Ni aibu kubwa sana kwa CHADEMA kufanya maandalizi ya maandamano Arusha wakati wananchi na mkoa upo kwenye majonzi na simanzi ya kupoteza wapendwa wao

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,272
9,716
Ndugu zangu Watanzania,

Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa CHADEMA kuendelea kufanya maandalizi na hamasa ya magari yao kuwa kesho wanafanya maandamano na kuwataka watu washiriki katika maandamano hayo, wakati mkoa mzima wa Arusha na wananchi wake wapo katika majonzi na simanzi za kupoteza wapendwa wao waliokufa katika ajali. Mkoa kwa sasa unalia, unabubujikwa machozi, una simanzi, umepigwa na ganzi, unasononeka, mkoa wa Arusha umekosa nguvu, morali na nguvu za kufanya kazi kwa kuwa umepatwa na msiba wa mkoa.

Watu wa Arusha kwa sasa wana majeraha, wana maumivu makali mioyoni mwao. Wengine bado wanawauguza wapendwa wao mahospitalini, wengine bado wapo vyumba vya wagonjwa mahututi, wengine bado wapo na vilio katika kaya zao, wengine bado hawaelewi hata hatima ya maisha yao kwa kuwa wamepoteza wale waliokuwa wanawategemea katika kuwasomesha na kuendesha familia. Wengine wamebaki yatima, wajane na hawajuwi ni vipi wanakwenda kuanza maisha mapya yaliyobadilika ghafla kwa kupoteza wapendwa wao ndani ya dakika moja.

Chama chenye busara, hekima, utu, ubinadamu, uungwana, upendo, hisia na kuguswa na matatizo ya watu kisingeendelea na ratiba ya maandamano kwa siku ya kesho. Kingeungana na wana Arusha kutoa pole kwa familia zilizopata msiba. Kingeungana na kuunganisha wanachama wake kwenda mahospitalini kuwajulia hali wagonjwa waliopata ajali na wengineo pamoja na kujitolea damu kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu. Kingenunua vitu na kusaidia wenye uhitaji, kingeomba hata nafasi ya kwenda kufanya usafi kwenye hospitali hata moja kuonyesha kuwa kinaungana na wote walio mahospitalini na kuwatakia uponyaji wa haraka.

Chama makini kingefanya haya kwa kutambua kuwa kitapata kura kutoka kwa hawa hawa ambao leo ndio wana majonzi na simanzi na wanahitaji faraja kubwa sana kwa wakati huu, wanahitaji maombi na kutiwa nguvu wakati huu wa giza katika mioyo yao. Kingetambua kuwa watu hawa waliopatwa na msiba hawahitaji neno maandamano wala neno katiba mpya katika mioyo yao wakati huu ,bali wanahitaji neno la faraja la kuponya mioyo yao iliyo sagika kwa maumivu makali.

Hivyo chama makini kingesogeza mbele na kupanga siku nyingine ya maandamano. Kwa hakika kingekuwa kimegusa hisia za Watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama wala makabila yao wala imani zao za dini. Kingeteka mioyo ya Watanzania wote. Lakini kwa sababu chama hakina mwenye kuwaza haya ndio maana kinaendelea kusonga mbele kama kipofu gizani.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa CHADEMA kuendelea kufanya maandalizi na hamasa ya magari yao kuwa kesho wanafanya maandamano na kuwataka watu washiriki katika maandamano hayo,wakati mkoa mzima wa Arusha na wananchi wake wapo katika majonzi na simanzi za kupoteza wapendwa wao waliokufa katika ajali. Mkoa kwa sasa unalia,unabubujikwa machozi,una simanzi,umepigwa na ganzi,unasononeka, mkoa wa Arusha umekosa nguvu,morali na nguvu za kufanya kazi kwa kuwa umepatwa na msiba wa mkoa.

Watu wa Arusha kwa sasa wana majeraha,wana maumivu makali mioyoni mwao. Wengine bado wanawauguza wapendwa wao mahospitalini,wengine bado wapo vyumba vya wagonjwa mahututi,wengine bado wapo na vilio katika kaya zao,wengine bado hawaelewi hata hatima ya maisha yao kwa kuwa wamepoteza wale waliokuwa wanawategemea katika kuwasomesha na kuendesha familia. Wengine wamebaki yatima,wajane na hawajuwi ni vipi wanakwenda kuanza maisha mapya yaliyobadilika ghafla kwa kupoteza wapendwa wao ndani ya dakika moja.

Chama chenye busara,hekima ,utu, ubinadamu,uungwana,upendo,hisia na kuguswa na matatizo ya watu kisingeendelea na ratiba ya maandamano kwa siku ya kesho.kingeungana na wana Arusha kutoa pole kwa familia zilizopata msiba.kingeungana na kuunganisha wanachama wake kwenda mahospitalini kuwajulia hali wagonjwa waliopata ajali na wengineo pamoja na kujitolea damu kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu.kingenunua vitu na kusaidia wenye uhitaji,kingeomba hata nafasi ya kwenda kufanya usafi kwenye hospitali hata moja kuonyesha kuwa kinaungana na wote walio mahospitalini na kuwatakia uponyaji wa haraka.

Chama makini kingefanya haya kwa kutambua kuwa kitapata kura kutoka kwa hawa hawa ambao leo ndio wana majibu na simanzi na wanahitaji faraja kubwa sana kwa wakati huu,wanahitaji maombi na kutiwa nguvu wakati huu wa giza katika mioyo yao. Kingetambua kuwa watu hawa waliopatwa na msiba hawahitaji neno maandamano wala neno katiba mpya katika mioyo yao bali wanahitaji neno ya kuponya mioyo yao iliyo sagika kwa maumivu makali.

Hivyo chama makini kingesogeza mbele na kupanga siku nyingine ya maandamano.kwa hakika kingekuwa kimegusa hisia za watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama wala makabila yao wala imani zao za dini.kingeteka mioyo ya watanzania wote.lakini kwa sababu chama hakina mwenye kuwaza haya ndio maana kinaendelea kusonga mbele kama kipofu gizani.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Mpaka leo bado haujalamba uteuzi !.
 
Ni aibu vilevile Taifa likiwa kwenye Giza totolo,Upungufu wa Sukari & Ukosefu wa Maji safi na salama kwa wananchi nchi nzima Halafu Bi Chaudele kutwa nzima kiguu na njia kwenye mataifa ya watu!
Kwa sasa umeme unapatikana kwa 85% baada ya mtambo kuwashwa katika bwawa la mwalimu Nyerere na kutoa megawati 235 zilizounganishwa katika grid ya Taifa.
 
Asilimia hizo 85% zinapatikana huko kwao Bi Chaudele Kizimkazi,lakini mimi na wewe bado tutaendelea kuishi kwenye Tanzagiza hadi Yesu atakaporudi!
Kwa sasa nchi yote inakwenda kuwa katika mwanga .pia uwe na adabu kwa Mheshimiwa Rais wetu
 
Sishabikii upande wowote lakini nadhani sababu nikwamba maandamano na vibali vyake inachukua na kupitia michakato mirefu.

Ngoja tuone labda maandamano yatahamasisha hata kuwashika mkono wafiwa pamoja na majeruhi
 
Sishabikii upande wowote lakini nadhani sababu nikwamba maandamano na vibali vyake inachukua na kupitia michakato mirefu.

Ngoja tuone labda maandamano yatahamasisha hata kuwashika mkono wafiwa pamoja na majeruhi
Kibali kinatokewa na polisi na wala hakuna mlolongo wowote ule.kwa hiyo ilikuwa ni suala la kutoa taarifa polisi juu ya kuahirishwa kwa maandamano na sababu zake.
 
Back
Top Bottom