Sehemu za kazi ni sehemu hatari sana ingawa tunapokea chochote kitu

Mama Edina

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
748
1,816
Waungwana,

Maeneo tunayojidai ni maeneo ya kazi au shughuli zetu tunazotenda kila siku ni sehemu ambazo zina michakato kiutendaji na fani na maudhui mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku.

Ni sehemu tunamoonesha utendaji kazi ili kiuweza kumshawishi boss akupe bonus kama ni kiwandani na kadhalika lakini kama ni hospitalini boss hakai hapo, kama ni shuleni boss hakai hapo sana sana hapo wamejaa machawa na watu ambao wanaumbea asikuambie mtu.

Ni sehemu za kutendea haki, tuishi lakini ni sehemu za kuogopa sana, bianadam unaofanya nao kazi waogope sana. Usiwadharau wala usijipendekeze kwao, kikubwa ni kaa mbali sana viumbe anayeitwa mfanyakazi mwenzio!
 
Kwenye taasisi yetu Nilikuwa best performing staff of the year_ 2023. Kwa Sasa Nimetengwa na watu wote na nafanyiwa vimbwanga vya Kila namna Hadi ofisi imekuwa chungu kwangu Hadi natamani niache kazi.

Ajabu wao ndiyo walinipigia kura za kupewa hiyo certificate of award. Kwa ufupi napitia mambo mazito.
 
Kwenye taasisi yetu Nilikuwa best performing staff of the year_ 2023. Kwa Sasa Nimetengwa na watu wote na nafanyiwa vimbwanga vya Kila namna Hadi ofisi imekuwa chungu kwangu Hadi natamani niache kazi.

Ajabu wao ndiyo walinipigia kura za kupewa hiyo nafasi
POLE! Keep on fighting. Hawa wapo kila mahali yaani ni shida, Hata hivyo usikate Tamaa
 
Ukiogopa majungu na husda huwezi kuajiriwa labda uache kazi ukajiajiri kwenye biashara zako n.k

Kuna Ofisi niliwahi kufanya kazi miaka fulani ya nyuma

Kutokana na fani yangu, niliwahi kulazimika kuandika Dokezo la Siku 48 hivi na Timu yangu kwenda kufanya kazi Fulani hivi ambayo kama tungemwajiri Consultancy basi Taasisi yetu ingetumia more than 300M kumlipa.

Basi yalipigwa majungu pale kuanzia Wahudumu hadi Maafisa wengine wa idara nyingine

Kwa hali ile niliyoiona, nilipambana baada ya Mwaka mmoja niliomba kuhama ile Taasisi.

Majungu/Husda ni sehemu ya Maisha ya kuajiriwa
 
Back
Top Bottom