Sasa ni rasmi ukiwa Waziri Tanzania usipokuwa Bilionea umejitakia tu Mwenyewe kwa Ujinga wako

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,606
108,978
Kuwa na kiasi cha Pesa cha Kuanzia Shilingi Bilioni Moja katika Akaunti zao ni jambo la kawaida mno kama ilivyo katika Kushindana Kwao kuitafuta Shilingi Trilioni ili wawe na uhakika wa Maisha yao ya Kiujumla na Fedha ya uhakika ya kuwarejesha tena Bungeni kwa Kushinda katika Majimbo yao kila Uchaguzi Mkuu ukiwadia.

Mtakaonielewa GENTAMYCINE hasa kwa huu Uzi wangu kwa Kuusoma between the lines nawatakieni kila la kheri huku Mimi mifukoni mwangu kwa sasa nikiwa na Shilingi Elfu Moja tu na sijui hata nyingine nitaipata wapi kutokana na Maisha magumu na ya Dhiki Kubwa niliyonayo.

Ewe Mwenyezi Mungu fanya Maajabu yako Kwangu GENTAMYCINE ili nami Jina langu kamili la Kalemera Rwigyema Mazimpaka Kadogoo Kisungura lifike rasmi kwa Mteuwaji Rais Samia nami niwe Waziri ili haraka sana nianze kuitafuta Shilingi Milioni 500 kisha niwatafute Wenzangu wenye Shilingi Bilioni katika Akaunti zao kisha baadae nianze kuitafuta Trilioni kama wanavyoitafuta walioko sasa.
 
Chapa kazi kwanguvu sana mkuu utatoboa,achakuchagua kazi.
JamiiForums-1413076056.jpg
 
Utakuwa fala ukiwa waziri wa sekta kama mawasiliano, biashara na viwanda, usafirishaji na uchukuzi, fedha, nishati na madini kisha ukose angalau billion 100 kwenye account zako katika utawala huu wa kambale 😂!!! Utakuwa fala mno.

Uwaziri ambao hauna mchongo ni wa Sanaa na utamaduni kule aliko ndugu yetu Mwinjuma Khamis. Labda nae aunde program inayomake sense ya kuchota billions of money.
 
Pesa unaletewa kwenye viroba.
Daaaaahh
 
Back
Top Bottom