Na mbaya zaidi mtoa mada ni mbishi na inaonekana haelewi hii mambo. Anaongelea limit ya madeni na wakati huohuo anatoa mfano wa mkulima Stein aliyekopa enzi sijui za mwalimu huko na anakuja kudai leo, sasa sijui argument yake anaielewa kweli?
Ninakujibu kwa mara ya mwisho kwa sababu moja tu: naamini kuna mtu/watu anae/wanaofuatilia hii issue (kwa kuwa ame/wamekutana nayo). Na uzoefu wangu binafsi umenifanya nitambue kuwa serikali kupitia idara na taasisi zake zinawaonea watu kwa kuwa wanajua watu wengi hawajui haki zao. Na bahati mbaya zaidi watu wanaoonewa wanaamini kila kitu wanachoambiwa na waonezi wao.
Hata huku mtaani huwa nawasaidia watu wengi (wakati mwingine free of charges) ili wapate haki zao lakini kwa wao kutimiza wajibu wao pia kwa matakwa ya kisheria.
Obviously; WEWE ni mmoja wa wale wanao mislead watu. Hapa ama ni kweli hujui au unajifanya huelewi tofauti ya essence kati ya deni la mkulima Stein kwa serikali na TRA kumdai mlipakodi kinyume cha sheria. I will explain kwa manufaa ya anaefuatilia kwa nia ya kujua (and on this I am 110% certain kuwa ndivyo sheria ilivyo unless ibadilishwe):
Mtu (hata taasisi) ikiwasilisha madai ya kulipwa deni lake within time limits huwa hakuna limitations ya hilo deni kulipwa mpaka litakapokuwa settled kwa namna ambayo wahusika wameridhia. Mkulima Stein aliwasilisha madai yake ndani ya muda, serikali haikuwahi kumlipa deni lake; kwa hiyo limitation ya kudai deni HAIPO. Lakini asingedai within stipulated time leo hii HAKUNA mahakama ambayo inge-entartain madai yake.
Kwa upande wa tax management ya nchi hii mlipakodi anaetakiwa ku-file returns anapaswa kufanya hivyo within six months tangu afunge hesabu zake za mwaka husika. Hesabu hizo zitawezesha computation ya tax liability (kama alipata faida kwa mwaka husika). Asipofanya hivyo kuna penalty na interests anazopaswa kulipa. Mlipakodi asipowasilisha returns zake na ama kulipa au kuingia makubaliano jinsi ya kulipa kodi inayotakiwa HAWEZI KUPATA TAX CLEARANCE.
Lakini TRA wana haki ya kukagua hesabu zilizowasilishwa na mlipakodi husika ili kujiridhisha kuwa hesabu zilikuwa sahihi (na kama kuna material omissions basi TRA watatoa additional assessment ambako pia kunaweza kuhusisha penalties na interests). Lakini TRA wapo limited kufanya tax audit ndani ya miaka 5 tangu returns zilipofanyika. Na ndio maana mfanyabiashara anapaswa kutunza source documents zake (invoices, receipts, contracts etc) kwa angalau miaka 5 kwa kuwa anaweza kudaiwa kuzionyesha anytime ndani ya miaka hiyo mitano (unless ni payroll related information maana hizo zina time limits tofauti).
Katika mazingira ya namna hii; aniambie mtu hapa (mie mbumbumbu) TRA wamepata wapi uhalali wa kumdai mtu "kodi" ya 2006 (miaka 14 iliyopita) ambae:
(a) amekuwa ana-file returns consistently miaka yote
(b) amekuwa anafanyiwa tax audit miaka yote na hajawahi kudaiwa chochote
(c) amekuwa anapata tax clearance kwa miaka yote.