Hivi maendeleo huwa yanaletwa na Chama /serikali?

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,647
1,885
Mimi nafikiri maendeleo hayaletwi na chama au serikali bali na wananchi wenyewe kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa kulipa kodi na kwa kuchagua viongozi sahihi ambao siyo mafisadi bali wacha mungu ambao watawaongoza wananchi kupata maendeleo yao na kwa kusimamia kikamilifu rasilimali za nchi.

Kusema kuwa mkichagua wapinzani hatutawaletea maendeleo ni lugha mfilisi sana.Maana chama au serikali hakina uwezo wakuleta maendeleo kwa watu fulana kama watakuwa hawalipi kodi ,na kwa kufanya kazi kwa bidii.

Hivyo ilitakiwa lugha nzuri kama hii: chagueni viongozi ambao kwa kushilikiana nao tutaunda serikali thabiti ambayo itasimamia kikamilifu maendeleo yenu kupitia rasilimali za nchi na kwa kuwatafutia fursa ili mweze kujipatia kipato kizuri.

Mfano wa kuchagua viongozi wenye uwezo mdogo ni kama pale dr congo. Nchi ina rasilami nyingi za madini, lakini kagama, M23 na wazungu wanawaibia kila kukicha. Wanachi wamebaki kuwa top ten ya walevi africa huku nchi yao ikiwa maskini. Kama chama au serikali kingekuwa na uwezo kuwaletea maendeleo wananchi, basi tusingeona nchi ya kongo vitahaishi na kumbe kuna majizi yanawaibia madini na vito vya thamani sana.
 
Back
Top Bottom