Sasa ni Rasmi Magufuli amegoma kufa!

Ngoja tuone unachobisha nini maana mwaka wa tatu sasa bado magufuli anaongoza taifa kwa kauli na hotuba zake. Magufuli haters kina kipara bado wanapambana nae huku wakiabika tu mbele ya umma wa wananchi.
Una miaka Mingapi??
Nyerere Alipofariki Bado hotuba zake ziliongoza taifa mpaka miaka ya 2010s ndo walianza kufuata sheria badala ya hotuba za mwalimu..
Nyererw aliendelea kuishi kwa wananchi..

nakumbuka mwaka 2000 taifa walitanganza kupandisha Soda kutoka Tsh 150 mpaka Tsh 250 wakasema Hiyo Tsh 100 ni kwa ajili ya Rambirambi au kumbukumbu ya mwalimu..

So Nyerere watu waliamini hajafa na kuna wengine mpaka Leo wanaamini hajafa
 
Kumbe? Sasa ilikuaje akashindwa wasweka ndani majizi ya mali za CCM? Au waliotajwa ripoti ya makinikia?
Sasa ilikuaje? Ni aina gani ya swali umeuliza mkuu! Mbona limekaa kiumbeya umbeya!

ulikuwa huoni anachokifanya pindi yupo hai?
unataka nitumie nguvu kukueleza?
 
Kumbuka huyu ana siku maalum. Lakini mwamba JPM pamoja na siku ya kifo chake kuingizwa mambo mengine ila bado anaishi mioyoni mwa watu. Ipo siku ukweli wa kifo chake utawekwa wazi! Tukazane tu na maombi
Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi muovu bila damu kumwagika.
 
Sasa ilikuaje? Ni aina gani ya swali umeuliza mkuu! Mbona limekaa kiumbeya umbeya!

ulikuwa huoni anachokifanya pindi yupo hai?
unataka nitumie nguvu kukueleza?
Tuliona alivyopora 200b kutoka kwenye mfuko wa korosho, hakutosheka akatuma wanajeshi kununua korosho za wakulima kwa shuruti. Na tuliona nguvu yake kubwa kwa lile kundi lake la watekaji maarufu kama watu wasiojulikana.
 
Tuliona alivyopora 200b kutoka kwenye mfuko wa korosho, hakutosheka akatuma wanajeshi kununua korosho za wakulima kwa shuruti. Na tuliona nguvu yake kubwa kwa lile kundi lake kwa watekaji maarufu kama watu wasiojulikana.
Hiyo ni sehemu ya kazi pia.
Wakati mwingine ukombozi damu inamwagika!

Wengine kusikia lazima damu ziwatoke masikioni.

Leo huo upinzani umelifanyia nini taifa mbona ni wachumia matumbo tu! Ulitegemea watu wa namna hiyo wafanyweje?

Huwezi kutaka maendeleo ubaki unawachekea watu wajinga kama hao unaowatetea! Lazima uonyeshe udume kwelikweli.

Shukuruni sana Mungu alimchukua mapema! Hakika mngenyooka tu.
 
Wamekufa viongozi wengi wa nchi hii, lakini wakati wote Magufuli anaonekana kuongelewa kila mara na kila sehemu.

Wengine wanasema angekuwepo tungekuwa nchi ya ahadi kwa sasa, wengine wanasema bwana ya nyerere lingekuwa limeshaisha na hivyo mgawo wa umeme tungekuwa tunausikia tu.

Treni Dar Dodoma ingekuwa tayari. Upigaji wa hera za umma ungekuwa mdogo sana.

Hadi 2030 tutasikia mengi.

Jana watu walilia, mkuu wa majeshi mtaafu alilia.
ndio maana ya "Watu Wazuri Hawafi "
 
Hiyo ni sehemu ya kazi pia.
Wakati mwingine ukombozi damu inamwagika!

Wengine kusikia lazima damu ziwatoke masikioni.

Leo huo upinzani umelifanyia nini taifa mbona ni wachumia matumbo tu! Ulitegemea watu wa namna hiyo wafanyweje?

Huwezi kutaka maendeleo ubaki unawachekea watu wajinga kama hao unaowatetea! Lazima uonyeshe udume kwelikweli.

Shukuruni sana Mungu alimchukua mapema! Hakika mngenyooka tu.
Amenyooka yeye.
 
Wamekufa viongozi wengi wa nchi hii, lakini wakati wote Magufuli anaonekana kuongelewa kila mara na kila sehemu.

Wengine wanasema angekuwepo tungekuwa nchi ya ahadi kwa sasa, wengine wanasema bwana ya Nyerere lingekuwa limeshaisha na hivyo mgawo wa umeme tungekuwa tunausikia tu.

Treni Dar Dodoma ingekuwa tayari. Upigaji wa hela za umma ungekuwa mdogo sana.

Hadi 2030 tutasikia mengi.

Jana watu walilia, mkuu wa majeshi mstaafu alilia.
Hakika!
 
Sasa ilikuaje? Ni aina gani ya swali umeuliza mkuu! Mbona limekaa kiumbeya umbeya!

ulikuwa huoni anachokifanya pindi yupo hai?
unataka nitumie nguvu kukueleza?
Nimeuliza specifically... kamati ya Bashiru ilitaja mali zote zilizokwapuliwa pamoja na majina ya wahusika waliokua zaidi ya 500. Kwanini kesi ya jinai haipelekwi mahakamani?

Niambie kwanini alishindwa? Ilihali mnamsifia alinyoosha mafisadi
 
Ahahahaha hizi ndoto za mchana.. Mwambie aende pale Tanesco azuie mgao wa umeme kama enzi zake. Au auende pale Magufuli bus terminal akatukane kwanini stand nzima inanuka kinyesi kama anaweza
 
Anawezaje kufa yule mwamba!
Kile killikuwa kichwa haswaa! Wajinga wajinga walinyooka.

Yule dingi noma sana. Akisema sitaki ujinga anamaanisha na zile kauli zake kama umevurunda.
Unaweza kuzimua ukisia sauti yake.

Mola amupe pumziko la milele Jiwe
 
Nimeuliza specifically... kamati ya Bashiru ilitaja mali zote zilizokwapuliwa pamoja na majina ya wahusika waliokua zaidi ya 500. Kwanini kesi ya jinai haipelekwi mahakamani?

Niambie kwanini alishindwa? Ilihali mnamsifia alinyoosha mafisadi
Mfumo wa nchi hii.. huko mahakamani ni Bure kabisa.

Bora tu aliamua Kutumbua.
 
Kiongozi aliyegoma Kufa kwa miaka 20 ni Nyerere Peke yake
Akili zako ni ndogo sana .... HAKUNA KAMA JPM ALIKUTA NCHI IMECHAFUKA KIFISADI ...MFUMO MZIMA WA SERIKALI ULIKUWA CHINI YA RAIA FEKI NA MAFISADI..TOFAUTI NA NYERERE ...NYERERE KAPEWA NCHI IKIWA SAFI SANA KWENYE NYOYO ZA WATU.
 
Back
Top Bottom