Sasa ni dhahiri kuwa CHADEMA si Mbowe, Dr. Slaa, Lissu wala Lema. CHADEMA ni imani na haitakufa kirahisi!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,097
2,000
Kwa wasionifahamu (angalau kwa ufahamu wa humu JamiiForums), mimi ni kada kindakindaki wa CCM. Nimejiunga na chama hiki miaka ya mwanzoni mwa 80 baada tu ya kuhitimu shahada yangu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nilisomea sheria. Nikafanya kazi chamani, serikalini na hata kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Naijua nchi hii vyema, hasa kisiasa, ilipotoka-ilipo-na inapokwenda.

Katika utumishi wangu chamani, nimeshiriki kupanga na kutekeleza mipango mingi ya kisiasa. Mipango ya ushindi yenye na isiyo na ushindani. Mipango ya sirini iliyokwenda kutekelezwa sirini na hadharani. Mipango iliyoibakisha CCM madarakani kuanzia uchaguzi wa mwaka 1995 hata sasa. Kuanzia kurejeshwa kwa vyama vingi mwaka 1995, CCM imekuwa ikilenga vyama au chama pinzani chenye nguvu na ku-deal nacho.

Kwa mwaka 1995, NCCR-Mageuzi ililengwa na kusambaratishwa. Mwaka 2000 na 2005 ilikuwa zamu ya CUF. Kuanzia mwaka 2010 hadi sasa, CHADEMA imekuwa target ya CCM kisiasa. Imekuwa mpinzani wa karibu na wa kuharibu wa CCM uchaguzini, uraiani na hata maishani. Wapo makada waliokuwa wakiamini kuwa ili kuisambaratisha CHADEMA, ni lazima kuwasambaratisha viongozi wake. Kuwafanya wasiwe wamoja na hata kucheza na mmojammoja.

Hakika, CCM tulifanikiwa kwa Dr. Slaa na viongozi/wanachama waandamizi wa CHADEMA wengineo. Walinyoosha mikono na kujiunga nasi. Wakabaki akina Mbowe, Lissu, Lema na wengineo. Kazi ikaendelea. Iliendelea katika imani ya kuwa wakidhibitiwa na kumalizwa nguvu zao za kisiasa (zikiwemo na za kiuchumi) CHADEMA itasawajika na kusambaratika kwelikweli. Ilikuwa IMANI POTOFU.

Kama mkongwe wa kisiasa na kiserikali, nimejiridhissha kuwa CHADEMA si viongozi. Ni IMANI inayoishi ndani ya wanachama, wapenzi na mashabiki wao. CHADEMA imejitengeneza katika falsafa ya kiuanaharakati. falsafa ya kupambania usawa, haki, mshikamano, amani na utulivu. Imani hukaa moyoni na rohoni mwa watu. Ni ngumu kuichomoa huko. Wale makada wa CCM waliokuwa wakiamini katika kushughulika na viongozi ili kuidhibiti CHADEMA, sasa wamejiunga nami niliyekuwa nikipingana nao tangu mwanzo.

Sasa wamekuwa wafuasi wa msimamo wangu kuwa siasa ni kushindanisha na kuonesha sera na utekelezaji wake. Katika kuonesha mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, hakuna haja ya kutumika kwa Polisi au chombo chochote cha ulinzi kufanikisha hilo. Kitu halisi huonekana kiurahisi sana. Aliyekuwa Mwenyekiti wetu Mzee Jakaya Kikwete aliwahi kutuusia kuwa tusitegemee polisi hata katika kubishana kwa hoja.

Lakini, bado wapo makada wengi ambao bado wanaamini kuwa CHADEMA ni Mbowe, Lissu na viongozi wengine. Bado wanaamini kuwa 'muunganiko wa tangu enzi' wa CCM na vyombo vya usalama ni nguzo na nyenzo ya ushindi wa chama. Bado wanaamini katika siasa kale za kutumia ulaghai, wizi wa kura, mabavu na vitisho kubaki madarakani-eti tubaki kuwa chamadola. Wanajidanganya.

Utafika wakati, vyombo vya ulizi na usalama vitatamani kusikia kwanza sera bila hela na kushawishiwa na ahadi bila zawadi. Vitatamani kuona ushindani wa nje na ndani ya uwanja wa kisiasa kabla ya kuelendelea kulinda maslahi ya nchi badala ya chama. Vitatuacha solemba tukilia na kusaga meno. Tuoneshe maendeleo na maendeleo yaseme tukiwa tuko kimya. Na, imani ya wananchi kwa upinzani itapungua kwa kasi.

Wasiojulikana sasa wamejulikana?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
 
afsa

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
1,966
2,000
Kingai, Aziz, Goodluck, Mahita na Jumanne ndo wale wasiojulikana makada wa CCM tawi la dola. Hawa watu wametuharibia Sana CCM. Wanajali matumbo Yao na ya viongozi kuliko maslahi ya Taifa. Imani ya kuikataa CCM na viashiria vyake vyote ni kubwa Sana mtaani. Kuwashughulikia viongozi wa chadema ni sawa na kujilisha upepo.
 
pappilon

JF-Expert Member
Jan 27, 2015
3,093

Kifikiria wa matumbo zaidi kuliko kichwa kama wanacho lkini ndo kinasababisha hayo yote wako radhi kupindisha mambo kwa kuwasifia viongozi katika maamuzi yasiyo na maana yoyote ili matumbo yao yajae...nio Arusha kwa Sasa...kwa hii Hali ninayoiona kisiasa na kiuchumi vyama vya upinzani wakizichanga karata zao vizuri 2025. Wabunge wa upinzani wataingi wengi Sana bungeni
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
53,554
2,000
Kifikiria wa matumbo zaidi kuliko kichwa...kama wanacho lkini ndo kinasababisha hayo yote...wako radhi kupindisha mambo kwa kuwasifia viongozi katika maamuzi yasiyo na maana yoyote ili matumbo yao yajae...nio Arusha kwa Sasa...kwa hii Hali ninayoiona kisiasa na kiuchumi vyama vya upinzani wakizichanga karata zao vizuri 2025...wabunge wa upinzani wataingi wengi Sana bungeni
CCM ni genge la matapeli haswa
 
Diwani

JF-Expert Member
Oct 25, 2014
2,012
2,000
Siasa lazima iishi kwenye mioyo ya watu; lakini siasa zenye maana sio upumbavu
 
MAGALEMWA

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
6,352
2,000
@VUTA NIKUVUTE Hujagusia kesi ya Mbowe. Vipi haijawakwama kooni? Hao BAVICHA, BAWACHA nao vipi naona wanadunda tu?
Mabeberu wamecharuka kuhusu Mbowe, kodi za watu wao zinatumika ndivyo sivyo na dola ya CCM. Inabidi tuwatose kwa maana sisi ni masikini jeuri.

Ila kupaa kwa bei za mahitaji muhimu imekuwa noma, sijui na hilo mtalisambalitishaje?

VUTA UVUTIKE
 
Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
7,527
2,000
Wasiojulilana ambao Bado wapo sirini wasijekuwa wageni wako baada ya kuwapa ushauri wa kweli wanaougopa na wasiokuwa tayari kuusikiaasikioni mwao🤔.
 
Tardy

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
797
1,000
Kingai, Aziz, Goodluck, Mahita na Jumanne ndo wale wasiojulikana makada wa CCM tawi la dola. Hawa watu wametuharibia Sana CCM. Wanajali matumbo Yao na ya viongozi kuliko maslahi ya Taifa. Imani ya kuikataa CCM na viashiria vyake vyote ni kubwa Sana mtaani. Kuwashughulikia viongozi wa chadema ni sawa na kujilisha upepo.
Kwanini watajwe hao?
Walipata amri kwanani?
Chama kinatamko gani?
Dawa ni
Kofia moja ya Urais na chama kiwe na mwenyekiti.
 
PETER THE ROCK

Senior Member
Feb 17, 2014
157
250
Nakuunga mkono kwa maana kuwa mimi nijiunga Tanu mwaka 1968 na CCM mwaka 1977 nimesoma shule nzuri. Mchango wangu kuelekea uamuzi wa CCM kukubali sera ya vyama vingi upo. Nyerere alikuwa binadamu mwenye elimu, hekima, busara na upeo wa hali ya juu Kila kiongozi angekuwa anafikiria mbali na siyo tumbo lake, matumbo ya ndugu au rafiki zake tungekuwa mbali sana. Nyerere alijali sana damu ya mtu.

Tujifunze namna ya kuendesha nchi kistaarabu. Hata Simba na Yanga hawapotezi viongozi wa timu pinzani, wanatafuta wachezaji bora ili kushinda msimu husika.Tanzania ni Taifa kubwa tukiwa pamoja. Hili siyo Taifa la kujifunza kutoka Rwanda au Uganda. Tuwe na aibu tusifanye mambo ya ovyo. Historia itatusuta. Nakushukuru sana kwa andiko lako.
 
Drifter

JF-Expert Member
Jan 4, 2010
3,407
2,000
Siasa lazima iishi kwenye mioyo ya watu; lakini siasa zenye maana sio upumbavu
Itasaidia zaidi ukielimisha, angalau kwa ufupi, kuhusu “siasa zenye maana”.

Isije ikawa kila mtu ana tafsiri yake kama vile sifa ya “gaidi/terrorist” isivyo na muafaka dunia nzima.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
91,042
2,000
Kwa wasionifahamu (angalau kwa ufahamu wa humu JamiiForums), mimi ni kada kindakindaki wa CCM. Nimejiunga na chama hiki miaka ya mwanzoni mwa 80 baada tu ya kuhitimu shahada yangu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nilisomea sheria. Nikafanya kazi chamani, serikalini na hata kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Naijua nchi hii vyema, hasa kisiasa, ilipotoka-ilipo-na inapokwenda.

Katika utumishi wangu chamani, nimeshiriki kupanga na kutekeleza mipango mingi ya kisiasa. Mipango ya ushindi yenye na isiyo na ushindani. Mipango ya sirini iliyokwenda kutekelezwa sirini na hadharani. Mipango iliyoibakisha CCM madarakani kuanzia uchaguzi wa mwaka 1995 hata sasa. Kuanzia kurejeshwa kwa vyama vingi mwaka 1995, CCM imekuwa ikilenga vyama au chama pinzani chenye nguvu na ku-deal nacho.

Kwa mwaka 1995, NCCR-Mageuzi ililengwa na kusambaratishwa. Mwaka 2000 na 2005 ilikuwa zamu ya CUF. Kuanzia mwaka 2010 hadi sasa, CHADEMA imekuwa target ya CCM kisiasa. Imekuwa mpinzani wa karibu na wa kuharibu wa CCM uchaguzini, uraiani na hata maishani. Wapo makada waliokuwa wakiamini kuwa ili kuisambaratisha CHADEMA, ni lazima kuwasambaratisha viongozi wake. Kuwafanya wasiwe wamoja na hata kucheza na mmojammoja.

Hakika, CCM tulifanikiwa kwa Dr. Slaa na viongozi/wanachama waandamizi wa CHADEMA wengineo. Walinyoosha mikono na kujiunga nasi. Wakabaki akina Mbowe, Lissu, Lema na wengineo. Kazi ikaendelea. Iliendelea katika imani ya kuwa wakidhibitiwa na kumalizwa nguvu zao za kisiasa (zikiwemo na za kiuchumi) CHADEMA itasawajika na kusambaratika kwelikweli. Ilikuwa IMANI POTOFU.

Kama mkongwe wa kisiasa na kiserikali, nimejiridhissha kuwa CHADEMA si viongozi. Ni IMANI inayoishi ndani ya wanachama, wapenzi na mashabiki wao. CHADEMA imejitengeneza katika falsafa ya kiuanaharakati. falsafa ya kupambania usawa, haki, mshikamano, amani na utulivu. Imani hukaa moyoni na rohoni mwa watu. Ni ngumu kuichomoa huko. Wale makada wa CCM waliokuwa wakiamini katika kushughulika na viongozi ili kuidhibiti CHADEMA, sasa wamejiunga nami niliyekuwa nikipingana nao tangu mwanzo.

Sasa wamekuwa wafuasi wa msimamo wangu kuwa siasa ni kushindanisha na kuonesha sera na utekelezaji wake. Katika kuonesha mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, hakuna haja ya kutumika kwa Polisi au chombo chochote cha ulinzi kufanikisha hilo. Kitu halisi huonekana kiurahisi sana. Aliyekuwa Mwenyekiti wetu Mzee Jakaya Kikwete aliwahi kutuusia kuwa tusitegemee polisi hata katika kubishana kwa hoja.

Lakini, bado wapo makada wengi ambao bado wanaamini kuwa CHADEMA ni Mbowe, Lissu na viongozi wengine. Bado wanaamini kuwa 'muunganiko wa tangu enzi' wa CCM na vyombo vya usalama ni nguzo na nyenzo ya ushindi wa chama. Bado wanaamini katika siasa kale za kutumia ulaghai, wizi wa kura, mabavu na vitisho kubaki madarakani-eti tubaki kuwa chamadola. Wanajidanganya.

Utafika wakati, vyombo vya ulizi na usalama vitatamani kusikia kwanza sera bila hela na kushawishiwa na ahadi bila zawadi. Vitatamani kuona ushindani wa nje na ndani ya uwanja wa kisiasa kabla ya kuelendelea kulinda maslahi ya nchi badala ya chama. Vitatuacha solemba tukilia na kusaga meno. Tuoneshe maendeleo na maendeleo yaseme tukiwa tuko kimya. Na, imani ya wananchi kwa upinzani itapungua kwa kasi.

Wasiojulikana sasa wamejulikana?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
FB_IMG_1574277425198.jpg
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,377
2,000
Kimsingi ccm hapo ilipo inapambana na wakati, ni kawaida kila kizazi kuwa na mapenzi ya kitu fulani. Ccm sio chama cha kizazi hiki, hii inapelekra kunajisi chaguzi za nchi hii ili ibaka madarakani kwa shuruti. Hapo walipo ccm wameshajua kuwa hawana ushawishi tena kwa kizazi hiki. Ndio maana hawataki wapinzani hasa cdm wafanye mikutano ya hadhara, kwani wanajua fika cdm ndio inayokubalika na kizazi hiki.

Sasa hivi wapinzani hasa cdm wamejitoa kushiriki chaguzi zote, hii imepelekea chaguzi kukosa mvuto na kuwa na wapiga kura wachache sana. Rejea chaguzi kadhaa za marudio, na kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la ngorongoro zinazoendelea hivi sasa. Na iwapo wapinzani watasusia chaguzi zote iwapo hakuna mabadiliko ya tume ya uchaguzi na katiba mpya, vituo vya kura havitakuwa na wapiga kura tena hasa vijana, kwani ccm ni chama cha wazee. Hivyo CCM ijiandae kung'olewa madarakani kwa machafuko.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom