Suala la Bandari: Ni Wakati sahihi sasa Watanzania wa hali zote kuwekeza kwenye Bandari yao ili kuleta Mantiki kwenye umiliki wao

Misozwe

Member
Dec 23, 2022
21
26

Kinadharia, rasilimali za Tanzania, ikiwemo bandari, ni mali ya wananchi (umma) wa Tanzania. Kiuhalisia, mwenye maamuzi ya kuhusu lolote linaloweza kufanyika kwenye bandari ni Rais wa JMT. Kutokana na huu mjadala unaoendelea sasa, pengine ni wakati muafaka Watanzania wakaanza kuwekeza kidogo kidogo kwenye bandari, hata kama itachukua miaka 100 hilo kuwezekana sioni tatizo.

Bandari ilikuwepo toka mwaka 1500 bila "ufanisi", kusubiria miaka mingine 100 kuna shida gani. Hatua hii itatuhakikishia umiliki wa bandari kwa vizazi vyote vya mbeleni.

Inawezekanaje?

Bandari ina thamani kubwa na biashara kubwa sana ndio maana DP World wako interested. Serikali labda tuseme haina hela za ununuzi vifaa hitajika, ingawa kiasi cha investment inayotakiwa hakijawahi kutajwa. Tujue, tuelezwe, hata kama, kwa mfano, ni shilingi trillioni 10.

Sisi tunao wafanyabiashara wakubwa kama Bakhresa, Mo Dewji, Rostam, Angelina wa TPSF, wafanyabishara wa Kariakoo wana mitaji mikubwa tu, na wafanyabiashara wengi tu huku nchini, kuna mabenki ya biashara, kwanini tusiwashirikishe?

Unaweza sema wafanyabiashara wanaweza kuwekeza lakini hatuna wataalamu wa kuendesha bandari kisasa; sasa, kama tunaweza kuajiri makocha wa timu za taifa kutoka popote duniani na kuwatimua pale wasipofikisha malengo, kwanini ishindikane kuajiri wataalamu wa bandari toka popote duniani na kuwapa malengo? Mbona DP World wanatumia njia hii ya kuajiri wataalamu na wanafanikiwa?

Kuna njia nyingi za kupata mitaji. Mfano mmoja tu, tuko watu milioni 60 (yes, kuna watoto, wagonjwa, wazee, wasiojiweza, n.k. katika hao), lakini tukifanya kwa wastani kila mtu akachanga shilingi 100 tu kwa siku (zinaweza kuwa nyingi zaidi au kidogo kutokana na uwezo) kama hisa (au watu milioni 6 wakachanga shilingi 1000 kila siku, jambo ambalo kwa takwimu za biashara ya miamala kwa mitandao ya simu linawezekana), zinaweza patikana shilingi bilion 6 kwa siku tu; je kwa mwezi, kwa mwaka?

Baada ya miaka michache si tutakuwa tumepata mtaji tayari? Hatuna haraka, bandari haiwezi kuhama. Watanzania tunaweza, tusijidharau.
 
Wafanyabiashara wengi wa kibongo ni wezi tu, waliopata mali kwa ujanjaujanja kwa kushirikiana na viongozi wa serikali kwa kuoa huduma fake kisha kugawana hela.

Mfano ku supply uniform hewa na wanapiga hela ndefu hao ndo wanapitisha mizigo bila kulipia ushuru hawawezi kuendesha hiyo bandari
 
Wafanyabiashara wengi wa kibongo ni wezi tu, waliopata mali kwa ujanjaujanja kwa kushirikiana na viongozi wa serikali kwa kuoa huduma fake kisha kugawana hela.

Mfano ku supply uniform hewa na wanapiga hela ndefu hao ndo wanapitisha mizigo bila kulipia ushuru hawawezi kuendesha hiyo bandari
Teknolojia inawezesha kupunguza mianya ya upotevu, malipo yote yatakuwa yanafanyika kielektroniki na mteja kufikishiwa mzigo mpaka mlangoni. Itapunguza upigaji na rushwa kwa kiasi kikubwa
 
Tuwape Mama ntilie waiendeshe.
Mama ntilie wana uwezo wa kuwa sehemu ya wawekezaji, kwa umoja wao. Wataalamu wataendesha bandari. Nikukumbushe tu, Bakhresa miaka ile alianza biashara kwa kufanya uchuuzi, more or less kama mama ntilie wa kipindi hiki. Hivi saa ameajiri wataalamu wengi toka nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom