Sauti kutoka Kaburini - Ni Jambo la Kijinga Kutegemea Mikopo Kujiletea Maendeleo...

..manunuzi ya ndege yamegharimu trillion ngapi?

..halafu Atcl inaingiza hasara kiasi gani kila mwaka?

..1.3 trillion anayoizungumzia Rais ni mkopo nafuu wa athari za covid 19.

..Kusingekuwepo na janga la covid 19 huo mkopo usingekuwepo kwa terms hizo.

..Na according to Madame President sehemu ya hiyo 1.3 trillion imetumika kulipa mikopo iliyo-mature. Maana yake ni kwamba tuna-struggle kulipa mikopo.

..Mimi wasiwasi wangu ni kama jinsi tunavyokwenda mbele tunajenga uwezo wa ku-manage our finances.

..Kama tunajenga uwezo wa kulipa madeni yetu. Kama tunaongeza walipa kodi wa viwango mbalimbali. Kama Watz wanazalisha zaidi.

..Mwisho, katika awamu ya Mkapa Tz ilikuwa a Highly Indebted Poor Country. Tukapigana mpaka tukasamehewa baadhi ya madeni.

..Sasa tujiulize, jama tunarudi kuwa HIPC, au tuna-move away from that kuelekea kwenye prosperity.
Mimi ushauri wangu kwa serikali kuongeza wigo wa walipa kodi tu, wasahau mambo yao ya azimio la Arusha, sijui ujamaa
 
Vyovyote iwavyo, kukopa trillioni 10 ndani ya miezi 9 kwa ajili ya madawati tena bila idhini ya bunge ni jambo lisilokubalika, na hili ni lazima liondoke na mtu!

Wapi imeandikwa zimekopwa 10 Trillion na ni kwaajili ya madawati. Mkopo uliokopwa ni 1.3T kwaajili ya madarasa 15000 na tumeyaona
 
Mimi nimesikitika sana baada ya kumsikia Rais akisema jana kwamba Waziri wa fedha kamshauri yeye (Rais) kwamba sehemu ya mkopo itumike kulipia mikopo ambayo tayari imemature.

Hapo inaonesha kwamba kama Taifa tumekwama hatuna option nyingine.

Mzee wako akikopa mikopo ya muda mfupi tena ya kibiashara alikuwa anawaza nini? Ndo madeni yake hayo tunapambana kuyalipa
 
Trillion 2 za Covid 19 ziliemda kwenye madarasa na madawati, dollar bilioni 3 (trillion 8) zimeenda kwenye madarasa na madawati na kidogo zimepelekwa Zanzibar, na hata tozo za miamala 100bn per month zinaenda kwenye madarasa na madawati, piga hesabu wewe mwenyewe

Leta source ya taarifa yako
 
Wakati Magufuli anakopa , walikaa kimya na jamaa alikuwa anakopa Mikopo ya kibiashara


..katika kukopa Magufuli alikuwa pamoja na Samia, Majaliwa, Dr.Mpango,...serikali nzima kwa ujumla.

..Na walikuwa wanadanganya wananchi kuwa miradi inatekelezwa kwa fedha za ndani. Kwamba hadaiwi mtu.

..Wanatakiwa waeleze walikopa wapi, kwa ajili ya nini, na kwa masharti gani.
 
Trillion 2 za Covid 19 ziliemda kwenye madarasa na madawati, dollar bilioni 3 (trillion 8) zimeenda kwenye madarasa na madawati na kidogo zimepelekwa Zanzibar, na hata tozo za miamala 100bn per month zinaenda kwenye madarasa na madawati, piga hesabu wewe mwenyewe
Ni mwezi upi serikal imekusanya bil100 kwa tozo? Kila mwezi inapatikan chin ya 50 wee hiyo 100 umeipata wapi mbumbumbu wew
 
Wapi imeandikwa zimekopwa 10 Trillion na ni kwaajili ya madawati. Mkopo uliokopwa ni 1.3T kwaajili ya madarasa 15000 na tumeyaona
Pesa iliyokopwa jumla ni Trillion 10 ndani ya miezi 9. Kuna Trillion 2 pesa za Covid19 zimeenda kwenye madarasa na madawati, pia kuna hizo dollar bilioni 3 ambazo ni shs.Trillion 8, zimeenda kwenye madarasa, madawati na Zingine Zanzibar. Na kuna bilioni 100 tozo za miamala ya kila mwezi tunakatwa ambazo pia ni za madarasa, madawati na Zahanati, sasa piga hesabu wewe mwenyewe.
 
MASKINI AKIKOPA KAPATWA, TAJIRI AKIKOPA KAPATA

Na. M. M. Mwanakijiji
Tuangalie ukweli wa hoja hii na tulinganishe nani yuko karibu zaidi na hili kati ya wanaotetea mikopo isiyoulizwa na wale wanaouliza kuhusu mikopo na misaada ya kigeni. Yanayofuatia siyo maneno yangu nimeyanukuu tu.

Njia moja tunayotumia kujaribu kuepukana na lazima hii ya kukiri kodi zaidi ikiwa twataka fedha zaidi ni kutilia sana mkazo fedha za kutoka nje ya Tanzania. Fedha hizi za kutoka nje ni za aina tatu:-

(a) Zawadi: Yaani Serikali ya nje iipe Serikali yetu fedha za bure tu kama sadaka kwa ajili ya mpango fulani wa maendeleo. Wakati mwingine shirika lo lote la nje liipe Serikali yetu au Shirika jingine katika nchi yetu msaada fulani kwa ajili ya maendeleo.

(b) Mkopo: Sehemu kubwa ya fedha tunazotazamia kupata kutoka nchi za kigeni si zawadi au sadaka, bali ni mkopo. Serikali ya nje au Shirika la nje, kama vile Benki, hukopesha Serikali yetu fedha fulani kwa ajili ya kazi zetu za maendeleo. Mkopo huu huwa una masharti yake ya kulipa, kama vile muda wa kulipa, na kima cha faida.

(c) Raslimali ya Kibiashara: Aina ya tatu ambayo pia ni kubwa kuliko ya kwanza, ni ile ya fedha za watu au makampuni yanayotaka kuja katika nchi yetu kuanzisha shughuli mbali mbali za uchumi kwa manufaa yao wenyewe. Na sharti kubwa walitakalo jamaa hawa wenye fedha zao ni kwamba shughuli yenyewe iwe ni ya faida – kwao – na pia kwamba Serikali iwaruhusu kuondoa faida hiyo Tanzania na kuipeleka kwao. Hupenda pia kwa jumla Serikali iwe na siasa wanayokubaliana nayo au ambayo haihatarishi uchumi wao.

Hizo ndizo njia tatu kubwa za kupata fedha kutoka nje ya nchi yetu. Kuna mazungumzo mengi ajabu juu ya jambo hili la kupata fedha kutoka nchi za kigeni. Serikali yetu na viongozi wetu wa makundi mbalimbali hawaachi kufikiria njia za kupata fedha kutoka nje.

Na tukizipata au japo tukipata ahadi tu ya kuzipata mara magazeti yetu, au radio zetu na viongozi wetu hutangaza jambo hilo ili kila mtu ajue kuwa neema imekuja au iko njiani inakuja. Tukipata msaada hutangaza; tukipata mkopo hutangaza; tukipata kiwanda kipya hutangaza; tukiahidiwa msaada, mkopo au kiwanda kipya hutangaza. Japo tukianza mazungumzo tu na nchi au shirika la kigeni juu ya msaada, mkopo au kiwanda, mara hutangaza japo hatuna hakika ya matokeo ya mazungumzo hayo. Na kisa? Ni kuwajulisha wananchi kwamba, tunaanza mazungumzo ya neema!

TUSITEGEMEE FEDHA KULETA MAENDELEO

Ni jambo la kijinga kuchagua fedha kuwa ndiyo chombo chetu kikubwa cha maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni maskini. Ni ujinga vile vile, kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa tunaweza kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea fedha za kutoka nje badala ya fedha zetu wenyewe. Ni ujinga kwa sababu mbili. Kwanza, hatuwezi kuzipata. Ni kweli kwamba zipo nchi ambazo zaweza na zapenda kutusaidia.

Lakini hakuna nchi moja duniani ambayo iko tayari kutupa misaada au mikopo au kuja kujenga viwanda katika nchi yetu kutimiza shabaha zake zote za maendeleo. Nchi zenye dhiki ni nyingi sana duniani. Na hata kama nchi zote zenye neema zingekubali kuzisaidia nchi zenye dhiki, bado ingekuwa msaada huo hautoshi. Lakini nchi zenye neema hazitakubali. Hata katika nchi ile ile, matajiri huwa hawatoi fedha zao kwa hiari ili zisaidie Serikali kuondoa dhiki. Njia ya kuzipata fedha za matajiri ili zisaidie umma ni kuwatoza kodi wakipenda wasipende. Hata hivyo huwa hazitoshi.

Ndiyo maana japo tungewakamua vipi wnanachi na wakazi wa Tanzania, matajiri na maskini, hatuwezi kupata fedha za kutosha kutimiza mipango yetu ya maendeleo. Wala duniani hakuna Serikali ambayo yaweza kuyatoza kodi mataifa yenye neema, yakipenda yasipende, ili kusaidia mataifa yenye dhiki. Hata hizo zisingelitosha. Hakuna Serikali ya Dunia nzima.
Fedha ambazo nchi zenye neema hutoa huwa kwa wema wao, au hiari yao au kwa manufaa yao wenyewe. Haiwezekani basi, tupate fedha za ktuosha kwa njia hiyo.

MISAADA NA MIKOPO VITAHATARISHA UHURU WETU

Pili, japo kama tungeweza kuzipata; hivyo ndivyo tunavyotaka kweli? Kujitawala ni kujitegemea. Kujitawala kwa kweli hakuwezekani ikiwa Taifa moja linategemea misaada na mikopo ya Taifa jingine kwa maendeleo yake. Hata kama pangetokea Taifa au mataifa ambayo yako tayari kutupa fedha zote tunazohitaji kuendesha mipango yetu ya maendeleo isingekuwa sawa kwa nchi yetu kuipokea misaada hiyo bila kujiuliza matokeo yake yatakuwa nini kwa Uhuru wetu na uzima wetu.

Msaada ambao ni kama chombo cha kuongeza juhudi, au nyenzo ya juhudi, ni msaada ambao una manufaa. Lakini msaada unaoweza ukawa sumu ya juhudi si msaada wa kupokea bila kujiuliza maswali. Kadhalika mikopo. Kweli mkopo ni bora kuliko misaada ya “bure”. Mkopo nia yake ni kuongeza jitihada au kuifanya jitihada itoe matunda mengi zaidi. Sharti moja la mkopo huwa ni kuonyesha jinsi utavyoweza kuulipa. Maana yake ni kwamba sharti uonyeshe kuwa unakusudia kuufanyia kazi itakayoleta manufaa ya kukuwezesha kuulipa.

Lakini hata mikopo ina kikomo. Sharti upime uwezo wa kulipa. Tunapokopa fedha kutoka nje mlipaji ni Mtanzania. Na kama tulivyokwisha sema Watanzania ni watu maskini. Kuwabebesha watu maskini mikopo ambayo inawazidi kimo si kuwasaidia bali ni kuwaumiza. Na hasa inapokuwa, mikopo hiyo ambayo wanatakiwa walipe haikuwafaidia wao, bali ilifaidia watu wachache tu.

Na Viwanda vya wenye raslimali zao je? Ni kweli tunavitaka. Hata tumepitisha katika Bunge sheria ya kulinda raslimali ya wageni wanaoanzisha mipango mbali mbali ya uchumi katika nchi yetu. Nia yetu na matumaini yetu ni kuwafanya waone kuwa Tanzania ni nchi inayofaa kuingiza raslimali zao. Kwani raslimali yao itakuwa salama italeta faida. Na faida hiyo wenyewe wataweza kuiondoa bila vipangimizi. Tunayo matumaini ya kupata fedha za maendeleo mbali mbali kwa njia hii. Lakini hatuwezi kupata za kutosha.

Lakini hata kama tungeweza kuwaridhika kabisa Wageni hao na Makampuni hayo mpaka yakubali kuanzisha mipango yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi yetu, hivyo ndivyo tunavyotaka kweli? Kama tungeweza kushawishi wenye raslimai wa kutosha kutoka Amerika, na Ulaya kuja kwetu na kuanzisha Viwanda vyote, na mipango mingine yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi hii, hivi kweli tungekubali bila kujiuliza maswali? Tungekubali kweli kuacha uchumi wetu wote uwe mikononi mwa wageni kwa ajili ya kupata faida na kuipeleka katika nchi zao?

Hata kama wasingedai kuhamisha faida na kupeleka makwao, bali faida yote watakayopata wataitumia hapa hapa Tanzania kwa maendeleo zaidi. Hivi kweli tungekubali jambo hili bila kujiuliza hasara zake kwa Taifa letu? Huu Ujamaa tunaosema kuwa ndiyo shabaha yetu tungeujengaje? Twawezaje kutegemea nchi za nje na Kampuni za nje kwa misaada na mikopo na raslimali kwa maendeleo yetu bila kuhatarisha uhuru wetu? Waingereza wana methali isimayo “Amlipaye mwimbaji ndiye huchagua wimbo”. Tutawezaje kutegemea nchi za kigeni na Makampuni ya kigeni kwa sehemu kubwa ya maendeleo yetu bila kuzipa nchi hizo na makampuni hayo sehemu kubwa ya uhuru wetu wa kutenda tupendavyo. Ukweli wenyewe ni kwamba hatuwezi.

Tukariri basi. Tumefanya makosa kuchagua fedha, kitu ambacho hatuna, kiwe ndicho chombo kikubwa cha mipango yetu ya maendeleo. Tunafanya makosa kudhani kuwa tutapata fedha kutoka nchi za kigeni. Kwanza, kwa sababu kwa kweli hatuwezi kupata fedha za kutosha kwa maendeleo yetu. Na pili, hata kama tungeweza, huko kutegemea wengine kungehatarisha uhuru wetu na siasa nyingine za nchi yetu.

Julius Nyerere - Azimio la Arusha (1967) Uk. 13 - 19.

Maswali:
a. Msimamo wa Ndugai kuhusu Mikopo unakaribiana na huu wa Azimio la Arusha
b. Msimamo wa Azimio la Arusha ni potofu na hivyo msimamo wa sasa wa kifikra wa serikali ndio sahihi - tutegemee mikopo na misaada kuleta maendeleo?
Ndugai anashabihiana na msimamo wa Azimio la Arusha
Tukope kwenye uhitaji na fedha zisimamiwe zitumike ipasavyo palipo tegemewa zifanye kazi husika
Pasiwe na upigaji
Viongozi waache unafiki wa kumshabikia rais hata kama anatupeleka kubaya
 
Zamani nilikuwa nanunua gazeti sababu ya maandiko yako mwanakijiji,siku hizi hata haya unayoweka bure jamii forum nashindwa kusoma.
 
Mzee Mwanakijiji naona ubakie msomaji makala za wengine tu siku hizi. Huna mvuto tena. Angalia mataifa yanayoongoza kukopa hapo

View attachment 2069918
nafikiri unaangalia namba kuelewamaana yake. Nchi kama Marekani na nyingine zote za Advanced economies, hazikopi kwa kutafuta mkopeshaji umombe akukopeshe kama tanzania tunavyofanya, wao wanauza governement bonds kwa mtu yeyote, hata wewe unaweza kuzinunua. katika mkopo wa namna hiyo, wauzaji wa hizo bonds ndio wanoweka masharti yake. Tanzania inakopa kwa kwenda kuomba kwenye taasisi za fedha na serikali za nje, na hivyo kukubali masharti ya watoaji mkopo huo. Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo rwanda ilikuwa inauza governement bods kwenye soko la Ulaya, ila sijui kama walifanikiwa. Government bonds ndio mkopo mzuri, kwani serikali haiwezi kuwa mtumwa wa mkopeshaji
 
Wapi imeandikwa zimekopwa 10 Trillion na ni kwaajili ya madawati. Mkopo uliokopwa ni 1.3T kwaajili ya madarasa 15000 na tumeyaona
Kuna trillion 2 zilikopwa kwa ajili ya Covid19, zilienda kwenye madarasa na madawati, pia kuna dollar bilion 3 ambazo ni trillion 8, zimeenda kwenye madarasa, madawati na zingine zimeenda Zanzibar. Pia kuna tozo za miamala tunakatwa bilion 100 kila mwezi kwa ajili ya madarasa, madawati na Zahanati. Piga hesabu wewe mwenyewe
 
Ni mwezi upi serikal imekusanya bil100 kwa tozo? Kila mwezi inapatikan chin ya 50 wee hiyo 100 umeipata wapi mbumbumbu wew
Walitangaza ya mwezi wa 7/8, ya mwezi wa 9 walitangaza wapi? Tozo na kodi za Miamala ni zaidi ya 100bn kwa mwezi, kumbuka kabla ya 50bn za tozo kulikuwa na kodi tayri over 80bn inakusanywa kwenye miamala ya simu
 
Leta source ya taarifa yako
Unataka nikuletee source ya Trillion 2 mkopo wa Covid19? Unataka nikuletee source kwamba wamekopa dollar bilioni 3? Au source kwamba wanakata Tozo na kodi kwenye miamala ya simu 100bn kwa mwezi? Au Source ya kipi?

=================================


D7A121EE-5DD9-4E82-B986-C96009E99C35.jpeg

F6DB5068-82FD-45DF-B4F6-61F5675AF1E2.jpeg
 
Vyovyote iwavyo, kukopa trillioni 10 ndani ya miezi 9 kwa ajili ya madawati tena bila idhini ya bunge ni jambo lisilokubalika, na hili ni lazima liondoke na mtu!
 
Back
Top Bottom