Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,669
- 7,556
Wewe kama ni mmiliki wa Channel ya YouTube au mmiliki wa Website na unapata pesa kwa njia ya Google Adsense basi jua sasa hivi TRA wanakata Kodi mpaka huko YouTube na kwenye Websites kwa pesa unayokusanya kupitia Google AdSense. Hivyo uwezi kutoa pesa mpaka uwe na TIN namba pia, tofauti na zamani Google walikuwa wanataka kitambulisho cha NIDA, Leseni ya udereva na Passport tu na anuani ya makazi.
Ila mpaka mwaka huu 2025 naona TRA wamekuwa makini na kuongeza ukusanyaji kodi mpaka mitandao, na hii haina muda mrefu sana itakuwa imeeanza miezi ya June, July, August au September hapa katikati, maana mimi mwezi May 2025, nilichukua pesa Google AdSense bila kuombwa TIN Number. Leo nimepita kuangalia naona wanaomba niweke TIN Number au namba ya mlipa Kodi au cheti cha mlipa Kodi.