Sangara Ziwa Victoria: Ni Baraka kwa Uchumi au Laana kwa Ikolojia ya Samaki wetu wa Asili?

Jephta2003

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2008
Posts
6,721
Reaction score
6,590
Habari za muda huu wana-JF,

Nimekuwa nikifanya tafakari ya kina juu ya hali ya Ziwa Victoria tangu miaka ya 1980 hadi sasa. Wote tunajua kuwa katika miaka ya 1950, uamuzi ulifanywa wa kumwingiza Sangara (Nile Perch) ndani ya Ziwa Victoria akitokea Ziwa Albert na Mto Nile nchini Uganda.

Lengo la wakati ule lilikuwa ni kukuza biashara na michezo ya uvuvi. Lakini leo hii, tunashuhudia mambo mawili mazito:

  1. Kutoweka kwa Samaki wa Asili: Sangara amemeza zaidi ya spishi 200 za samaki wa asili (kama Furu), hali iliyovuruga mfumo wa usafi wa maji ziwani.
  2. Kupungua kwa Samaki kwa Kasi: Licha ya Sangara kuleta viwanda vya minofu (fillets) na fedha za kigeni, kwa sasa samaki wamepungua sana kulinganisha na miaka ya 1984.

Maswali yangu kwa wadau:

  • Je, uamuzi wa kumleta Sangara ulikuwa ni wa busara kiuchumi au tuliharibu urithi wetu wa asili kwa faida ya muda mfupi?
  • Nini kifanyike sasa ili kurejesha utajiri wa ziwa letu? Je, tufunge ziwa kwa muda (Closed Season)? Au tukaze kamba kwenye kuzuia nyavu haramu?

Nawasilisha hoja ili tujifunze na pengine mamlaka husika zione maoni yetu.
 
Sangara ni mhamiaji aliyeletwa, kaja na kuanza kuwala samaki wenyeji, kawala hasa na sasa anatawala ziwa hilo. Kashindwa kummaliza sato, sato bado anapatikana. Pamoja na ubabe wa sangara ndio samaki mwenye minofu na soko lake ni kubwa
 
1772679112298.jpeg

View: https://youtu.be/mwVgLi0cvfo
 
Changamoto inayoendelea ziwa Victoria ni Uzembe wa watendaji wetu.Binadamu tumepewa mamlaka ya kuitawala Dunia, Hivyo umakini ukiwepo akuna kinacho haribika- Kuna nchi nyingi tu zimepandikiza Samaki wageni katika mito/Maziwa Yao na Maisha yana kwenda kama kawaida.(1) 100% Inawezekana kuongeza wingi wa Sato ziwani na uwepo wa Wingi wa Sato ndo pia Wingi wa uwepo wa Sangara. Sato wakiwa wengi ,Sangara nao Wanazaliana kwa wingi na pia kuwa na size kubwa na Zipo njia raisi za kuongeza sato ziwani ambazo Serikali na watahalamu waliopo wanazijua na wanaziweza lakini Vipaumbele vya Serikali yetu ni Siasa na sio Sayansi na Tekenolojia. Viwanda vya kuchakata minofu ya Samaki Vinaendelea kufungwa na mamia ya ajira Kanda ya ziwa Kila kukicha zinapotea- na kuna Mawaziri, Makatibu wakuu na Wakurugenzi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wanaaga Familia zao kila kukicha kuwa wanaenda Kazini lakini akuna wanachokifanya so ni kama awapo!!! Uzembe wanaofanya kila kukicha haya ndo matokea yake (2) Magugu Maji pia yanapunguza Oxygen na hivyo kufanya mazingira ya Samaki ziwani yasiwe rafiki nayo haya yanapunguza uwingi wa samaki wa aina zote-Kuna Nchi zaidi ya 5 Magugu maji yanatumika kama malighafi ya Bidhaa mbalimbali zikiwemo pedi za Kike na kuzalisha ajira za kudumu mamilioni kadhaa.Sisi tupo tuna Lia Lia TU!. Kuna maelfu ya Watanzania waliopo karibu na hili ziwa Awana ata maji ya kutumia 😭.- Waje tuwape mwarobaini wa kuongeza samaki ziwani na kufanya magugu maji kuwa zao la Biashara na kuongeza ajira kwenye mikoa ya lake zone. YES IT CAN BE DONE JUST PLAY YOUR PART- JK Nyerere
 
Attachments

  • images (78).jpeg
    images (78).jpeg
    48.8 KB · Views: 4
  • images (77).jpeg
    images (77).jpeg
    38.7 KB · Views: 4
Nembe, gogogo, ningu, furu, joa etc ni baadhi ya samaki zilizopendwa sana na jamii ya kanda ya ziwa ila sasa hazipo. Anyway booming ya biashara ya viwanda vya samaki(sangara) miaka ya 90s na early 2000s ilinyanyua sana uchumi wa kanda ya ziwa.
 
Mimi ni mtoto wa kanda ya ziwa. Nimekua nikitazama mawimbi ya Ziwa Victoria yakipiga fukwe za Musoma, na nimeona kwa macho yangu mabadiliko ya kutisha na mengine nmesimuliwa kuanzia miaka ya 1950 hadi leo.

Wakati wataalamu wa zamani wakisifu kuingizwa kwa Sangara (Nile Perch) kama "mapinduzi ya kiuchumi," mimi nasimama hapa kusema ukweli mchungu: Huu ulikuwa moja ya uamuzi mbaya zaidi wa kimazingira kuwahi kufanywa katika historia ya Afrika Mashariki.

Tuliaminishwa kuwa Sangara ilipandikizwa ili kukuza uchumi Kupitia shughuli za uvuvi. Lakini hii ilikuja na gharama kubwa ambazo tutalipa Kwa miaka yote iliyobakia.

Sangara ni samaki mla nyama (carnivorous) anaishi Kwa kula samaki wengine. Tangu alipoingizwa kutokea Ziwa Albert, amemeza zaidi ya spishi 200 za samaki wa asili.

Samaki hao hawakuwa tu samaki wa chakula; walikuwa "wafanya usafi" wa ziwa. Walikula mimea (phytoplankton) na kuzuia uchafu.

Leo hii, Ziwa Victoria lina kiwango kikubwa cha uchafu na upungufu wa mwanga na kiwango kikubwa Cha turbidity kuliko maziwa mengine kama Tanganyika na Nyasa. Unaweza kudhani ni kwa sababu Victoria ni ziwa lenye kina kifupi kuliko mengine tajwa, bali ni kwa sababu tulimleta "kiumbe" aliyewala walinzi wa mazingira ya maji.

Siyo nadharia; mimi ni mwathirika wa hali hii. Baba yangu alifanya kazi kwenye viwanda vya kuchakata minofu ya samaki mkoani Mara. Nakumbuka miaka ya nyuma, viwanda kama Nile Perch, Mara Fish, na Kwa Obeto vilikuwa vikifanya kazi usiku na mchana (shift ya mchana na usiku).

Mji wa Musoma ulichangamka, samaki walikuwa wengi, na kila mmoja aliona fursa nmeshuhudia watu wengi wakitajirika Kupitia biashara ya Sangara mfano Chikwakala na wengine wengi. Lakini kuanzia mwaka 2010, kilele cha mafanikio kilianza kuporomoka.

2010 - 2012: Shift za usiku zilikufa. Viwanda vilianza kufanya kazi mchana pekee.

2013: Uzalishaji ulishuka hadi siku tatu kwa wiki kutegemea upatikanaji wa samaki.

2014: Kiwanda cha Nile Perch kilianza kupunguza wafanyakazi kwa kasi. Hapo ndipo familia yangu ilipopoteza mhimili wake—baba yangu alipoteza kazi.

Hadi tunavyozungumza sasa, viwanda vyote nilivyotaja vimefungwa. Musoma imebaki na magofu ya majengo ya viwanda. Huu ni uthibitisho kuwa uchumi wa Sangara ulikuwa wa "muda mfupi" (temporary achievement) kwa sababu haukuwa na mizizi ya mazingira na udhibiti madhubuti wa uzalishaji (total control of production).

Badala ya kuingiza spishi ngeni (exotic species) kwenye maji ya asili na kuharibu mfumo wa ikolojia, tungepaswa kuwekeza kwenye Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba (Cage Culture).

Laiti tungeanza na Cage Culture tangu zaman, tungekuwa na uwezo wa kudhibiti kile samaki wanakula bila kuathiri spishi nyingine.

Leo hii tunaona wafugaji wa vizimba wakivuna tani 2 kila siku kwa uhakika. Tungekuwa na viwanda vinavyofanya kazi mwaka mzima bila kutegemea "bahati" ya ziwani.

Tungebakiza samaki wetu wa asili wanaokula mwani, na ziwa letu lingebaki kuwa safi kama Tanganyika.

Uamuzi wa miaka ya 1950 uliangalia tumbo la wakati ule na kusahau uhai wa ziwa kwa vizazi vijavyo. Tumeshuhudia kutoweka kwa spishi, kuchafuliwa kwa ziwa, na hatimaye kuanguka kwa viwanda vilivyoajiri maelfu ya watu mkoani Mara na kanda ya ziwa Kwa ujumla.

Somo ni moja: Huwezi kushinda vita dhidi ya asili. Tunahitaji kurejea kwenye sayansi ya ufugaji wa kisasa (Cage Culture) ili kuokoa kilichobaki Kwa ajili ya vizazi vijavyo, badala ya kuendelea kutegemea mfumo uliovunjika.
 
Maziwa mengi tu yana hali mbaya kwenye uvuvi.Hata huko Tanganyika,kilio ni kikubwa samaki hakuna licha ya kufunga ziwa mara kadhaa.

Ni,muda wa wataalamu wetu kufanyakazi kisayansi Ili kupata samaki wengi na kurudisha species zinazo taka kutoweka.Mambo yakiwa hivi hivi Kuna kizazi kitaishia kusoma kwenye vitabu au simulizi juu ya aina Fulani za samaki kwamba walikuwepo
 
Mimi ni mtoto wa kanda ya ziwa. Nimekua nikitazama mawimbi ya Ziwa Victoria yakipiga fukwe za Musoma, na nimeona kwa macho yangu mabadiliko ya kutisha na mengine nmesimuliwa kuanzia miaka ya 1950 hadi leo.

Wakati wataalamu wa zamani wakisifu kuingizwa kwa Sangara (Nile Perch) kama "mapinduzi ya kiuchumi," mimi nasimama hapa kusema ukweli mchungu: Huu ulikuwa moja ya uamuzi mbaya zaidi wa kimazingira kuwahi kufanywa katika historia ya Afrika Mashariki.

Tuliaminishwa kuwa Sangara ilipandikizwa ili kukuza uchumi Kupitia shughuli za uvuvi. Lakini hii ilikuja na gharama kubwa ambazo tutalipa Kwa miaka yote iliyobakia.

Sangara ni samaki mla nyama (carnivorous) anaishi Kwa kula samaki wengine. Tangu alipoingizwa kutokea Ziwa Albert, amemeza zaidi ya spishi 200 za samaki wa asili.

Samaki hao hawakuwa tu samaki wa chakula; walikuwa "wafanya usafi" wa ziwa. Walikula mimea (phytoplankton) na kuzuia uchafu.

Leo hii, Ziwa Victoria lina kiwango kikubwa cha uchafu na upungufu wa mwanga na kiwango kikubwa Cha turbidity kuliko maziwa mengine kama Tanganyika na Nyasa. Unaweza kudhani ni kwa sababu Victoria ni ziwa lenye kina kifupi kuliko mengine tajwa, bali ni kwa sababu tulimleta "kiumbe" aliyewala walinzi wa mazingira ya maji.

Siyo nadharia; mimi ni mwathirika wa hali hii. Baba yangu alifanya kazi kwenye viwanda vya kuchakata minofu ya samaki mkoani Mara. Nakumbuka miaka ya nyuma, viwanda kama Nile Perch, Mara Fish, na Kwa Obeto vilikuwa vikifanya kazi usiku na mchana (shift ya mchana na usiku).

Mji wa Musoma ulichangamka, samaki walikuwa wengi, na kila mmoja aliona fursa nmeshuhudia watu wengi wakitajirika Kupitia biashara ya Sangara mfano Chikwakala na wengine wengi. Lakini kuanzia mwaka 2010, kilele cha mafanikio kilianza kuporomoka.

2010 - 2012: Shift za usiku zilikufa. Viwanda vilianza kufanya kazi mchana pekee.

2013: Uzalishaji ulishuka hadi siku tatu kwa wiki kutegemea upatikanaji wa samaki.

2014: Kiwanda cha Nile Perch kilianza kupunguza wafanyakazi kwa kasi. Hapo ndipo familia yangu ilipopoteza mhimili wake—baba yangu alipoteza kazi.

Hadi tunavyozungumza sasa, viwanda vyote nilivyotaja vimefungwa. Musoma imebaki na magofu ya majengo ya viwanda. Huu ni uthibitisho kuwa uchumi wa Sangara ulikuwa wa "muda mfupi" (temporary achievement) kwa sababu haukuwa na mizizi ya mazingira na udhibiti madhubuti wa uzalishaji (total control of production).

Badala ya kuingiza spishi ngeni (exotic species) kwenye maji ya asili na kuharibu mfumo wa ikolojia, tungepaswa kuwekeza kwenye Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba (Cage Culture).

Laiti tungeanza na Cage Culture tangu zaman, tungekuwa na uwezo wa kudhibiti kile samaki wanakula bila kuathiri spishi nyingine.

Leo hii tunaona wafugaji wa vizimba wakivuna tani 2 kila siku kwa uhakika. Tungekuwa na viwanda vinavyofanya kazi mwaka mzima bila kutegemea "bahati" ya ziwani.

Tungebakiza samaki wetu wa asili wanaokula mwani, na ziwa letu lingebaki kuwa safi kama Tanganyika.

Uamuzi wa miaka ya 1950 uliangalia tumbo la wakati ule na kusahau uhai wa ziwa kwa vizazi vijavyo. Tumeshuhudia kutoweka kwa spishi, kuchafuliwa kwa ziwa, na hatimaye kuanguka kwa viwanda vilivyoajiri maelfu ya watu mkoani Mara na kanda ya ziwa Kwa ujumla.

Somo ni moja: Huwezi kushinda vita dhidi ya asili. Tunahitaji kurejea kwenye sayansi ya ufugaji wa kisasa (Cage Culture) ili kuokoa kilichobaki Kwa ajili ya vizazi vijavyo, badala ya kuendelea kutegemea mfumo uliovunjika.
Umenyoosha vyema kabisa.
 
Changamoto inayoendelea ziwa Victoria ni Uzembe wa watendaji wetu.Binadamu tumepewa mamlaka ya kuitawala Dunia, Hivyo umakini ukiwepo akuna kinacho haribika- Kuna nchi nyingi tu zimepandikiza Samaki wageni katika mito/Maziwa Yao na Maisha yana kwenda kama kawaida.(1) 100% Inawezekana kuongeza wingi wa Sato ziwani na uwepo wa Wingi wa Sato ndo pia Wingi wa uwepo wa Sangara. Sato wakiwa wengi ,Sangara nao Wanazaliana kwa wingi na pia kuwa na size kubwa na Zipo njia raisi za kuongeza sato ziwani ambazo Serikali na watahalamu waliopo wanazijua na wanaziweza lakini Vipaumbele vya Serikali yetu ni Siasa na sio Sayansi na Tekenolojia. Viwanda vya kuchakata minofu ya Samaki Vinaendelea kufungwa na mamia ya ajira Kanda ya ziwa Kila kukicha zinapotea- na kuna Mawaziri, Makatibu wakuu na Wakurugenzi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wanaaga Familia zao kila kukicha kuwa wanaenda Kazini lakini akuna wanachokifanya so ni kama awapo!!! Uzembe wanaofanya kila kukicha haya ndo matokea yake (2) Magugu Maji pia yanapunguza Oxygen na hivyo kufanya mazingira ya Samaki ziwani yasiwe rafiki nayo haya yanapunguza uwingi wa samaki wa aina zote-Kuna Nchi zaidi ya 5 Magugu maji yanatumika kama malighafi ya Bidhaa mbalimbali zikiwemo pedi za Kike na kuzalisha ajira za kudumu mamilioni kadhaa.Sisi tupo tuna Lia Lia TU!. Kuna maelfu ya Watanzania waliopo karibu na hili ziwa Awana ata maji ya kutumia 😭.- Waje tuwape mwarobaini wa kuongeza samaki ziwani na kufanya magugu maji kuwa zao la Biashara na kuongeza ajira kwenye mikoa ya lake zone. YES IT CAN BE DONE JUST PLAY YOUR PART- JK Nyerere
Kumbe magugu maji yana dili? sasa mbona huku kwetu yanatusumbua na hatujui cha kufanya
 
Duhh babu yangu kafanya kazi miaka mingi sana Nile perch ya mwanza! Bahati mbaya alishafariki huenda ningejifunza kitu kutoka kwake ila sikuwaza kama haya yote yaliwahi kutokea! Nilijua sangara ni samaki kama sato tu kumbe ni carnivore tu🙆🏽‍♀️
 
Changamoto inayoendelea ziwa Victoria ni Uzembe wa watendaji wetu.Binadamu tumepewa mamlaka ya kuitawala Dunia, Hivyo umakini ukiwepo akuna kinacho haribika- Kuna nchi nyingi tu zimepandikiza Samaki wageni katika mito/Maziwa Yao na Maisha yana kwenda kama kawaida.(1) 100% Inawezekana kuongeza wingi wa Sato ziwani na uwepo wa Wingi wa Sato ndo pia Wingi wa uwepo wa Sangara. Sato wakiwa wengi ,Sangara nao Wanazaliana kwa wingi na pia kuwa na size kubwa na Zipo njia raisi za kuongeza sato ziwani ambazo Serikali na watahalamu waliopo wanazijua na wanaziweza lakini Vipaumbele vya Serikali yetu ni Siasa na sio Sayansi na Tekenolojia. Viwanda vya kuchakata minofu ya Samaki Vinaendelea kufungwa na mamia ya ajira Kanda ya ziwa Kila kukicha zinapotea- na kuna Mawaziri, Makatibu wakuu na Wakurugenzi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wanaaga Familia zao kila kukicha kuwa wanaenda Kazini lakini akuna wanachokifanya so ni kama awapo!!! Uzembe wanaofanya kila kukicha haya ndo matokea yake (2) Magugu Maji pia yanapunguza Oxygen na hivyo kufanya mazingira ya Samaki ziwani yasiwe rafiki nayo haya yanapunguza uwingi wa samaki wa aina zote-Kuna Nchi zaidi ya 5 Magugu maji yanatumika kama malighafi ya Bidhaa mbalimbali zikiwemo pedi za Kike na kuzalisha ajira za kudumu mamilioni kadhaa.Sisi tupo tuna Lia Lia TU!. Kuna maelfu ya Watanzania waliopo karibu na hili ziwa Awana ata maji ya kutumia 😭.- Waje tuwape mwarobaini wa kuongeza samaki ziwani na kufanya magugu maji kuwa zao la Biashara na kuongeza ajira kwenye mikoa ya lake zone. YES IT CAN BE DONE JUST PLAY YOUR PART- JK Nyerere
Mkuu umepita humo humo,asante
 
Nembe, gogogo, ningu, furu, joa etc ni baadhi ya samaki zilizopendwa sana na jamii ya kanda ya ziwa ila sasa hazipo. Anyway booming ya biashara ya viwanda vya samaki(sangara) miaka ya 90s na early 2000s ilinyanyua sana uchumi wa kanda ya ziwa.
Yes ilinyanyua uchumi na kumaliza samaki ziwani,sasa tunafanyaje?
 
Sangara ni mhamiaji aliyeletwa, kaja na kuanza kuwala samaki wenyeji, kawala hasa na sasa anatawala ziwa hilo. Kashindwa kummaliza sato, sato bado anapatikana. Pamoja na ubabe wa sangara ndio samaki mwenye minofu na soko lake ni kubwa
Sangara ni israel
 
Vipe kambale naye apelekwe huko wakaleteane ubabe na sangara tuone nani zaidi ni mbabe, au kambale haishi kwenye maji hayo na hana soko?
 
Yes ilinyanyua uchumi na kumaliza samaki ziwani,sasa tunafanyaje?
Tutumie Technologia zilizopo na zinazotumiwa na nchi zingine zilizokuwa na matatizo kama yetu na ziwa letu kuongeza wingi wa samaki bila kufunga ziwa na pia kutumia magugu maji kama malighafi ya bizaa mbalimbali kama nchi zingine wanavyofanya! Na pia kutumia sayansi pale Sayansi inapohitajika na kutumia Siasa pahala pake. Tujaribu kuwa makini katika maamuzi yetu hasa yale yenye mstakabali wa Maisha yetu na ya vizazi vijavyo. Na kwa kuongezea SANGARA pia Wanaweza fugwa kama Sato! Hivyo Sirikali inaweza anzisha ufugaji wa Sangara na hili kupelekea Ufufuaji wa Viwanda vya Minofu ya Sangara na kurudisha ajira kwa wakazi wa Lake zone na pia kukuza uchumi wa mikoa hii kama hapo zamani. Limeshatufika hivyo atutakiwi kulia Lia. Tufute Machozi tuingie kazini tulete mabadiliko. Twende Kazini
 
Attachments

  • Screenshot_2026-03-05-14-02-00-972_com.android.chrome-edit.jpg
    Screenshot_2026-03-05-14-02-00-972_com.android.chrome-edit.jpg
    116.5 KB · Views: 5
Back
Top Bottom