Kwa hili janga la umeme nahisi sasa watanzania wameelewa Magufuli aliposema yeye ni Rais wa wanyonge

live on

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
791
1,266
Magufuli alipokuwa anajiita Raisi wa wanyonge wachache sana ndio tuliyomuelewa ila Kwa Sasa na hili janga la umeme kukatika mara 10 Kila siku Kwa muda wa zaidi miezi 3 Hadi hata wale matahira nahisi Sasa wamesha muelewa Magufuli Kwa Nini alijiita Raisi wa wanyonge

Hu Sasa mwezi 3 umeme unakatwa mfululizo Kila siku mara 10 au zaidi wanyonge wameuliza shida nini hakuna aliyewajibu

Katika hili wananchi wanyonge ndio wanaumia na hawana wa kuwatetea wakipaza sauti hakuna anayejali wao ndio kwanza wapo bize na ma V8 na safari zao za Dar to Dodoma kesho yake wanageuza Dodoma to Dar

Hata ukiangalia matangazo ya solar katika TV siku hizi yamebadirika Yanawalenga watu wa mjini
Tangazo linaanza watu wanaangalia mpira umeme unakatika wanaanbiwa wakanunue solar

Wakati zamani matangazo ya solar yalikuwa yanawalenga watu wa vijijini Yani maeneo ambayo umeme bado haujafika ila Kwa Sasa hakuna tofauti kati ya mijini na vijijini maana mda wote umeme hakuna

Tuongee tu ukweli mambo haya yanayofanywa na Tanesco Kama Magufuli angekuwepo hivi kweli Kuna mtu angebaki pale Tanesco?

Kuna familia ambazo Ili wapate pesa ya kula wanahitaji umeme mfano vinyozi na mafundi wa kuchomelea na wengine wengi tu.

Sasa unapokata umeme bila ya sababu ya msingi bila ya ratiba kama Kuna mgao Ili watu wajue bado hata ukiwaka unakatika katika mara Kwa mara hawa watu wataishi vipi?

Nchi hii mambo hayawezi kuenda bila ya viboko

R.I.P Magufuli
 
Umeme unakatwa kila ifikapo saa moja na nusu ....Leo hali kadharika, tena wanachagua transformer au service line ya kukata. Hii ni aina ya uhujumu uchumi wa maksudi kabisa!.

Haiwezekani hata mabwawa ya zamani ya Kidatu na Mtera au vinu va gesi visizalishe umeme wa kutosha.
 
Mtu anaona sifa kuitwa mnyonge! Yaani mtu anakuonea halafu anakubeza kwa kukuita mnyonge na wewe unafurahi! Kwa sababu lenyewe lilikuwa jizi kama majizi mengine huko CCM.
sasa mkuu ulitaka atuite matajiri wenzie kutuita wanyonge alimaanisha wewe unaweza dhurumiwa haki yako na tajiri na huna pakumpeleka sasa yeye akachukua jukumu lakutusemea wanyonge au wewe kwenu umeme hua haukatiki au una chuki na magu wa vyeti feki nn
 
Kuna siku niliwahi kumuuliza muajiriwa mmoja wa Tanesco, ambae tunaishi nae jirani, kuwa umeme wanarudisha saa ngapi? akasema hata yeye mwenyewe haelewi.

Hapo ndio nilipojua kuwa sasa kweli mambo yameharibika.

Nikachoka kabisa. Hivi sasa naandika haya, niko gizani. umeme umekata tokea saa mbili. Niko jirani na ofisi ya tanesco, na yenyewe iko gizani.
 
Kuna siku niliwahi kumuuliza muajiriwa mmoja wa Tanesco, ambae tunaishi nae jirani, kuwa umeme wanarudisha saa ngapi? akasema hata yeye mwenyewe haelewi.

Hapo ndio nilipojua kuwa sasa kweli mambo yameharibika.

Nikachoka kabisa. Hivi sasa naandika haya, niko gizani. umeme umekata tokea saa mbili. Niko jirani na ofisi ya tanesco, na yenyewe iko gizani.
2025 mkuu sio mbali andaa kichinjio ukipiga kura usiondoke mpaka mshindi atangazwe kaa umbali wa hizo mita 100 zao mwaka huu tunaanza na hao wenyeviti wao walipita bila kupingwa
 
2025 mkuu sio mbali andaa kichinjio ukipiga kura usiondoke mpaka mshindi atangazwe kaa umbali wa hizo mita 100 zao mwaka huu tunaanza na hao wenyeviti wao walipita bila kupingwa
Dawa ni kuwafuata wandishi wa habari pale pale kituoni, na kuweka wazi kura yako umempa nani wa chama gani. Huu usiri baada ya kupiga kura na kufukuza wapigakura utakoma, maana matokeo yatakapo tangazwa ni lazima yafanane na ushuhuda wa wapigakura.
 
Hamna mtetezi jeshi nalo lipo kimyaaa

Mbona wenzao wa burknafaso watu wamewafurahia sana kushika madaraka
Jeshi letu liko kisiasa zaidi kuliko kitaaluma. Hii hali ya hovyo ilianza baada ya vita vya Kagera, ndipo vikabuniwa vyeo vya kisiasa Jeshini na mtu wa kwanza kuteuliwa alikuwa Moses Mnauye na baadaye kina Komba wakafuata mkumbo.

Jeshini hamna mjeshi mwenye mawazo ya kimapinduzi kama alivyo Ibrahim Traoré anayefuata nyayo za Thomas Sankara. Wajeshi wetu ni watu wa kuridhishwa na vipesa na marupurupu kidogo na kujisikia wamefika kwenye system.

Baada ya hapo ni vitambi kwa kwenda mbele.

Mjeshi akiishaingia kwenye system na vita hakuna, ndio tunaona wanajeshi wanavyopiga raia.
Rejea tukio la juzi, mwananchi anapigwa Knockout kwa kukaribia jeneza la Lowassa....kosa lake ni nini ? Kujipendekeza kwa Lowassa ambaye sasa ni mali ya CCM au Serikali? 😲😮
 
Back
Top Bottom