Njooni tuambizane ukweli, wamiliki, Wafanyakazi na wateja wa hoteli, migahawa, Mama Ntilie, Baa na sehemu nyinginezo

kitoto wa vitoto

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
360
386
Kwanza kabisa nawasalimia kwa salamu ya pamoja, poleni na pilika za kutwa nzima,
Karibuni unaweza kuondoka hapa na chochote,

Leo nitawazungumzia watu wa makundi ya aina 3
1. WAMILIKI
2. WATEJA
3. WAFANYA KAZI

1: WAMILIKI,
kundi hili ni watu wenye uwezo kidogo au sana, ndio wanaotufanya tuishi mjini kwa kutupa ajira/vibarua
Ndio watu wanaoongoza kwa kuvunja haki za binadamu na kuvunja Sheria za ajira za nch husika
Mara nyingi huambizana wenyewe kwa wenyewe kiasi Cha kumlipa mfanya kazi ukitoka hapa ukaenda pale unakuta mshahara ni huo huo.

Mara nyingi mishahara Ya wafanyakaz wao Huwa Kati ya 50,000 Hadi 250, 000 kwa wachache sana hulipwa Zaid ya hiyo na ukikuta hivyo ujuwe mmiliki siyo mbongo ni mlami(mzungu)/ngozi nyeupe

Pia hawana saa maalumu za kazi wafanyakazi wao. Wengine huingia saa kumi na mbili asubuhi wanatoka saa saba usiku na wengine wachache Huwa na shift,

*Ni wakali sana pale watakapogundua unajua haki zako za msingi na wanakufukuza mara moja bila kufuata utaratibu.

*Wanakuwa na wanasheria uchwara wanaojifanya vipofu pale mfanya kazi anapovunjiwa haki zake za msingi na kuamua kumtetea boss kwa gharama yoyote,

*Baadhi Yao ni wadhulumu sana hawana hata hofu ya mungu
Hawa ndio baadhi ya wamiliki wa hizo sehemu tajwa hapo juu walivyo,

WATEJA,

Hawa ndo huja kutumia
Na ndio mtu anayedhaminiwa kuliko mtu yyte yule pale kwenye ile biashara (Mteja ni mfalme)

*Baadhi Yao Huwa na dharau kupita kiasi

Humuona muhudumu kama kama mtu wa mwisho kwenye hii Dunia hivyo Hana haki yyte ya kusema no
Hivyo basi anataka kila neno lake liitikiwe ndio,

*Baadhi Yao pia wanawafukuzisha baadhi ya wafanyakazi kwa kukataa kutii amri zao hasa za kutaka ngono,
Ukikataa hushtakiwa kwa boss na kuwekelewa makosa mengi ya uongo hatimaye hufukuzwa,

*WATEJA wengine wanataka huduma Bora Ila wabahili sana,

*UKITAKA HUDUMA BORA

Fanya hivi mtu atakayekudumia chakula/kahawa/ mvinyo, au huduma yyte Toka mahali pale mpe tip kidogo hata 1000 alafu uone kesho kama hatakipa huduma bora zaidi.

Nb huduma Bora ni kwa kila mteja Ila anayetoa tip hudhaminiwa na kupewa huduma kwa wakati,

Ukijifanya nunda utazunguka hotels zote restaurant zote club zote pub zote hutapata huduma Bora wafanyakazi wa maeneo hayo huishi kwa kutegemea tip maana mishahara Yao ni midogo, pia Wana tabia ya kumsusa mteja asiyetoa tip

Mfano unaweza kutangulia kufika mahali kama hapo ukaketi ukisubiri hudumu Cha kushangaza watakupita kama hawakuoni hasa wakiwa bize Ila atakuja mteja baada yako atapokelewa kwa ukarimu wa Hali ya juu sana na ataonyeshwa sehemu nzuri ya kuketi na kupewa dhuduma muhimu kama wifi password , penye socket ya kuchajisha simu au laptop yako.

Kama Kuna baridi sana utapewa na Masai shuka ujifunike kama Kuna joto watakuuliza wakuwashie feni,
Wakati huo we bahili hata kinywaji hujasikilizwa.

Akili mtu wangu!!! Utashtaki kwa meneja kesho ukija ni Yale Yale ukihama restaurant nyingine siku ya kwanza unapokelewa vizuri hujaacha tip ukija kesho ni Yale Yale,
Jiongezen watu wangu!!!!!!

WAFANYA KAZI
Kwanza kabisa siyo wavumilivu

Husain mkataba bila kuusima na kuelewa,

Wanadhamini sana walami kuliko wabongo

Hulia shida mara zote hawajiongezi kwa shughuli ingine ya kumpatia kipato

Wala hawajiongezi kielimu Wala kimaarifa

Hustaafu wakiwa fukara kuliko watu ambao hawakuwahi kuajiriwa/kufanya kazi

Walio wengi hawaoni UMUHIMU WA elimu kwa watoto wao,

Huthamini pesa kuliko utu

Walio wengi ni walevi , waasherati, nk

Walio wengi pia hawana utulivu wa hisia za. Mwili

Hudate na kila mtu hasa mameneja kwa ajili ya kuonekana Bora,

*Wengi wao hawajui sheriazinazowalinda Wala hawajishughulishi kuzijua

Naomba niishie hapa
 
N๐ ๐จ๐ฃ๐š ๐ง๐ข๐ซ๐ฎ๐๐ข๐ž ๐ญ๐ž๐ง๐š ๐ค๐ฎ๐ฎ๐ฌ๐จ๐ฆ๐š ๐ก๐ฎ๐ฎ ๐ฎ๐ณ๐ข ๐ฌ๐ข๐ฃ๐ฎ๐ข ๐ฎ๐ฆ๐ž๐ฐ๐š๐ณ๐š ๐ง๐ง
 
Dawa kali ya kumfanya mteja akiingia bar, anogewe asiondoke na amalize pesa zake zote, pia asikome kuja hapo katika bar yako! ๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
 
kati ya ujinga walionao wahudumu ni kuanza kuamini tip "ni haki yao" sasa huu ufal.a nauona anao pia mleta mada.

Hivi nitoe tip alafu bill unalipa wewe mhudumu au ?! Kwahyo nyie makima mkienda kwa mangi kununua bidhaa je hua mnatoa tip kwa ukarimu wake ?!

yani kua mkarimu na kufanya wajibu wako mpaka upewe tip ?! Unajua wahudumu ndio maana kama ulivyosema mnadharaulika sana maana ni wajinga sana pia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom