Sasa ni dhahiri kuwa CHADEMA si Mbowe, Dr. Slaa, Lissu wala Lema. CHADEMA ni imani na haitakufa kirahisi!

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
38,992
2,000
Wasiojulikana Out
.
20211203_205020.jpg
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
21,500
2,000
Leo umekuwa muwazi kweli. Heshima kwako mkuu.

Andiko lako linastahili 'rejoinder' yenye nguvu za hoja. Pengine tutapata muda na nguvu kuitendea haki mada yako hii mhimu huko mbele ya safari.

Kuna watu, tuliipenda sana CCM kikiwa chama cha wakulima na wafanya kazi; sasa kimekuwa chama ambacho ni adui mkubwa wa taifa letu! CCM kimegeuka kujiona kuwepo kwacho ni muhimu zaidi kuliko uwepo wa taifa letu, ndiyo maana wamejiingiza kwenye kulihujumu taifa hili.

Nyinyi wanachama wachache mliobaki huko mnaoona udhaifu huu wa chama chenu mmeshindwa kuwa na msaada wa kubadili mwelekeo wa chama chenu huko ndani kwa ndani; kwa hiyo iliyobaki ni hukumu ya wananchi tu, na wala siyo hukumu ya vyombo vya ulinzi wala taasisi zingine zilizotekwa na chama chenu ziwatumikie nyinyi.

Pamoja na kusema CHADEMA si viongozi, lakini ukweli ni kwamba bila ya uwepo wa hao wachache waliokataa kuisujudia CCM, chama hicho kingesambaratika vibaya na lengo la CCM lingetimia.

Sasa hivi uwepo wa Mbowe, Lissu. Msigwa, Sugu. Henche, Mnyika na wengi wengine inawezekana isiwe muhimu sana kama ilivyokuwa huko nyuma kwa vile wananchi wa nchi hii hata wasiokuwa wanachama wa chama chochote cha siasa wametambua uovu wa CCM, na wapo tayari kushirikiana na vyama kama CHADEMA kuiondoa CCM bila kujali ni nani anakiongoza chama hicho, kama ilivyokuwa huko siku za nyuma; mradi tu viongozi hao wawe na uwezo wa kuwaunganisha wananchi kutimiza wajibu wao wa kuilinda nchi yao dhidi ya adui huyu mkubwa CCM.

Hawa viongozi ni lazima wawepo ndani ya CHADEMA kuweza kuendesha harakati hizi mpya za ukombozi wa nchi yetu.
Chadema will stay forever
 

Mwl.RCT

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
10,053
2,000
Naijua nchi hii vyema, hasa kisiasa, ilipotoka-ilipo-na inapokwenda.
Sijawahi kujutia kusoma maandiko yako, maana penye ukweli huwa unazungumza ukweli, Na nyeupe huiita nyeupe, Tofauti na wana_CCM wengine wa hapa JF

🙌

CHADEMA imejitengeneza katika falsafa ya kiuanaharakati. falsafa ya kupambania usawa, haki, mshikamano, amani na utulivu Imani hukaa moyoni na rohoni mwa watu. Ni ngumu kuichomoa huko.

Sasa wamekuwa wafuasi wa msimamo wangu kuwa siasa ni kushindanisha na kuonesha sera na utekelezaji wake.

Utafika wakati, vyombo vya ulizi na usalama vitatamani kusikia kwanza sera bila hela na kushawishiwa na ahadi bila zawadi. Vitatamani kuona ushindani wa nje na ndani ya uwanja wa kisiasa kabla ya kuelendelea kulinda maslahi ya nchi badala ya chama.
Ikiwa nchi ya Ghana imeweza, Na hakika hata tanzania tunaweza, Vyombo vyetu vya usalama wanalakujifunza toka Ghana.
 

Mwl.RCT

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
10,053
2,000
Kuwashughulikia viongozi wa chadema ni sawa na kujilisha upepo.

Mhu 1:14 SUV​

Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo.
 

Mtoto wa Shule

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
8,126
2,000
Kwa wasionifahamu (angalau kwa ufahamu wa humu JamiiForums), mimi ni kada kindakindaki wa CCM. Nimejiunga na chama hiki miaka ya mwanzoni mwa 80 baada tu ya kuhitimu shahada yangu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nilisomea sheria. Nikafanya kazi chamani, serikalini na hata kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Naijua nchi hii vyema, hasa kisiasa, ilipotoka-ilipo-na inapokwenda.

Katika utumishi wangu chamani, nimeshiriki kupanga na kutekeleza mipango mingi ya kisiasa. Mipango ya ushindi yenye na isiyo na ushindani. Mipango ya sirini iliyokwenda kutekelezwa sirini na hadharani. Mipango iliyoibakisha CCM madarakani kuanzia uchaguzi wa mwaka 1995 hata sasa. Kuanzia kurejeshwa kwa vyama vingi mwaka 1995, CCM imekuwa ikilenga vyama au chama pinzani chenye nguvu na ku-deal nacho.

Kwa mwaka 1995, NCCR-Mageuzi ililengwa na kusambaratishwa. Mwaka 2000 na 2005 ilikuwa zamu ya CUF. Kuanzia mwaka 2010 hadi sasa, CHADEMA imekuwa target ya CCM kisiasa. Imekuwa mpinzani wa karibu na wa kuharibu wa CCM uchaguzini, uraiani na hata maishani. Wapo makada waliokuwa wakiamini kuwa ili kuisambaratisha CHADEMA, ni lazima kuwasambaratisha viongozi wake. Kuwafanya wasiwe wamoja na hata kucheza na mmojammoja.

Hakika, CCM tulifanikiwa kwa Dr. Slaa na viongozi/wanachama waandamizi wa CHADEMA wengineo. Walinyoosha mikono na kujiunga nasi. Wakabaki akina Mbowe, Lissu, Lema na wengineo. Kazi ikaendelea. Iliendelea katika imani ya kuwa wakidhibitiwa na kumalizwa nguvu zao za kisiasa (zikiwemo na za kiuchumi) CHADEMA itasawajika na kusambaratika kwelikweli. Ilikuwa IMANI POTOFU.

Kama mkongwe wa kisiasa na kiserikali, nimejiridhissha kuwa CHADEMA si viongozi. Ni IMANI inayoishi ndani ya wanachama, wapenzi na mashabiki wao. CHADEMA imejitengeneza katika falsafa ya kiuanaharakati. falsafa ya kupambania usawa, haki, mshikamano, amani na utulivu. Imani hukaa moyoni na rohoni mwa watu. Ni ngumu kuichomoa huko. Wale makada wa CCM waliokuwa wakiamini katika kushughulika na viongozi ili kuidhibiti CHADEMA, sasa wamejiunga nami niliyekuwa nikipingana nao tangu mwanzo.

Sasa wamekuwa wafuasi wa msimamo wangu kuwa siasa ni kushindanisha na kuonesha sera na utekelezaji wake. Katika kuonesha mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, hakuna haja ya kutumika kwa Polisi au chombo chochote cha ulinzi kufanikisha hilo. Kitu halisi huonekana kiurahisi sana. Aliyekuwa Mwenyekiti wetu Mzee Jakaya Kikwete aliwahi kutuusia kuwa tusitegemee polisi hata katika kubishana kwa hoja.

Lakini, bado wapo makada wengi ambao bado wanaamini kuwa CHADEMA ni Mbowe, Lissu na viongozi wengine. Bado wanaamini kuwa 'muunganiko wa tangu enzi' wa CCM na vyombo vya usalama ni nguzo na nyenzo ya ushindi wa chama. Bado wanaamini katika siasa kale za kutumia ulaghai, wizi wa kura, mabavu na vitisho kubaki madarakani-eti tubaki kuwa chamadola. Wanajidanganya.

Utafika wakati, vyombo vya ulizi na usalama vitatamani kusikia kwanza sera bila hela na kushawishiwa na ahadi bila zawadi. Vitatamani kuona ushindani wa nje na ndani ya uwanja wa kisiasa kabla ya kuelendelea kulinda maslahi ya nchi badala ya chama. Vitatuacha solemba tukilia na kusaga meno. Tuoneshe maendeleo na maendeleo yaseme tukiwa tuko kimya. Na, imani ya wananchi kwa upinzani itapungua kwa kasi.

Wasiojulikana sasa wamejulikana?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
Unatafuta kiki tu za mtandaoni.
 

mweusi asili

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
1,658
2,000
kweli, There's a light at the end of the tunnel...

inafurahisha kuona bado kuna wanaCCM wanaamini kwenye siasa za ushindani wa huru na haki, ukiondoa hili wimbi la miaka hii la machawa wanaojua kusifu na kuabudu CCM haiwezi kusimama kwa hoja bila kutumia dola
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,376
2,000
Hata uchaguzi uliopita mimi bado sikuafiki sana cdm kushiriki na msimamo wangu ule uliufahamu. Nadhani hata nyie mliokuwa na mashaka na mtazamo wangu, mmejiridhisha pasi na shaka kuwa kwa muundo huu wa uchaguzi na tume hii ni kupoteza muda. Kwa tulipofikia sasa bila mabadiliko ya tume ya uchaguzi, na katiba mpya, machafuko pekee ndio njia ya uhakika ya mabadiliko.
Iwapo wapinzani watasusia"?
Nashukuru kwamba huko mwishoni umerekebisha kauli hii...,"Hivyo CCM ijiandae kung'olewa madarakani kwa machafukoivyo"

Sioni kamwe ni kwa jinsi gani chama kama CHADEMA kitashiriki tena uchaguzi wa aina yoyote ile bila ya uwepo wa Tume huru ya Uchaguzi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom