Zamani kidogo shoga yangu alikuwa na graduation tumemaliza wakasema twende gold crest club kule underground si ndo mara ya kwanza naingia club!
Yesuuuu kuna baridi sio kwa Ac ile , kizuri pembeni kulikuwa na sofa safi mimi na shoga yangu hatutumii pombe tukakaa pale
Watu wanacheza mziki balaa watu wanatoka jasho mimi naskia baridi, nikaita mhudumu aniletee chai



akasema huko chini chai hakuna mpaka hotelini juu. Nikajisemea huu upuuzi gani nina hela yangu siwezi pata ninachotaka.
Kumbe club watu wanacheza na watu ambao hawawajui? Kha! Ile mishiko ndo sikupenda yaan zero sistance mmh
Mimi nimejikalia hapo naona vikaka vinakuja vinanishika eti tukacheze nikajisemea mimi sishikwe na mtu simjui



nisije shikwa na litoto lidogo.
Mara nikamuona mhudumu mtu mzima, kumbe meneja, nikamuuliza siweza pata maziwa akaniambia unataka sehem tulivu nikasema ndio. Akanielekeza kule juu, manina nafika huko nilkuta watu wa maana nikajisemea huku ndo dunia ilipo.
Kutupia jicho namuona waziri fulani wakati ule alikuwa mbunge, na vijana wake nikajisemea kumbe huku ndo wakubwa wanakaa. Sehemu ile nzuri kama unataka utulivu panafaa.
Nilienjoy ile sehemu. Nikaletewa nilivyotaka siku ikaisha.
Sema kitu nilichoona club ile ni sehem ya kutoa stress, watu kule wana raha sana.
Ambao hatutumii pombe kuna kitu tunakikosa, yaan kuna starehe tunaikosa.