Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,713
- 13,464
Habari Wakuu,
Kutoka Kisutu, kesi namba 456 ambayo inahusu kuzuia taarifa za upelelezi wa jeshi la Polisi inayowakabili wakurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo na Mike William inaendelea kuunguruma leo Mahakama ya Kisutu. Kesi hii iliahirishwa jana, hivyo leo inaendelea.
Kujua kilichojiri jana soma => Yaliyojiri katika Kesi namba 456: Jamhuri dhidi ya JamiiForums - Oilcom na Uchakachuaji/Ukwepaji kodi bandarini Dar
Tuwe pamoja kujuzana yatakayojiri.
=========
Jana wakati Tundu Lissu anamfanyia Cross Examination, shahidi alitoa kifungu cha Sheria na Kumpa hakimu asome. Endelea...
Tundu Lissu anatoa kifungu...Hakimu anapelekewa akisome 164 (1).
Baada ya kusoma hicho kifungu, Hakimu Kasema kesho Muda wa saa nne asubuhi kesi itaendelea.
Leo inaanzia hapa;
Ile document ya jana tulipoishia iliyokuwa na utata kama iwe kidhibiti au la, imepokewa mahakamani...
Lissu anaendelea na cross examination
Hakimu anasema shahidi aisome yote...ili mahakama iijue
Shahidi anaisoma (Ni majibu kutoka JF kwa barua ya polisi ya 1/4/2016, Inaeleza kuwa wako tayari kutoa ushirikiano kwa polisi ila kuna utata katika wajibu wa mteja wa kulinda faragha ya mteja... Pia wanazungumzia kuwa kifungu kinachotumika kuomba taarifa kiko katika kesi Mahakama Kuu...)
Lissu: Sasa shahidi inaonekana kuwa mawakili wa watuhumiwa walionesha nia yao ya kushirikiana na Jeshi la Polisi
Shahidi: Hawakuonesha nia kwani hawakutoa kinachotakiwa bali walikuwa wanazungusha tu....
Tundu Lissu: Kuna sehemu walisema hawataki kushirikiana?
Shahidi: Hakuna ila....
Tundu Lissu: Inatosha.
Tundu Lissu: Je, mliomba taarifa hizo kwa mujibu wa sheria ya Makosa ya Mtandaoni?
Shahidi: Kwa mujibu wa barua yetu tulitaja.....
Tundu Lissu: Mliomba au hamkuomba?
Shahidi: Nakumbuka katika barua ya kwanza tuliomba kwa kutumia kifungu 32 cha sheria ya mtandao.
Tundu Lissu: Barua uliyoisema ni ya 23/2/2016??.. naomba uitambue ili nikuulize maswali
Shahidi anaitambua
Tundu Lissu: Haya mueleze hakimu kama mliomba kwa kutumia kifungu tajwa
Shahidi: Hapana
Tundu Lissu: Haya angalia na barua yenu ya pili ya 1/4/2016. Je, mlitumia kifungu chochote cha sheria ya Makosa ya Mtandao?
Shahidi: Naomba nisijibu kutumia barua hii kwa sababu sikuiandaa mimi.
Tundu Lissu: Hii barua sisi tumeijua kutoka kwako kwani uliitolea ushahidi jana....
Hakimu anamwambia ajibu
Shahidi: Hatukutaja kifungu chochote
Tundu Lissu: Je, ni kweli washtakiwa wote wawili wameshitakiwa kwa kuzuia Jeshi kufanya upelelezi kwa mujibu wa kifungu namba 22(2) cha sheria ya makosa ya mtandao?
Shahidi: Kweli
Tundu Lissu anamtaka shahidi asome kifungu 32(1) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao.
Kifungu kinasema kuwa polisi anaweza toa order ya kupata taarifa muhimu inayohusu upelelezi...
Tundu Lissu: Kwanini hamkuwaandikia mawakili wa JamiiForums waliowataka kutumia Sheria ya Makosa ya Mtandao?
Shahidi: Ni kweli tulitakiwa kufanya hivyo ila hatukufanya lakini mimi siwezi kujibu badala yake atakuja kujibu aliyeandika
Tundu Lissu: Katika barua ya 1/4/2016 mlitumia kifungu namba 10(2) cha Criminal Procedure Act
Shahidi: Ndio
Tundu Lissu: Naomba usome kifungu namba 22(2) cha Cybercrimes Act
Shahidi: Kinasema atakayeshindwa ku-comply na kifungu cha sheria ya Makosa ya Mtandao ana kosa.
Tundu Lissu: Sasa kwanini mliwakamata wakati hawakuenda kinyume na sheria ya Makosa ya Mtandaoni?
Shahidi: Hata Criminal Procedure Act inatumika nchini...
Tundu Lissu: Kwahiyo aliyesema kuwa anayeenda kinyume na sheria ya Makosa ya Mtandao atashitakiwa kwa makosa ya kimtandao alikuwa hana akili?
Tundu Lissu anasoma barua toka kwa polisi....inasema jeshi la polisi "linaomba" kupatiwa taarifa.
Tundu Lissu: Kifungu namba 32(1) cha Cybercrimes Act kinasema Polisi watoe amri ya kupata taarifa.... Je, mlitoa amri au mliomba?
Shahidi: Hata kuomba ni amri
Tundu Lissu: Kuomba sio amri....
Tundu Lissu: Je, katika barua yenu ya 1/4/2016 mliomba au kutoa amri?
Shahidi: Tuliomba
Tundu Lissu: Je, washtakiwa walifanya kosa gani kukataa ombi lenu?
Shahidi: Haijalishi lugha iliyotumika kwani kifungu cha sheria kimetajwa
Tundu Lissu: Kifungu kilichotajwa sio cha Makosa ya Mtandao. Je, mlileta maomba mahakamani ya kuwataka washtakiwa kutoa taarifa mnazotaka kama sheria ya Makosa ya Mtandao 32(3) inavyowataka?
Shahidi: Hatukuleta
Tundu Lissu: Mweleze hakimu kama mmewahi kuwaambia hawa washtakiwa wawape kompyuta zao au wawawezeshe kuingia ili mpate taarifa.
Shahidi: Mimi sijawahi
Tundu Lissu: Sheria inawapa mamlaka ya kuingia kwenye kompyuta za washtakiwa ili kuchukua taarifa?
Shahidi: Ndio
Hakimu: Sheria gani?
Tundu Lissu: Cybercrime Act 32(4)
Tundu Lissu: Naomba umweleze hakimu kama umewahi kuninyang'anya simu yangu na kukaa nayo wiki 6...
Shahidi: Sikunyang'anya, nilichukua.
Tundu Lissu: Kama uliweza kuchukua simu yangu ni nini kilikuzuia kuchukua kompyuta za JamiiForums na kuchukua taarifa utakazo?
Shahidi: Kama nilivyoeleza kuwa mimi sikuchukua...sijui kama wenzangu hawakuchukua.
Tundu Lissu: Je, katika upelelezi wenu mliwahi kuomba msaada kutoka TCRA?
Shahidi: Tulifanya mawasiliano na TCRA....
Tundu Lissu: Mna barua mliyopeleka TCRA?
Shahidi: Hamna
Tundu Lissu: Katika shauri hili, nani hasa mlalamikaji? Wewe au Usama Mohammed?
Shahidi: Ni mimi...
Tundu Lissu: Kama wewe ndo mlalamikaji, ulirekodi statement ya mlalamikaji?
Shahidi: Ndio
Tundu Lissu: Tunaiomba Mahakama tupatiwe hii rekodi for further cross examination.
(Statement imetolewa.)
Tundu Lissu anasema ana maswali matatu.
1. Mweleze hakimu kama kuna sehemu yoyote ulisema kuwa umepatiwa taarifa na Usama Mohammed...
Jibu: Hakuna.
2. Je, kuna sehemu ulieleza katika statement kuwa kuna taarifa JamiiForums kuhusu Oilcom kukwepa kodi na kuiibia Serikali
Jibu: Hakuna.
3. Je, kuna sehemu umemtaja "Fuhra JF Expert Member" au Maxence Melo au Micke William?
Jibu: Kwa maelezo hayo, hakuna.
Tundu Lissu: Naomba document(statement ya shahidi, PW1) hii itumike kama exhibit.
Wakili wa serikali ana-object
Wakili wa JamiiForums (Lissu) anasema ni muhimu iwekwe kwa matumizi ya baadae.
Tundu Lissu anatoa kifungu ku-support ombi.
Imepokewa na inaitwa exhibit D2.
Tundu Lissu kamaliza anakuja Mtobesya
Wakili wa serikali, Salum anaendelea na maswali kwa shahidi....
Salum: Ukisoma exhibit D1 ambayo ulisema jana kuwa huitambui na usome inarejea barua ya tarehe ngapi? Anampa exhibit D1 na shahidi anasema inarejea barua ya tarehe 1/5 toka kwa Polisi
Salum: Kuna barua mliwaandikia JamiiForums 1/5/2016
Shahidi: Hakuna
Salum: Kumbukumbu namba ya barua yenu ya 1/4 na barua hii inayodaiwa kuijibu zinafanana?
Shahidi: Hazifanani
Mtobesya: Sisi tumecrosscheck zinafanana
Hakimu: Shahidi ameshasema hazifanani
Salum: Unaweza kuzisoma reference numbers zote mbili?
Hakimu ameziomba hizo documents kwanza na anazisoma namba hizo, Zimesomwa na hakimu na ziko tofauti...
Salum: Unaiongeleaje hii barua ambayo jana ulisema huifahamu??
Shahidi: Nasema kuwa siifahamu barua hii...
Salum: Umehojiwa na Lissu na Mtobesya na kukubali kuwa washtakiwa wameshtakiwa na sheria ya makosa ya mtandao na sio criminal procedure act iliyotumika kwenye barua...je sheria ya makosa ya mtandao inasema criminal procedure act isitumike??
Shahidi: Hapana
Salum: Kuna sheria inayoi-overrule Criminal Procedure Act??
Shahidi: Hapana
Salum anaomba exhibit P1
Anampa shahidi asome
Shahidi: "Mteja wetu angependa kujua ni kwa kifungu gani mnaomba taarifa ukiacha kifungu namba 32 cha Cybercrime act"
Salum: Je, kwa kipande hicho cha barua unadhani JF walikuwa hawajui kifungu gani unaombea taarifa?
Shahidi: Walikuwa wanajua
Salum: Uliulizwa na wakili wa JamiiForums kama barua mlizowaandikia zilitaja majina ya Wakurugenzi.. Unazungumziaje hili
Shahidi: Hatukuwataja watuhumiwa kwani ile ni kampuni hivyo tuliwaandikia wakurugenzi na nisingejua majina yao
Salum: Wewe unaweza kujua taarifa za BRELA za kampuni??
Shahidi: Hapana siwezi kujua
Salum: Uliulizwa pia kama barua yenu ilimtaja Usama Mohammed, unaweza kutuambia kwanini hamkumtaja Usama?
Shahidi: Tulikuwa tunachunguza shauri lililoripotiwa polisi la kuleta taarifa za uongo mahakamani...hatukuhitaji kumtaja mlalamikaji...