Sawa una First Class degree, una A ya Hesabu na wewe ni best student. So what?

Sawa una First Class degree, una A ya Hesabu na wewe ni best student. So what?

Acheni hizo siamini kama wewe na GPA yako ya 2.1 kama unaweza kumshinda kwenye interview mtu mwenye 3.5, siamini?

Japo mimi ni mzee wa makalai, lakini hao wanaopata GPA kuanzia 4.5 ni expetional aisee!
Wako wapi sasa watusaidie kwenye mikataba ya nchi.
 
Kebehi vipi. Huwezi kuwa A student na halafu usizijue big 4 ?
Maana hata vyuoni big 4 huwa wanakuja kila mwaka kwenye career fair na vyuo huwa vinabandika matangazo yao kwenye notice board ili finalist wanafunzi wenye gpa kubwa waanze ku apply. Na vigezo huwa vinawekwa kabisa.. average students wanapita pembeni maana vigezo vinawabana mapemaa

Haijalishi umesoma HKL ama umesoma PCB . Big 4 wanataka As tu kwenye vyeti vyako. Hawataki excuse za kusema mimi nimepata D sababu nimesoma Physics na yule amepata A sababu amesoma Language
Majigambo ni mengi sana Mzee wangu hadi unaboa
 
Nakubaliana na mleta mada.
Kwanza kufaulu sana mitihani darasani sio kwasababu unaakili but ni uwezo wako wakukariri ulivhofundishwa. Elimu ya mkoloni haimjengi msomi kujitegemea na kuchambua mambo kwa kutumia akili yake mwenyewe bali huwajenga kuwa tegemezi na kubana uwezo wao kufikiri

Ni ujinga kujiita msomi mwenye A ya math au GPA first class ya computer science wakati hata ujuzi wa kutengeneza cryber security au virus za udukuzi unashindwa utakuwa ni ukilaza wa kiwango cha lami
 
Big 4 ya kwenye auditing haiwezi kuwa big 4 ya kwenye automobile. Unapozungumzia big 4 ni lazima uweke bayana unajikita katika tasnia ipi.

Big 4 hazifanyi biashara ya auditing tu.
Biashara yao ni consultant ( wapo kwenye consultancy industry)

Hivyo pia big four wanahudumia industry zote ikiwemo hiyo uliyoitaja ya Automobile engineering

Pia hata kwenye ajira zinaajiri watu wa taaluma zote. Hata hao automobile engineers wanaajiriwa na big four pia

Na pia neno big four linamaanisha wao.

Kama unabisha jaribu ku google tu neno big four ama big 4. Uone results zote zitawataja kina nani ?
 
Big 4 hazifanyi biashara ya auditing tu.
Biashara yao ni consultant ( wapo kwenye consultancy industry)

Hivyo pia big four wanahudumia industry zote

Pia hata kwenye ajira zinaajiri watu wa taaluma zote. Hata hao automobile engineers wanaajiriwa na big four pia

Na pia neno big four linamaanisha wao.

Kama unabisha jaribu ku google tu neno big four ama big 4. Uone results zote zitawataja kina nani ?
Ngoja nitatazama Google pia ili nijifunze zaidi mkuu.
 
Leo tuangazie wasongo.

Unaweza kuwa kumefaulu vizuri na unaweza kuwa ni bora masomoni. Lakini unapokuja mtaani watu hawataki kuona vyeti bali wanataka wasikie kitu tofauti ulichonacho ukifananisha na pengine wanavyovijua au vya wenzako ambao mupo pamoja kwenye interview (usahili)

Wengine ushangaa kuna wale ambao darasani walikuwa midiocre (vilaza) lakini kila interview wakienda upata kazi, ili sio suala la kupendelewa au sijui ana ndugu bali ni kitazamo wa fikra.

Kuna watu wanaajiriwa pasipo kuulizwa vyeti, yaani professional resume (wasifu wako wa kitaaluma) pekee unatosha kukupa kazi.

Phrase ya SO WHAT? Ni namna unavyotakiwa kueleza mafanikio yako ya kishule unayashabihiaha vipi na kitu watu wanafanya au wanataka.

Yaani umefaulu Computer science na first class sasa tuambie kwenye mfumo huu wa biashara ama kwa biashara yetu ama kwa wateja wetu taaluma uliyonayo utakuja na njia gani mbadala ya kuwezesha ubora wa biashara.

Namna yote utakavyo jinasibu inabidi isharabu kwa nafasi au majukumu unayotarajia kuyaganya kwenye fursa iliyoko mbele yako.

Kwa hivyo basi tumia muda mwingi kujigenga kwenye business environment yaani namna gani biashara inafanywa, mapungufu yalipo kisha buni jinsi utakavyoweza kutatua changamoto zilizopo au zitakazo kuja.

Kwa kujenga fikra za namna hii basi Muhitimu au mtafuta fursa utakuwa katika nafasi nzuri ya kupata nafasi.

TUZIDI KUTAFAKARI ZAIDI
Mnatuonea wivu sisi Vipanga.Vilaza mna mambo.
 
Back
Top Bottom