Zawadini
JF-Expert Member
- Feb 2, 2012
- 2,213
- 1,638
Kwenye hili wanaouza hizo nyumba ni hao"masikini"waliopewa nyumba na Serikali baada ya nyumba zao kuvunjwa kupisha ujenzi wa nyumba za Michenzani.Fikra za kuifanya Zanzibar ijitenge?
Fikra za serikali tatu badala ya moja?
Hata Karume fikra zake nzuri za kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya maziwa an asali zimetupiliwa mbali na uongozi uliofuata.
Majengo ya ghorofa pale michenzani yaliyojengwa kwa ajili ya Wazanzibari wasio na kipato cha kutosha sasa hivi yana kaliwa na wenye ukwasi ambao pia wanawakodisha wengine huku maskini wakiishi kwenye vijumba vya mbavu za mbwa huko miferejini nk