Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,192
- 10,927
Yako mataifa kadhaa ya kiarabu na mataifa ya kiislamau ambayo yameonekana kufanya uzembe katika vita vya Gaza.Hata hivyo taifa la Saudia linaongoza kwa kusaidiana na Marekani kuipa nguvu Israel iue na kuangamiza mpango wa kuundwa kwa taifa la Palestina.
Iran iliahidi mstari mwekundu ukivukwa ingekuwa ndio muda wao kupambana na Israel.Mstari ulipovukwa ndio ikakaa kimya kabisa.
Uturuki chini ya raisi wake ndumila kuwili pamoja na kuwa na nguvu kubwa za kijeshi na kuchangiana bahari na Gaza pia hawajafanya lolote zaidi ya maneno matupu.Kikubwa siku moja kwenye kikao cha bunge waliacha kunywa soda za cocacola na vyakula vyengine vyene nembo za Israel na Marekani. Huenda ni siku hiyo tu.
Jordan na Misri ambao ndio wenye maamuzi ya juu kuhusu usalama wa Israel nazo zimekaa kimya.Wanashindwa kufungua mipaka na kupeleka misaada kwa wahitaji wa Gaza na Palestina yote. Iko siku Jordan iliomba ruhusa kudondosha misaada kwenye kituo chake Gaza na wakaishia hapo hapo
Sasa tuuangazie utapeli na unafiki wa Saudi Arabia.
Kwa miezi kahdaa kulikuwa na tetesi za kukaribia kukamilika kwa mpango wa Saudi Arabia kurudisha uhusiano na Israel mpango uliosimamiwa na Marekani. Kutokea kwa ghafla kwa vita baina ya Hamas na Israel ndiko kulikotibua mpango huo.
Nchi zote mbili hizo katika kipindi hiki zimekuwa zikifanya diplomasia za hadaa za kuipa muda Israel ifanye mauaji inavyotaka kwa wanawake na watoto wa Gaza.
Mapema wiki iliyopita Saudi Arabia iliingia gharama kubwa ya kuwakushanya maraisi na wawakilishi wa nchi zaidi ya 50 za kiarabu na waislamu kujadili vita hivyo.
Japo mkutano huo ulifanyika katikati ya vita na mabomu mabaya ya kuua umati na bado hakukuwa na cha maana kilichojadiliwa wala kilichokubaliwa.
Leo wakati shule na mahospitali yenye watoto wadogo na wachanga vikipigwa na kuuliwa bado Saudi Arabia imepanga kuwakushanya mawaziri wa nchi za nje wa nchi za kiarabu ili waende China kuzungumzia vita vya Gaza tena wiki ijayo na sio leo leo.
Kwa kasi ya kuuliwa watoto na kunyimwa chakula na maji wiki ijayo inaweza ikawa ni muda wa kuzika umati ulioangamia.
Kilichotakiwa leo ni kuchukua hatua za papo kwa papo kushinikiza kusimamishwa vita.Saudia ina uwezo mkubwa kuliko wa wanamgambo wa Houth wa Yemen. Kinachotakiwa ni vitendo vyake na sio maneno na ahadi na hadaa mbele ya wajibu wake.