Sauti ya Ujerumani: TANESCO hoi bin taaban kifedha!

Sauti ya Ujerumani: TANESCO hoi bin taaban kifedha!

Serikali ya Tanzania imewekwa mtegoni kuamua kupandisha bei yya umeme au ikose mkopo wa dola millioni 200 kutoka benki ya dunia.
Benki ya dunia unasema shirika LA umeme LA Tanesco linaendeshwa kwa hasara kubwa na linaelemewa na madeni makubwa.
Benki hiyo imesema kuwa madeni ya Tanesco yamepanda kutoka dola milioni 200 mwaka Jana hadi dola milioni 363.
Benki hiyo ya dunia imesisitiza kuwa hakuna namna isipokuwa lazima shirika LA Tanesco lipandishe umeme ili kulipunguzie mzigo wa madeni na benki ya dunia ilidhie huo mkopo.
Note: PENYE UKWELI UWONGO HUJITENGA:
Source: DW
Any decision you make in life you are responsible for it
 
Tusiposikiliza wataalam na badala yake kuwaweka mbele wanasiasa na propaganda zao hili shirika litakufa na Tanzania itakuwa giza.

Hii inamaanisha ndoto ya Tanzania ya viwanda inaishia hapo. Kazi zitapotea.

Watanzania tutafakari au tulipe prise sasa hivi au tujifute katika ulimwengu wa umeme.

Amini usiamini mkurugenzi wa TANESCO aliyetumbuliwa alikuwa yupo sahihi.
 
DW wana ajenda gani na Tanzania? Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa hii Radio ya Ujerumani haina zuri la kusema kuhusu Tanzania. Inajulikana msemaji wa Lowassa Abubakar Liongo alikuwa anafanya kazi huko inaelekea bado mkakati bado unafanya kazi. Tuwatakie kila la heri.

Inasema kweli Deutsch well ni mapenzi ya Mungu
 
Hahahahahahaahaha aifungie kwa uchochezi aone makali ya iron Lady Angela Merkel
 
World bank wamechoka Mda mrefu wamekuwa wakitushauri Tuache kusubsides A monopolistic companY kama Tanesco later PSRC walikuja na wazo zuri sana la kuligawa hili shirika katka mashirika matatu ila things Hii wizara ina politiks za pekeee basi lile wazo likatupwa mbali ukiangalia written propasal abt Tanesco wasomi wa nchii hii wanauchungu sana
 
Yani wanakopa ili walipe deni
Na waziri wa nishati ni mmoja wa waliobeba hela kwa rumbesa, na anasubiri kupewa mkopo. Sie tumelogwa si bure saa hizi huyu muhongo angekuwa keshasahaulika huyu kwa nchi zenye uongozi makini.
 
Hapo tutaumia sis wananchi ndio wanunuzi wa umeme na sio serikali maana inatumia umeme bure maofisini....,bado nyumba za askari bureee bado mikataba tata so lazma shirika liwe hoi kifedha
 
hao benki ya dunia wanataka kutuhujumu tusipate Tanzania ya viwanda. wamekuwa wakifanya hivyo siku zote.
 
Yaani nchi yetu inaendeshwa na bila master plan ni watu wameamkaje kila siku hatuna pesa ya Tanesco lakini tunapesa ya kununua ndege ambazo kila mtu anajua hazisaidii chochote zaidi ya kuleta hasara!!Jamani kampuni zote zipelekwe kwenye ubinafsi tutajifunza lini!!
 
Faida ya ndege mpaka ije imfikie mkulima wa pilipili inachukua hata miezi sita
 
Yaani nchi yetu inaendeshwa na bila master plan ni watu wameamkaje kila siku hatuna pesa ya Tanesco lakini tunapesa ya kununua ndege ambazo kila mtu anajua hazisaidii chochote zaidi ya kuleta hasara!!Jamani kampuni zote zipelekwe kwenye ubinafsi tutajifunza lini!!
Anayofanya Magufuli anatekeleza sera za chadema ---- ------ Sumaye
 
Huu ni mpambano mwingine kati ya serikali,benki ya dunia na IMF.

Mmoja ni ule wa mgodi wa Dhahabu dutwa ambako benki ya dunia ina hisa,na wamefutiwa leaeni,mwingine ni huu wa tanesco.

Natabiri kuibuka kwa mgongano mkubwa sana kati ya Tanzania na mashirika haya,na ndani ya miaka miwili ijayo mashirika haya yatakuwa "yametunyoosha"

Mashirika haya hayaendeshwi na siasa,yanaijua tanesco nje ndani,yanasoma hesabu kwanza ndipo yanatoa hela,kama hesabu inasema lazima bei upande,itapanda tu

Wakati huo huo wachina tumewavuruga kwenye reli,sioni kama tuna mahala pa kukimbilia
TUKIMBILIE KWA WARABU.....PESA IPO KULE
 
DW wana ajenda gani na Tanzania? Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa hii Radio ya Ujerumani haina zuri la kusema kuhusu Tanzania. Inajulikana msemaji wa Lowassa Abubakar Liongo alikuwa anafanya kazi huko inaelekea bado mkakati bado unafanya kazi. Tuwatakie kila la heri.
Acha DW Ujerumani yote ni CHADEMA
 
Kwa kawaida mtu anayekuambia Ukweli bila unafiki ndiyo rafiki wa kweli hao DW ni rafiki wa Ukweli hawana Unafiki kama china au Nchi zingine wanaanika Ukweli ili serikali ipate kujifunza.
Wa kujifunza sasa ndio sijamuona bado. Tokea alipotumbuliwa Mramba hapo ndipo nilipo jiridhisha pasipo shaka kwamba kwenye hiyo hiyo tumbua tumbua, wapo watu wanao tafutwa. Hadi sasa sijaona kosa hasa la Mramba ni lipi.
 
Mramba alitumbuliwa kuficha aibu ya serikali!!
 
Mramba alitumbuliwa kuficha aibu ya serikali!!
Na mimi nilielewa hivyo hivyo but kwanini wamchafulie mtu jina ili hali kosa sio lake? And again, kwanini mtu afanywe kua jobless kwa uzembe wa mwingine!? Kulikua na shida gani kumuweka au hata kumhamishia hata wizarani huko akaendelee na shughuli zingine kuliko kumfanyia walicho mfanyia!? Tutakua na hakika gani kwa hao wengine waliotumbuliwa kama na wao hawakuonewa sasa!?
 
Hapa duniani kufanyiwa jambo kama hilo ni kawaida kabisa! Kwa mfano mtu anaweza kuuawa ili kuficha ukweli ambao unaweza kuathiri maslahi ya wengine!!
 
kwani ni uongo kwamba tanesco wanadaiwa dola millioini 363
Huyu naye yaani ukweli hupo na hata pro alisema wataenda kukopa pesa nje sasa unafikiri wao watakupa pesa pasi na kuangalia biashara yako na faida
 
Back
Top Bottom