchitis’ ambayo ilisababisha kupanda kwa ‘blood pressure’.
Hali hiyo ilimtokea ghafla juzi Ijumaa, tarehe 5 Machi, hapo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere wakati akiwa katika hatua za mwisho za kuondoka kuelekea Muscat, Oman kwa ziara ya binafsi.
Ingawa alikuwa akisumbuliwa na ‘bronchitis’ kwa siku kadhaa, alikuwa akiendelea vyema na shughuli zake hadi alipokutwa na tatizo hilo wakati akiwa Uwanja wa Ndege.
Kwa kuwa Maalim Seif ni kiongozi wa kitaifa ambaye anaheshimiwa na Watanzania walio wengi tumeona kuna haja ya kutoa taarifa hii ili Watanzania wajue. Tunawahakikishia wana-CUF na Watanzania wote kwamba hali yake ya kiafya inaendelea vizuri na daktari wake ameridhika kwamba ataweza kuendelea na shughuli zake za kawaida katika siku chache zijazo.
Haki Sawa kwa Wote
Imetolewa na:
Salim Bimani,
Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma, CUF
Simu: +255 777 414 112

Tunashukuru kwa taarifa hii ambayo itaondoa speculations!
 
letest toka Hindu Mandal: Maalim Seif, ameruhusiwa kutoka hospitali, ila ameshauriwa kuendelea kupumzika hospital leo atatoka rasmi kesho.
 
letest toka Hindu Mandal: Maalim Seif, ameruhusiwa kutoka hospitali, ila ameshauriwa kuendelea kupumzika hospital leo atatoka rasmi kesho.

At least we can breath now!
Huyu jamaa anaeitwa RISK TAKER ametupa jakamoyo kubwa!
 
.....Tunashukuru kwa taarifa ingawa kitaalam Brochitis haisababishwi na high blood pressure.

Bronchitis ni "inflammation of the airway" na husababishwa na virusi, bakteria, kemikali, vumbi au uvutaji wa sigara.

Ushauri: Ni vyema wasemaji wa CUF wakawaachia wataalam wa tiba kutoa maelezo ya kitaalam kuhusu afya ya kiongozi wao.
Kwa waelewa Bronchitis na BP ni vitu viwili tofauti na havina mahusiano ya karibu.
 
Poleni sana ila kuna umuhimu watu kama hawa wawe na tabia ya kupima afya zao kila wakati na sio mpaka Tatizo litokee
 
.....Tunashukuru kwa taarifa ingawa kitaalam Brochitis haisababishwi na high blood pressure.

Bronchitis ni "inflammation of the airway" na husababishwa na virusi, bakteria, kemikali, vumbi au uvutaji wa sigara.

Ushauri: Ni vyema wasemaji wa CUF wakawaachia wataalam wa tiba kutoa maelezo ya kitaalam kuhusu afya ya kiongozi wao.
Kwa waelewa Bronchitis na BP ni vitu viwili tofauti na havina mahusiano ya karibu.

Kabla ya kukimbilia utaalamu mwingi ni vizuri ukajifunza kusoma.

Rejea taarifa

Chama Cha Wananchi – CUF kinawajulisha wanachama na wapenzi wa CUF na Watanzania wote kwa ujumla kwamba Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, amelazwa katika hospitali ya Hindu Mandal, mjini Dar es Salaam ambako anapatiwa matibabu kufuatia kusumbuliwa na ‘bronchitis' ambayo ilisababisha kupanda kwa ‘blood pressure'.

Kuna tofauti kati ya ulichosema wamesema na walichosema, elewa tofauti ya "ilisababisha" na "ilisababishwa"

You got it backwards, hawakusema kwamba blood pressure imesababisha bronchitis.Hawakusema bronchitis haisababishwi na bacteria.Wamesema Hamad ana bronchitis ambayo ilimsababishia blood pressure kupanda.

Mimi si mtaalamu, lakini hata mtu asiye mtaalamu mwenye general interest anajua kwamba moyo ni pampu na pressure ya damu ina uhusiano na mfumo wa kupumua. Si kweli kwamba bronchitis na high blood pressure havina uhusiano wa karibu.

Ona wataalam wanavyosema hapa

http://www.tappmedical.com/bronchitis.htm

Swelling in the ankles and legs, and sometimes swelling in the abdomen, may occur in advanced chronic bronchitis. This happens because blood vessels narrow (constrict) to try and divert blood to less damaged areas of the lungs where more oxygen is available. This constriction can lead to high blood pressure in the lungs (pulmonary hypertension). Pulmonary hypertension causes the right side of the heart to work harder than it should. Eventually, that side of the heart may not be able to keep up with the workload. This is called right heart failure, or cor pulmonale. Right heart failure may cause blood to back up in the liver, intestines, and legs. This may cause swelling in the ankles, legs, and abdomen. High blood pressure and chest pain may also occur.

Hatukatai mtu kutaka kuwa critic, that is the salt of JF. Lakini kabla ya kushutumu watu fanya homework yako kwanza.

Kwa sababu kazi ya kuwa critic ni sacred, na kama huifanyi vizuri tupo hapa ma "critic's critic" .
 
Kabla ya kukimbilia utaalamu mwingi ni vizuri ukajifunza kusoma.

Rejea taarifa

Kuna tofauti kati ya ulichosema wamesema na walichosema, elewa tofauti ya "ilisababisha" na "ilisababishwa"

You got it backwards, hawakusema kwamba blood pressure imesababisha bronchitis.Hawakusema bronchitis haisababishwi na bcteria.Wamesema Hamad ana bronchitis ambayo ilimsababishia blood pressure kupanda.

Mimi si mtaalamu, lakini hata mtu asiye mtaalamu mwenye general interest anajua kwamba moyo ni pampu na pressure ya damu ina uhusiano na mfumo wa kupumua. Si kweli kwamba bronchitis na high blood pressure havina uhusiano wa karibu.

Ona wataalam wanavyosema hapa

http://www.tappmedical.com/bronchitis.htm

Hatukatai mtu kutaka kuwa critic, that is the salt of JF. Lakini kabla ya kushutumu watu fanya homework yako kwanza.

Kwa sababu kazi ya kuwa critic ni sacred, na kama huifanyi vizuri tupo hapa ma "critic's critic" .

Kiranga ni noma!!!!!!
 
Kiranga ni noma!!!!!!

Watu wengine wanaudhi na umajununi wao, sijui wakiona Kiranga anazodoa wanafikiri kuzodoa ni kazi rahisi. Kuzodoa kunataka ufanye kazi, ufanye utafiti, ujue unachosema, least of all ujue kusoma na comprehension, sio kujitia ujanja mwingi kumbe mbele kiza.

Maalim Seif get well soon.
 
Alhamdullilah...mungu akuweke Maalim...mpaka "mission" iwe "accomplished" (amin)
 
Hali ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad, imeimarika kiafya baada ya kupata matibabu katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar leo.

Kuimarika kwa afya ya mwanasiasa huyo mwandamizi wa kambi ya upinzani na Katibu wa CUF imeondoa hofu na minong’ono iliyoenea jijini kwamba Maalim Seif, amefariki dunia.

Maalim Seif amesema tatizo linalomsumbua ni kupanda kwa shinikizo la damu na kwamba juzi lilimsababishia kushindwa kusafiri.

Amesema shinikizo la damu lilipanda ijumaa saa 11 jioni alipokuwa akisubiri kupanda ndege kwenda Oman kwa ajili ya shughuli zake binafsi.

“Kweli nilipata matatizo ya kiafya kidogo ijumaa iliyopita kama kwenye saa 11 jioni wakati nasubiri kwenda Oman kwa shughuli binafsi, ndiyo hali ilipobadilika ghafla... lakini sasa naendelea vizuri tatizo kubwa ni high blood pressure (kupanda kwa shinikizo la damu) ila tangu nilipolazwa haijapanda tena.

“... Ugonjwa huu unanisumbua tangu mwaka 1989 lakini kwa kipindi kirefu ulikuwa under control (chini ya uangalizi) ila kwa sasa naona limekuwa kubwa mno, nadhani ni kwa ajili ya kazi nyingi.

“Madaktari wamenipima moyo wameona upo safi, damu safi na mapigo ya moyo yapo safi sasa wamenipumzisha na Mungu akipenda leo jioni au kesho Inshaalah nitaruhusiwa,” alisema Maalim.

"Kwa sasa hali yangu imeimarika na nipo chini ya uangalizi wa madaktari kwa ajili ya kupumzika wakati wakiendelea kudhibiti shinikizo hilo la damu alisema mkongwe huyo wa siasa visiwani Zanzibar."

Aidha, Maalim Seif liwashukuru Watanzania walioguswa baada ya kupata taarifa za ugonjwa wake na wengi wao kmtumia salamu za pole hali iliyomfariji na kuona jinsi wananchi wanavyoshirikiana

Picha hizi ni alipotembelewa na watu mbali mbali na kuongea na waandishi hospital

Mpigapicha wa Globu ya Jamii, Francis Dande akimpa pole Maalim Seif.JPG.jpeg

Maalimu Seif akipewa pole.JPG.jpeg

Maalimu akifanyiwa mahojiano na TBC1.JPG.jpeg

Maalimu Seif akiwa hospitali ya Hindu Mandal leo.JPG.jpeg

Source michuzi blog
 
Back
Top Bottom